UVCCM kuna kasoro

UVCCM kuna kasoro

Naamini kila Mtanzania ana haki ya kuhoji mustakabali wa maendeleo ya kila nyanja katika nchi yetu ya Tanzania.

Kwa mfano: suala la Bandari hivi sasa linazungumzwa karibu na kila Mtanzania,wapo wanaokosoa na wapo ambao wanaona ni sawa Tanzania inahitaji kuingia ubia na Kampuni husika.

Kuna mijadala mingi sana Mitandaoni ambayo inaendelea, lakini nataka niongee kwa upande wa UVCCM ambao ni vijana wa chama cha Mapinduzi.

Hawa vijana baadhi yao wamekuwa vinara kwenye kuzungumza juu ya uhalali wa Tanzania kuingia makubaliano na kampuni ya DP World.

Kwanza,naomba niseme sio kosa kwa vijana wa UVCCM kuunga mkono hata kidogo!

Lakini cha kushangaza ni pale ambapo wanaposhindwa kuieleza jamii manufaa ya kuingia ubia na kampuni hiyo,badala ya kujenga hoja ili iwe ni msaada kwa serikali kuielimisha jamii wao wanashindwa kutetea hoja.

Kwa mfano nimeona wengi wanawauliza swali hili 👇

“Mnasema kuna nchi zimefaidika kama Rwanda na Somalia,je wamenufaika vipi na kabla ya hapo ilikuwaje?

Swali jingine ni Kama ni mkataba mbona wananchi hawakuwa na taarifa wala wabunge?

Swali jingine 👉 tuambieni kifungu gani ambacho kimegusa ushirikiano wa wawekezaji na wananchi ambao watahitaji ajira.

Sasa wanapobandikwa maswali wanashikwa na hasira,kiasi ambacho unahisi huenda huyu mwana UVCCM haelewi kuhusu mambo ya uchumi,au hata hayo makubaliano hakupata kuyasoma ndipo ajimwage Mitandaoni.

Unaweza kuona ni kwanamna gani ambavyo mwana UVCCM kwenye majibizano anajigamba kwamba hata iweje mambo yataenda tu 😢

Kwa maoni yangu ni kwamba hao vijana wasaidiwe namna bora ya kuweza kupambanua masuala mazito ambayo yanagusa mtima wa kila mwananchi.

Kwanza wasome vizuri kama ni mikataba au makubaliano,waelewe kabla ya kutoka hadharani,inakuwa kichekesho kwamba maswali mengine yanajibika wanayobishana Mitandaoni na vijana wenzao wa vyama vingine au wananchi wengine ambao wana mitazamo tofauti.

Kwamba hawa wanatakiwa kutafakari kwanza wakae wakijua kwamba Tanzania kuna Vichwa ambavyo vina uelewa mkubwa sana.

👉 Mwisho kabisa mimi sio mwanachama wa chama chochote na similiki kadi yoyote wala Kura sijawahi kupiga tangu nizaliwe ila ni mdau wa maendeleo tu basi.

Ahsante
Hakuna uvccm atakaye kuja kujibu hizi hoja, vijana walio huko wanavizia uteuzi,usije ukawaza watakuja kujibu hoja zako
 
Haha uwoga ulipitiliza = utii. Hii kitu Aliitengeneza nyerere kwa sababu tofauti kipindi hiko but then mwenyewe akaja kukemea at one time alipotoka madarakani akianza kipiga vita uoga ulipitiliza maana imetengeneza raia waoga, uwoga umejaa unafki, unafki umetengeza viongozi wabovu

Sisemi kiongozi atukanwe, akosolewe. Uvccm hamna uwezo wa kumkosoa kingozi wenu hata akosee vipi
Si kweli....

Tunawakosoa VIONGOZI wetu katika vikao stahiki na vikao halali kikatiba...

Sisi kweli ni watiifu....hatukosoani hadharani......

PRAISE IN PUBLIC

CRITICIZE IN CLOSETS[emoji1787]
 
TUNAHITAJI UWEKEZAJI KWENYE BANDARI, ILI UFANISI UONGEZEKE, TUINUE UCHUMI, TUTOE AJIRA ZA KUTOSHA, TUSOMESHE WANAFUNZI WENGI, NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA JAMII.
UWEKEZAJII HUUU NI MUHIMU SAANA ACHENI KUJIPA UJUAJI WA KIZAMANII.
Makubaliano au Mkataba? Terms zao zikoje?
 
Hakuna uvccm atakaye kuja kujibu hizi hoja, vijana walio huko wanavizia uteuzi,usije ukawaza watakuja kujibu hoja zako
Unatudogosha sana....

Hivi sisi wote UVCCM tunaweza kuteuliwa katika hizo nafasi chache ?!!!![emoji1787]

Tatizo lenu hamtaki kukiri kuwa kazi yetu ni kukijenga chama....si hadharani kukikashifu na VIONGOZI wake....

Huo ni MWIKO kwetu...

Karibu Al Kasus hapa "Mandi" Lumumba [emoji120]
 
Unatudogosha sana....

Hivi sisi wote UVCCM tunaweza kuteuliwa katika hizo nafasi chache ?!!!![emoji1787]

Tatizo lenu hamtaki kukiri kuwa kazi yetu ni kukijenga chama....si hadharani kukikashifu na VIONGOZI wake....

Huo ni MWIKO kwetu...

Karibu Al Kasus hapa "Mandi" Lumumba [emoji120]
Sasa niambie terms of the conditions ya ule mkataba kifungu kwa kifungu, na je wote wanaopinga hawajui hicho unachokijibu?
 
Back
Top Bottom