nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 805
- 2,843
MWENYEKITI UVCCM TARIME APEWA MILIONI 30 KUFANYA ZIARA KUMBEBA MWITA WAITARA NA GERALD MARTIN KUELEKEA KURA ZA MAONI TARIME MJINI NA VIJIJINI
Uongozi wa UVCCM Tarime umeamua kuchukua mkondo wa kuegemea kwa watia nia, na tayari wameunda timu yao wanayoiita chaguo la vijana kuelekea mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika majimbo ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini.
Ili kufanikisha nia yao wameanza ziara ya kuzunguka na kukagua uhai wa jumuia ya vijana, kuwa ni kuwaandaa kuelekea kura za maoni ndani ya chama. Ziara hiyo imezua sintofahamu kwa jinsi inavofanyika kwani haijalenga kukutana na wanachama wote wa UVCCM bali imelenga kukutana na wajumbe wanaoingia mkutano mkuu katika kura za maoni za kuchagua wagombea.
Vijana wengi wameshitukia tabia za Mwenyekiti UVCCM Tarime, Ndugu Godfrey Francis kuwatumia vijana hao au umoja huo ili kujipatia kipato, na fahamu ya kuwa Mwenyekiti huyo hana kazi ya kujiingizia kipato na amegeuka dalali wa watia nia ili walau apate kipato cha kuendesha familia yake, na hata gari anayoendesha kanunuliwa na watia nia, maana hana hata genge la kuchoma mahindi yeye, wala mke wake, kiufupi anategemea siasa ili kuendesha maisha yake.
Vijana wa UVCCM Tarime wameshitukia michezo ya huyo Mwenyekiti maana ni muda mrefu amekuwa akiitisha makongamano na kuomba pesa ili kuwawezesha vijana na zinaishia mfukoni mwake yeye, katibu wake, Katibu Hamasa, ambaye naye hana kazi ya kufanya naye anategemea siasa ili mkono uende kinywani.
Katika kundi kundi la UVCCM Tarime, mwanachama mwenye namba 0622348451 (Daniel Mkiriti) amehoji, namnukuu “Viongozi wa wilaya jumuiya ya vijana tunaomba mtuwekee ratiba ya ziara yenu ili kila kata ijiandae mbona mnaificha?, kushitukiza watu sio vizuri na sisi tuandae walengwa manake hamuwezi kuja kukaa na viongozi tu” mwisho wa kunukuu.
Katika ziara hiyo kuna mtu wa Mwita Waitara na wa Gerald Martin, ambao viongozi wa UVCCM Tarime wakishazungumza na hao wajumbe basi watu hao huwaita pembeni na kuwapa viongozi hao pesa kama kishawishi cha kumpigia kura Mwita Waitara na Gerald Martin.
Milioni 30 alizopewa Godfrey, ni kwa ajili ya kusaidia ziara hiyo katika kata zote za Wilaya ya Tarime, pia kwa ajili ya posho yake, Katibu wake Newton Mwongi na Katibu Hamasa, Pascal Mkapa. Na kila wakifika katika kata wawakilishi wa watia nia hao, huwapa posho za 30,000 kwa kila kiongozi ambaye anaingia mkutano wa wilaya/jimbo.
Hata hivyo, ziara hiyo imewagawa wanachama wa UVCCM kwanza kwa viongozi wao kuamua kubagua wagombea wengine na kuamua kuwa madalali, pili kwa viongozi hao kuitumia jumuiya hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe. Na wengi wamedhamiria kutowaunga mkono wagombea hao ambao viongozi wao wamewabatiza kuwa ndio viongozi wa vijana.
Na nakishauri Chama kiangalie mienendo ya hawa viongozi wa UVCCM Tarime kwani wanatumika kukigawa chama kwa maslahi yao binafsi.
Ni mimi,
Venance Marwa
Mwanachama – UVCCM Tarime.