R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Zanzibar imesema juhudi za Chama cha Wananchi (CUF), kupinga Muungano uliopo na kutaka mkataba au serikali tatu ni azima yao ya kukamilisha mpango wa kuyapoteza na kuyafuta Mapinduzi Zanzibar.
Dai hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, wakati alipozungumza na wanachama wa jumuiya hiyo katika Ofisi za CCM Tawi la Mbweni mjini Unguja leo.
Shaka alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umefikia miaka 49, kwa muda mrefu umekuwa kikwazo kwa maadui wa nje na ndani katika kufikia malengo ya kuyafuta Mapinduzi hayo.
"Nje ya Muungano kuna ajenda tete ikipigiwa debe na CUF, tokea mwaka 1964 Muungano uliwakera watawala waliopinduliwa kurejea vyama vingi mwaka 1992 kumeifufua Hizbu nyuma ya CUF kukamilisha mpango huo," alidai Shaka.
Alisema pamoja na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayovishirikisha vyama vya CCM na CUF, bado CUF wanajionesha ni wapinzani hatari wa Mungano na Mapinduzi ya Zanzibar.
Alieleza kuwa jambo hilo halihitaji mwanga wa tochi kuona bali vitendo vya CUF, viongozi wake na matamshi yao ni ushahidi usiotia shaka. Aidha, aliwataka vijana katika kizazi cha sasa kusimama imara na kuyatetea mapinduzi hayo kwa nguvu, akili na maarifa yao kabla ya urithi huo haujaporwa na maadui.
"Walioteseka na kupoteza maisha ni bibi na babu zetu wa Kiafrika, urithi huu ni haki na halali yetu, tukikubali kuupoteza tutakwisha kwani maadui wanakesha usiku na mchana kutaka kutunyang'anya, alisema Shaka.
Akizungumzia kuhusu changamoto za ajira kwa vijana, Shaka alisema jumuiya yake imejipanga kuhakikisha inatoa mikopo ya ujasiriamali na uwezeshaji kiuchumi kupitia makundi ya vijana.
Kuhusu mjadala wa marekebisho ya Katiba, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM alisema msimamo wa chama chake ni kubaki na muundo wa serikali mbili kwani kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuhatarisha amani na usalama uliopo.
Source: Tanzania Daima