barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,825
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Arusha,umepokea kwa furaha kuondolewa kwa Mkuu wa Mkoa Ndugu Ntibenda na kuteuliwa kwa Mkuu wa Mkoa mpya Mh.Mrisho Gambo.Furaha hiyo imetokana na UVCCM Arusha kutoa tamko ambapo haujapita hata mwezi na Rais kaweza kuwasikia na kutekeleza ombi la kuondolewa kwa mkuu wa Mkoa.
Mwenyekiti wa UVCCM Arusha,Lengai Ole Sabaya anasema kuondolewa kwa Mkuu huyo wa Mkoa ni furaha kwa jumuiya yao,kwani Rac huyo alikuwa ni mtu asiyetoa ushirikiano kwenye jumuiya hiyo kiasi cha wao kutuma maombi kwa Rais na kutaka amuondoe ndugu Ntibenda na kuweka mtu mwingine ambaye ataendana na kasi ya Mkoa huyo,ambapo Rais ametekeleza kwa kumteuwa Mh.Gambo ambaye vijana wa Arusha wanaamini watafanya nae kazi na atataendana na kasi ya siasa za mkoa wa Arusha.
Itakumbukwa hivi karibuni UVCCM Mkoa wa Arusha,wakishirikiana na DC wa wakati huo Mrisho Gambo na kwa msaada wa mfanyabiashara maarufu na kada wa CCM waliungana katika kumuomba Rais kuivunja halmashauri ya Jiji la Arusha inayoongozwa na CHADEMA kutokana na kile walichosema ni kushindwa kwa uongozi huo wa upinzani kuongoza Jiji hilo.
Ole Sabaya anasema kuondoka kwa Mh.Ntibenda kutaihuisha Jumuiya hiyo ktk jiji la Arusha ambayo kwa uongozi wa Ntibenda ilianza kuzorota kwa RC huyo kujiweka kando nao.Lakini kwa uteuzi wa kijana Gambo sasa Jumuiya inaenda kuwa imara na thabiti,pia wamemtuhumu Ntibenda kuzembea ktk swala la ulinzi na Usalama kiasi kwamba ndani ya muda mfupi,shule kadhaa katika mkoa wa Arusha zilichomwa moto.