UVCCM: Magufuli akubalika asilimia 85

UVCCM: Magufuli akubalika asilimia 85

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeonesha mafanikio makubwa kwa mgombea wake wa urais, Dk John Magufuli kukubalika kwa wananchi katika kampeni zake mikoani, huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ukisema mgombea wake, Edward Lowassa anakubalika vivyo hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kusema imefanya tathmini ya mgombea wake urais, Dk. John Magufuli na kubaini kuwa amekubalika kwa asilimia 85 kwenye maeneo aliyopita kufanya kampeni.

Tathmini hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano wa UVCCM, Egla Mamoto kuwa baada ya Dk. Magufuli kuzunguka katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kufanya kampeni CCM imezidi kukubalika zaidi kwa wananchi.

"Wiki mbili zilizopita utafiti wetu ulionesha CCM inakubalika asilimia 78, lakini baada ya Magufuli kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali CCM imekubalika kwa asilimia 85, hii imechangiwa na mambo mengi ukiachilia mbali rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi wa mgombea wetu," alisema.

Alisema kilichosababisha tathmini hiyo kupanda ni kutokana na ilani ya uchaguzi mwaka huu na uwezo mkubwa wa Dk. Magufuli katika kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi.

Mamoto alisema hadi sasa Dk. Magufuli ametembelea mikoa sita ambayo ni Mbeya, Ruvuma, Njombe, Katavi, Rukwa na Mtwara pamoja na majimbo yote yaliyopo katika mikoa katika kampeni ya kuomba wananchi wamchague Oktoba 25, mwaka huu.

Alisema katika mikoa hiyo aliweza kufanya mikutano ya hadhara zaidi ya 49 na mikutano 126 ya barabarani ambayo wananchi walikuwa wakimsimamisha ili wamsalimie na kumueleza matatizo yao.

"Maeneo yote hayo amezunguka kwa kutumia mitumbwi, gari na kutembea kwa miguu kwa zaidi ya kilometa 5,900 na bado matazunguka na kutembea mikoa yote na majimbo yote," alisema.

Lowassa kaingia mitini

Katika hatua nyingine, Mamoto alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilitoa ratiba ili kila mgombea kuwafikia wananchi na kunadai sera zao, lakini baadhi ya wagombea wamekuwa wakienda kinyume cha ratiba.

"Kwa mfano, Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameshaanza kuonesha dalili za kuchoka ma kushindwa kufika katika maeneo aliyohitajika afanye mikutano," alisema.

Katibu huyo alisema Lowassa alitakiwa afike Ludewa (Njombe) na Tunduru (Ruvuma), ambako wananchi walikwisanyika wakimsubiri wamsikilize sera zake lakini hakuonekana.

"Jambo hili limewaudhi wananchi wale na hakika wameapa kutompa kura maana amewadharau, kutokana na kitendo cha yeye kuchagua baadhi ya maeneo muhimu ambayo ndiyo atakayoyafikia tu.

"Hali hiyo imeanza kuwatia mashaka Watanzania kuwa ni mbaguzi, amekosa hoja za kuzisimamia baada ya wimbo wa ufisadi kupamba moto kila kona, ama amechoka au ni uoga uliyowaingia kuona dalili za kutokukubalika," alidai.

Chadema

Pia, alisema tuhuma ambazo zinasambazwa nchi nzima kuwa wao ndiyo wanapanga vurugu kwa kuwachafua Chadema si za kweli.

"CCM ni chama ambacho kinaamini katika maadili, hivi sasa tunajikita katika kutafuta kura na si kukaa na kupanga kufanya vurugu," alisema.

Alisema Chadema wasimtafute mchawi, mchawi wanao wao wenyewe, wao wakae wasubiri ushindi wa kishindo kutoka CCM na kwamba wanaosambaza taarifa hizo wapuuzwe.

Mamoto alisema udhaifu wa wapinzani ndiyo utakaowafanya washindwe katika uchaguzi huu, kwa sababu muda mwingi wanatumia kujitetea na kujisafisha badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.

Mwito kwa Watanzania

Katibu huyo alitoa mwito kwa Watanzania kuwa waungane pamoja bila kutazama tofauti zao za udini, rangi na ukabila na kuwataka watu wanaowagawa mafisadi, wala rushwa na wanaoamini kuwa wanaweza kuwanunua Watanzania wawapuuze.

