Uvamizi wa Ndege wenye kinyesi cha ajabu Kagera

Uvamizi wa Ndege wenye kinyesi cha ajabu Kagera

HarakatiNews

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
218
Reaction score
187
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imetuma wataalum wake katika kisiwa cha msira mkoani Kagera kuchunguza ndege wa ajabu wanaokunya kinyesi cha ajabu kinachosababisha kutu kwenye mabati na kusababisha yatoboke kwa muda mfupi na kusababisha kuku na mbuzi kufa.

Hao ndege kama wanavyoonekana katika picha hadi sasa wamesababisha jumla ya kuku 516 na mbuzi 12 kufa.

NDEGE+2.jpg
NDEGE+5.jpg

Afisa Tarafa Rwamishenyi Abdon Kahwa na mtaalamu kutoka wizara ya afya mwenye nguo ya blue Dk Munda Elias , akiwaeleza wananchi hatua zinazochukuliwa na serikali.

Chanzo hapa:HARAKATINEWS Blog

===========

Ndege wa ajabu wavamia makazi Kagera

Bukoba. Ndege wa ajabu wanaosadikiwa kutoa kinyesi chenye sumu kali, wamevamia Kisiwa cha Musira kilichopo Manispaa ya Bukoba na kusababisha vifo vya mifugo na ndege wafugwao, huku ukali wa sumu hiyo ukisababisha kutoboka mabati ya nyumba zilizopo kisiwani humo.

Ndege hao wanaoaminika kuvamia kisiwa hicho mwezi mmoja uliopita tayari wameshasababisha vifo vya kuku 516 na mbuzi 12 wanaodaiwa kugusa au kula kinyesi chao. Hata hivyo, bado haijafahamika ndege hao wanatokea nchi gani.


Akithibitisha habari hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Massawe alisema Serikali ilipata taarifa hizo kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na baadaye kuundwa timu ya kutafuta taarifa za awali za tatizo hilo.

Massawe alisema ndege hao, pamoja na kusababisha vifo vya mifugo na ndege wafugwao pia baadhi ya miti katika kisiwa hicho imekauka na mabati kutoboka inapotokea kinyesi chao kitaangukia kwenye paa za nyumba zao.

Pia Massawe alisema kuwa, taarifa ya kuwapo kwa ndege hao katika Kisiwa cha Musira, ilifikishwa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kebwe Stephene Kebwe aliyekuwa mkoani humo wiki iliyopita na kuwa suala la kuwapo kwa ndege hao siyo la ghafla kwa kuwa walikuwapo hapo awali.

Dk. Kebwe alisema wizara imetuma wataalamu kuchunguza tatizo hilo na kuwa wizara hiyo itaangalia ukubwa wa tatizo hilo linavyoweza kuwaathiri wananchi.

Hata hivyo, alisema suala hilo pia linahitaji ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Dk. Munda Elias alikwishawasili kwa ajili ya uchunguzi na kuthibitisha kuwa tayari kinyesi cha ndege hao kimepelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi na Mkoa unasubiri matokeo ya utafiti huo.

Naye Ofisa Tarafa wa Rwamishenye, Abdon Kahwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Ziporah Pangani alisema tayari Serikali imechukua hatua za kupiga marufuku kupeleka au kusafirisha mifugo kutoka kisiwani humo kwenda maeneo mengine kwa hofu ya kusambaa kwa sumu hiyo.

Pia alisema ndege hao wameleta hofu kwa wakazi wa kisiwa hicho, kwani kinyesi chao kinapodondoka kwenye bati hupata kutu na kutoboka, huku kukiwa na hofu nyingine kwamba huenda mifugo nayo imeathiriwa.

Source: Mwananchi


My take:
Nimejaribu kuangalia hapa jamvini kama hii habari ilishaletwa lakini sikuiona, mods kama ilikuwepo basi iunganishe.

Cha kusikitisha ni kuwa ndege wa hatari wanatokea tena katika hili eneo ambalo tayari limeanza kuwavutia watu wengi duniani kwa uzuri wake!
 
kutoka na hali hiyo Wananchi wa Kisiwa cha Msira, manispaa ya Bukoba wametahadharishwa kutosafirisha mbuzi na kuku kutoka na kuingia kisiwani humo kwa muda ili kupisha uchunguzi wa kitaalamu.

Mtaalam wa Utafiti wa Wanyama na Ndege kutoka Wizara ya Afya Dtk. Munda Elias amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kipindi ambacho wataalam hao watakuwa wanafanya uchunguzi.

Amesema kuwa utafiti huo utachukua muda wa siku tatu, ambapo watachunguza aina ya ndege hao na kinyesi chao.
 
Majanga hayo.
Kuku na mbuzi wakuwaje na mgusano na hao ndege ?
Na kama ni kinyesi kuwadondoke je hakuna mtu aliyewahi kudondokewa na kenyesi cha hao ndege?
Kama alikuwepo yeye alijisikiaje?
Hao ndege na kuku wanaonekanaje kabla ya kufa?
 
