aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 776
- 1,121
Naamini kila Mtanzania ana haki ya kuhoji mustakabali wa maendeleo ya kila nyanja katika nchi yetu ya Tanzania.
Kwa mfano: suala la Bandari hivi sasa linazungumzwa karibu na kila Mtanzania,wapo wanaokosoa na wapo ambao wanaona ni sawa Tanzania inahitaji kuingia ubia na Kampuni husika.
Kuna mijadala mingi sana Mitandaoni ambayo inaendelea, lakini nataka niongee kwa upande wa UVCCM ambao ni vijana wa chama cha Mapinduzi.
Hawa vijana baadhi yao wamekuwa vinara kwenye kuzungumza juu ya uhalali wa Tanzania kuingia makubaliano na kampuni ya DP World.
Kwanza,naomba niseme sio kosa kwa vijana wa UVCCM kuunga mkono hata kidogo!
Lakini cha kushangaza ni pale ambapo wanaposhindwa kuieleza jamii manufaa ya kuingia ubia na kampuni hiyo,badala ya kujenga hoja ili iwe ni msaada kwa serikali kuielimisha jamii wao wanashindwa kutetea hoja.
Kwa mfano nimeona wengi wanawauliza swali hili 👇
“Mnasema kuna nchi zimefaidika kama Rwanda na Somalia,je wamenufaika vipi na kabla ya hapo ilikuwaje?
Swali jingine ni Kama ni mkataba mbona wananchi hawakuwa na taarifa wala wabunge?
Swali jingine 👉 tuambieni kifungu gani ambacho kimegusa ushirikiano wa wawekezaji na wananchi ambao watahitaji ajira.
Sasa wanapobandikwa maswali wanashikwa na hasira,kiasi ambacho unahisi huenda huyu mwana UVCCM haelewi kuhusu mambo ya uchumi,au hata hayo makubaliano hakupata kuyasoma ndipo ajimwage Mitandaoni.
Unaweza kuona ni kwanamna gani ambavyo mwana UVCCM kwenye majibizano anajigamba kwamba hata iweje mambo yataenda tu 😢
Kwa maoni yangu ni kwamba hao vijana wasaidiwe namna bora ya kuweza kupambanua masuala mazito ambayo yanagusa mtima wa kila mwananchi.
Kwanza wasome vizuri kama ni mikataba au makubaliano,waelewe kabla ya kutoka hadharani,inakuwa kichekesho kwamba maswali mengine yanajibika wanayobishana Mitandaoni na vijana wenzao wa vyama vingine au wananchi wengine ambao wana mitazamo tofauti.
Kwamba hawa wanatakiwa kutafakari kwanza wakae wakijua kwamba Tanzania kuna Vichwa ambavyo vina uelewa mkubwa sana.
👉 Mwisho kabisa mimi sio mwanachama wa chama chochote na similiki kadi yoyote wala Kura sijawahi kupiga tangu nizaliwe ila ni mdau wa maendeleo tu basi.
Ahsante