Ukawa

Katika hatua nyingine, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema utashinda kwa asilimia 80 katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema katika uchaguzi huo hakutakuwa na ushindi wa kupishana kwa asilimia moja au mbili kama ilivyozoeleka na badala yake umoja huo kupitia mgombea wao urais, Edward Lowassa watashinda kwa kishindo.

Mbatia alisema wameendelea kufanya uchunguzi katika kila mahali ambapo hadi sasa wagombea wao wamefika na kuona namna wanavyopokelewa. Alisema umoja huo umejipanga, umejiratibu, umesimamia na kuelekeza vizuri hivyo wana uhakika wa kushinda.

Kampeni

Akizungumzia kuhusu hali ya kampeni za vyama hivyo inayoendelea katika mikoa mbalimbalali nchini, alisema tangu walivyoanza kampeni zao na hali ya kupokelewa kwao kuna matumaini makubwa ya kufanya mabadiliko.

"Kwa namna tunavyopokelewa kuna matumaini makubwa ya kushinda na kufanya mabadiliko kwani kwa umoja wetu tumesimamia mabadiliko," alisema.

Alisema hata kule ambako iliaminika ni ngome za CCM wamekubalika na kubainisha kuwa hiyo ni raundi ya kwanza, lakini vyama vingine vitegemee cheche kwani hizo ni rasharasha.

Mweyekiti huyo alisema mbali na mwanzo huo lakini wamejipanga kuhakikisha Ukawa wanazunguka mikoa yote kwa kugawanyika kuhakikisha wanamnadi mgombea wao na kutangaza sera na ilani yao.

Agenda

Mbatia alisema kuwa pamoja na kuzunguka katika mikoa mbalimbali nchini agenda yao kuu ni sauti ya umma na umoja wa katiba ya wananchi kwani wanahitaji Watanzania wapate katiba wanayoitaka na yenye maridhiano yao.

"Tutaondoa katiba hii iliyoundwa na muungano wa ASP na Tanu kandamizi na tutaleta katiba itakayobadilisha mfumo mzima wa katiba hii kwani maendeleo yanaletwa kwa kujenga mfumo ambao mtu hawezi kuuvunja,"alisema.

Alisema kuwa ilani na agenda yao kubwa ni kuwa na katiba mpya ya Tanzania.

Uchochezi

Akizungumzia hali ya vurugu zinazojitokeza na zilizojitokeza katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Mbatia alisema licha ya ukimya wao wanaona ni vema Serikali ikaona umuhimu wa kuangalia maslahi ya taifa na si ya chama.

"Kuna mambo hapa yametokea yanatia hasira, yanajenga chuki na kusababisha uchochezi katika imani za kidini, ukabila, ukanda, misingi ya itikadi katika vyama vya siasa na kutotenda haki katika kusimamia amani.

"Ndiyo kwanza uchaguzi umeanza sasa mambo haya tukiyaacha ukiangalia bado kuna siku nyingi hadi kuukaribia uchaguzi tunaweza kupata matatizo," alisema.

Alisema katika hali iliyotokea Dar es Salaam juzi, vijana waliojitokeza kufanya vurugu kumpinga Lowassa huku wakijitambulisha kuwa ni vijana wa Chadema lakini cha kushangaza watu wema wamesema si wa chama hicho na badala yake ni vijana waliotengenezwa kufanya vurugu.

"Hali hii ni kama ile iliyojitokeza nchini Kenya kwa uchochezi ambapo mbali na nchi hiyo, pia katika nchi nyingi hali kama hii hutokea mara tu inapotokea chama tawala kinapoondoka madarakani," alisema.

Hata hivyo, alisema kuwa licha ya uwepo wa matukio ya uchochezi lakini Jeshi la Polisi halichukulii hatua jambo ambalo linashangaza.

Alisema kutokana na matukio hayo hadi hivi sasa jopo la wanasheria katika umoja huo tayari wameanza kuchukua vielelezo hivyo kama ushahidi kwani mambo hayo si ya kufumbiwa macho kwani haijulikani kesho itatokea nini.

Pia aliongeza kuwa vitu vyote vinavyojitokeza katika kipindi hiki tayari wamefikisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Polisi lakini la kushangaza havichukuliwi hatua.

"Mfano Agosti 23 wakati CCM inazindua kampeni zake walimaliza saa moja kasoro lakini jana mgombea wetu wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amezidisha dakika 6 tu amekamatwa jamani vitendo hivi vinaongeza chuki," alisema.

