Uvccm arusha wamuomba mlezi wao stephen wassira aokoe jahazi linalozama.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Baada ya mjumbe mmoja wa UVCCM-Arusha kutoa taarifa kuwa vijana waliomsindikiza mbunge wa viti maalum Catherine Magige kutoa msaada wa baiskeli kwa walemavu huko Arusha wamegomea posho ya 5,000 aliyogawa huyo mbunge,hali ya hewa imeanza kuchafuka.Mwanachama huyo Philimini Amo alitoa kauli hiyo wiki moja aliyopita kuwa wanachama hao wa umoja wa vijana wamechoka kudhalilishwa na wanasiasa wakongwe wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi na kuwaacha hoi bini taabani.

....Wakiongea leo vijana wa umoja huo wanadai hawamtambui ndugu
Philimini Amo,na wanashangaa amepata wapi mamlaka ya kuisemea UVCCM-Arusha,wakaendelea kusema kuwa mambo haya yalikemewa na mlezi wao Mzee Wassira sasa yameanza kujirudia tena wakati huu wa kuelekea kwenye mapambano huko Arumeru-Mashariki.Wakasema huyu mwanachama anatumiwa na kundi fulani la watu kuiangusha UVCCM kwa maslahi yake binafsi bila kutaja jina la huyo mwanachama wala cheo chake.Kutokana na hali wamemuomba Stephen Wassira aingilie kati maana umoja wao umeanza kuvurugwa wakati wanaelekea kwenye uchaguzi wa ARUMERU-Mashariki.

Source : TBC1 Dira ya mchana.

 
Hao TBC usiwategemee sana, ni mafundi wa kukarabati habari mpaka mwisho wa siku inatoka ndivyo sivyo! Kwa maneno mengine TBC sio reference nzuri kitaaluma.
 
Back
Top Bottom