Kumbe inawezekana eeh?!
Kumbe Wananchi wakijitambua inawezekana! Haya yote yanafanyika ili kujikosha baada ya kuona hali ya upepo wa Kisiasa si nzuri kwa Magamba. Eti wanawasimamisha Wakurugenzi wao walioshindwa kuwaibia kura ama kutangaza wagombea wao walioshindwa etc. Kama kweli CCM inania wawatimue MAFISADI wote hata wasipowashitaki mahakamani, masikio na macho yao yafunguke wasikilize na watekeleze kile wanachoambiwa au kuona kutoka kwa wananchi! Wananchi wamelalamika kuhusu Katiba mbovu iliyopo na hiyo pendekezwa, rushwa na ufisadi, double standard katika sheria, ukubwa wa serikali na matumizi makubwa yanayo aksi wizi wa mali ya umma etc.
Wananchi wasibweteke na hatua hizi mchwara za kujaribu kurudisha imani, wakiendelea kukaza kamba mpaka uchaguzi Mkuu ujao mbona kitaeleweka tu.