Alisema vitendo hivyo vinakiuka sheria na haki za binadamu kwa kiasi kikubwa kutokana na kutawala kwa matusi, kashfa, udhalilishaji unaofanyika katika maeneo mbalimbali na hata vituo vya habari lakini bado havichukuliwi hatua.

Mbatia alisema jambo lingine ambalo waliwahi kuliripoto katika mamlaka husika ni pamoja na kuchanwa kwa mabango ya wagombea wao pamoja na kukamatwa kwa watu wanaobandika mabango katika Mkoa wa Iringa na kukataliwa kwa baadhi ya maeneo kutoyabandika.

Alisema pamoja na mambo hayo yote wasifikiri upole wao na ukimya wao lakini ikifika wakati watasema hapana wamechoka.

"Sisi tunaambia Watanzania wasifanye vurugu pamoja na kuwasimamia vizuri lakini ikifika mahali tutawaachia Watanzania wafanye uamuzi wao. Tayari tumeitaarifu NEC, na wanasheria wetu wanashughulikia mambo haya na tutayapeleka mahakamani," alisema Mbatia.

Aliwataka Watanzania wasichoke na kwamba CCM itakapotangaza uchochezi, uvunjifu wa amani, chuki Ukawa utatangaza amani na kudumisha umoja.

Chanzo: Jambo Leo
 
Itakuwa ajabu la nane la dunia kama Magufuli atashinda kuliko hata JK 2005
 
Simkubali kabisa lowasa, lakini hii habari ya tafiti ni uandaaji wa mazingira fulani ovu, sawasawa na tunachoambiwa na mbowe kwamba zilifanyika tafiti kabla ya kumuuzia lowasa chama.
 
Ukitaka kuthibitisha hilo usitumie ushabiki nenda mtaani waulize kura watampa nani watakuambia. Leo nimekaa maeneo matatu tofauti walio weng wanasema kilichopo vichwani mwa watu sasa mikutanoni wanakwenda kwa Lowasa ila kura watampa Magufuli. Please weka ushabiki pembeni
 
Ukitaka kuthibitisha hilo usitumie ushabiki nenda mtaani waulize kura watampa nani watakuambia. Leo nimekaa maeneo matatu tofauti walio weng wanasema kilichopo vichwani mwa watu sasa mikutanoni wanakwenda kwa Lowasa ila kura watampa Magufuli. Please weka ushabiki pembeni
Kwa uchaguzi huu sioni kama kuna mgombea yeyote anayeweza kupata zaidi ya 60%, do not underestimate these nyumbus. Huo utafiti wa twaweza unazua mashaka.
 
DSC00018.jpg
DSC00020.jpg

jamani hivi UVCCM NDIO TWAWEZA????
EMBU SOMENI VZUR HAYO MAGAZETI!!!!

MTOA POST ACHA UPOTOSHAJI.

HYO KAZ IMEFANYWA NA UVCCM NA SIO TWAWEZA.

CCM ACHENI KUCHEZA NA AKILI ZETU KWA UONGO NA UHUNI WA KUTUMIA MAGAZET YENU KUDANGANYA WATZ.


YAAAN KAMPENI UPIGE WW NA RESEARCH UJIFANYIE WEW NA UJIPE MAJIBU???

NI MAZUZU TU WATAKUBALI HUO UTAFITI WA UVCCM WA WAO KWA WAO.
 
Tafiti zinafanya projection tu na mwishoni kadirio linakuwa chini kidogo ya hapo lakini ukweli unabaki km ulivyo ktk tafiti.
 
ni kwa nini n magazeti ya UHURU NA JAMBO LEO??TENA YA CCM YOTE.ACHENI KUTUMEZESHA MANENO MAJIZI NYIE
 
Ni ndoto za mchana mtu kuzani magufuri atakua raisi, vinginevyo huyo mtu awe alishawahi kuishi milembe
 
Utafiti ni wa UVCCM,tafiti za REPOA NA Twaweza Ccm wanatumia mamilioni ya pesa kuzikwamisha
 
Hakika, lakini hatopata zaidi ya 60%. Kuna kundi kubwa sana la nyumbu ambalo limeapa kutompa kura.

Wamekaa madarakani kwa miaka hamsini matokeo take wamevimbiwa kodi zetu sasa wanatuita malofa,wapumbavu,manyumbu,tunaaangalia kalenda tu,25 octoba watatujua
 
Hivi UVCCM ndio TWAWEZA siku hizi? Acheni propaganda za kijinga dawa yenu ni kwenye sanduku la kura tarehe 25 October.