Daah, yaan ni majanga baada ya majanga. Sijui hii ishu ishawahi kutokea sehemu yoyote duniani ili tuweze kupata reference? Pia tuweze kukopi na kupaste solution
 
Haw jamaa mbn kila janga linaazia kwao. Juliana, ebola, 7 day nk. Hao ndege yaelekea hicho kinyesi kinamchanganyiko wa acd ya majimaji ya katerero
 
Ndege wanaoonekana kwenye picha wanaitwa 'white herons' kwa kiingereza. Kuhusu kinyesi chao kuwa hatari kwa baadhi ya wanyama, madaktari wa wanyama na ndege (veterinarians) wachunguze ile sehemu ya 'mkojo' kwenye kinyesi. Inajulikana kwamba ndege hawakojoi kama wanyama wengine, ila uchafu majimaji huchanganywa na uchafu mzito na kutoka wote kama kinyesi kizito. Uchafu majimaji huu waweza kuwa na uric acid nyingi kiasi cha kuwa sumu. Hili lichunguzwe. Ni kweli kinyesi hiki chenye uric acid nyingi kikidondokea kwenye bati acid hiyo hutoboa bati. Hakuna la ajabu hapa, ni chemistry ya mazingira.
 
hii ni hatari! watalaam wanastahili pongezi kwa kuitikia kwa wakati, tunawaomba mkamilishe hili kwa wakati, ila nawashauri kuwashirikisha watu wa mifugo badala ya kukaa nalo kwenye wizara ya afya tu kwani laweza kuwa suala la afya mtambuka! (laweza kudhuru wanyama na binadamu).
 
Nauuliza ..kuwa kuna aina mbili za ndege moja weupe na pili weusi sasa wepi wenye madhara hayo?
lakini ipo faida na hasara... Utafiti maalumu wahitajika, kabla ya uuamuzi kuchukuliwa..
 
Vita vya Uganda na Tanzania .......

Haw jamaa mbn kila janga linaazia kwao. Juliana, ebola, 7 day nk. Hao ndege yaelekea hicho kinyesi kinamchanganyiko wa acd ya majimaji ya katerero
 
Haw jamaa mbn kila janga linaazia kwao. Juliana, ebola, 7 day nk. Hao ndege yaelekea hicho kinyesi kinamchanganyiko wa acd ya majimaji ya katerero
Akili inapofanya kazi kwa mtindo wa kufuli (ili ifanye kazi mpk ifunguliwe makalioni) matokeo yake ndo kuja na coment za majitaka kama hizi mb**a wewe
 
Mbona kama huyo oficer mwenye koti la blue kama kalala hivi kweli kuna masikilizano hapo?
 
WIZARA ya afya na ustawi wa jamii imetuma wataalam katika kisiwa cha Musira kilichoko katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ndege wa ajabu ambao kuku au mbuzi wakila kinyesi chao wanakufa.


Kutumwa kwa wataalam hao kumetokana na taarifa ya mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe kuhusu ndege hao kwa naibu waziri wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dk. Steven Kabwe alipokuwa mkoani Kagera wiki iliyopita.


Mmoja wa wataalam hao kutoka katika wizara hiyo Dk. Munda Elias ambaye ni mtaalam wa utafiti wa wanyama na ndege, amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kipindi ambacho watakuwa wanaendelea na uchunguzi ili tatizo hilo liweze kupatiwa ufumbuzi.


Dk. Elias amesema kuwa utafiti huo ulioanza Machi 12 mwaka huu utadumu kwa muda wa siku tatu na kuwa watachunguza aina ya ndege hao na kinyesi chao.


Mbali na kinyesi cha ndege hao kusababisha vifo vya wanyama na ndege kama kuku, pia kinyesi chao kinapodondoka kwenye bati inadaiwa linapata kutu na kisha linatoboka.


Kutokana na tatizo hilo wananchi wa kisiwa cha Musira wamepigwa marufuku kusafirisha mbuzi na kuku kutoka au kuingia kisiwani humo, ili kupisha uchunguzi huo wa kitaalam.


Agizo hilo limetolewa na afisa tarafa wa tarafa Rwamishenye Abdon Kahwa wakati akizungumza na wananchi wa kisiwa hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba, Zipporah Pangani.


Kahwa amesema kuwa tangu ndege hao waripotiwe kuingia katika kisiwa hicho zaidi ya mwezi mmoja uliopita, kuku 516 na mbuzi 12 wameripotiwa kufa baada ya kula nyasi na chakula kilichochanganyikana na kinyesi cha ndege hao.

Chanzo: NEWS ALERT: KINYESI CHA NDEGE WA AJABU CHAUA MBUZI, KUKU MKOANI KAGERA - Tabianchi
 
Ndio maana nyumba zote Bukoba zimechakaaa. KUUUMBEEEH.nilifikiri ni maji ya katerero kumbe ni hawa ndege? wahaya mnakula nyama ya ndege au tulete wahehe wawasaidie ?
 
Back
Top Bottom