Tiba
 
Wamekaa madarakani kwa miaka hamsini matokeo take wamevimbiwa kodi zetu sasa wanatuita malofa,wapumbavu,manyumbu,tunaaangalia kalenda tu,25 octoba watatujua
Mbona wamewastahi sana! Nyie ni zaidi ya nyumbu. Kuthibitisha hilo utaona mtakavyobadili uelekeo baada ya uchaguzi.
 
TATHMINI; siku 10 za Kampeni ya Dr John Magufuli.

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli amehitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni yake kwa mikoa 6 ya kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini ambayo ni KATAVI, RUKWA, MBEYA, NJOMBE, RUVUMA na MTWARA.

Katika kampeni zake Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara takribani 49 pamoja na mikutano midogo ya kusalimia wananchi zaidi ya 126 ambapo katika mikutano yote wananchi walijitokeza kwa Maelfu kumsikiliza akiwasilisha Ilani ya CCM ya 2015-2020.

Dr Magufuli ametembea takribani Kilometa 5,900 kwa kutumia gari na maeneo mengine akitembea kwa miguu ili kukutana na Wananchi wa Makundi mbalimbali akinadi sera za CCM.

Tafiti za awali za Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi yalionyesha kuwa CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya asilimia 60, lakini baada ya kuanza kwa Kampeni na mgombea kuzunguka akifanya mikutano mikubwa ya hadhara ambayo imekuwa ikirushwa moja kwa moja (live) kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii na kuwafikia watanzania takribani milioni 30, Umaarufu wa CCM na uwezekano wa kushinda umeongezeka kufikia asilimia 85 (tafiti za ndani)

Mambo yaliyopelekea CCM kuongeza umaarufu wake ni pamoja na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi aliyonayo mgombea wake, pamoja na uwezo mkubwa wa mgombea (Dr Magufuli) katika kutambua na kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa kada zote na maeneo yote ya Mijini na Vijijini.

Ilani ya CCM na namna mgombea anavyoinadi (Body language) imeongeza imani ya wananchi kwa CCM, mfano Dr Magufuli akisema anaichukia rushwa, mwili, haiba na sura yake vinaonyesha kuwa anamaanisha anachokizungumza. Ilani ya CCM imejikita katika kuleta mabadiliko kwa kuondoa Umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa Vijana, kuendeleza Vita dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu, Kuboresha huduma za jamii na kuendeleza Umoja wa Kitaifa pamoja na kudumisha Ulinzi na usalama.

Wakati Umaarufu na kukubalika kwa CCM kunaongezeka, bado inapata upinzani hafifu ktk kampeni zake. Rekodi zenye mashaka za wagombea wao zinazohusisha kashfa za rushwa, ufisadi, utendaji mbovu na uzembe. Hali tete na migogoro ya ndani ya vyama vya Upinzani ambayo imeshika kasi ktk kipindi hiki hasa kuhusu wagombea kwa nafasi ya Urais na baadhi ya majimbo. Hali ya Afya za wagombea wao ambazo zimewafanya kutoweza kufika katika baadhi ya maeneo waliyopanga kufanya mikutano mfano Ludewa na Tunduru ambapo wananchi walishakusanyika na mgombea akashindwa kutokea. Vyama vya upinzani kukosa Ilani madhubuti na hivyo wananchi kupunguza imani yao kwao.

NB;
Katika moja ya utaratibu bora kabisa wa Chama Cha Mapinduzi ni ule wa kujifanyia tathmini katika kila hatua ya mpango ama jambo lake lolote, utaratibu huu umeiwezesha CCM kubaki kuwa relevant na kuendelea kuaminiwa na kupendwa na watanzania walio wengi.
 
jamani hivi UVCCM NDIO TWAWEZA????
EMBU SOMENI VZUR HAYO MAGAZETI!!!!

MTOA POST ACHA UPOTOSHAJI.

HYO KAZ IMEFANYWA NA UVCCM NA SIO TWAWEZA.

CCM ACHENI KUCHEZA NA AKILI ZETU KWA UONGO NA UHUNI WA KUTUMIA MAGAZET YENU KUDANGANYA WATZ.


YAAAN KAMPENI UPIGE WW NA RESEARCH UJIFANYIE WEW NA UJIPE MAJIBU???

NI MAZUZU TU WATAKUBALI HUO UTAFITI WA UVCCM WA WAO KWA WAO.

Ili ufuzu stashahada ya uongo ni lazima udhihirishe kwamba unaweza kujidanganya mwenyewe
 
Back
Top Bottom