Lakini wananchi hao hao wanaendelea kupigia kura mafisadi. Tuna lalamika sana wakati njia pekee ni kuwaondoa kwa kutumia kura. hata kama wanaiba they can only steal up to a certain extent. Hauwezi kuendelea kulalamikia viongozi wakati wa uchaguzi ukifika una wapigia kura tena au hauendi kupiga kura ya kuwa pinga. Njia tunayo ambayo ni kura lakini hatuitumii tuna zidi kulalamika. Angalia chaguzi ndogo tu iliyo pita hapa juzi juzi, watu wameambiwa kuhusu ufisadi na madhambi yote ya uongozi lakini wame kichagua chama kile kile wanacho kilalamikia.
MwanaFalasafa,
Unazungumza kana kwamba wapigakura wameishabaini kuwa CCM imejaa wanachama mafisadi kwa hiyo hakuna mwana-CCM ambaye anastahili kupewa kura.
Sisi kijijini kwetu hakuna Chama kingine chochote wananchi wanachokijua zaidi ya CCM. Hata mtaani kwetu hapa jijini na mtaa wa pili na wa tatu tuna Wajumbe wa nyumba kumi wa CCM na wanatuhamasisha tukajiandikishe ama tuhakiki kadi zetu maana chaguzi zinakaribia. Huko kijijini, ukimuuliza mwanakijiji Mbowe ni nani hamjui, Slaa ni nani hajui, Zito ni nani hajui, Cheyo ni nani hajui, Lipumba ni nani hajui, Rostam ni nani hajui, Mengi ni nani hajui, Balali ni nani hajamsikia; Liyumba ni nani hajui, magorofa pacha ya BOT hajayasikia! Ukimuuliza Kikwete unamjua, atakwambia anamjua kuwa ndiye Rais wa Tanzania na ndiye alimpigia kura mwaka uleee wa neema ya kanga, tshirts, sukari etc CCM tulipofanya kampeni 'kabambe' hadi vijijini.
Viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani naomba mniwie radhi. Mnaudhi sana! Unapofika wakati wa uchaguzi ndio mnakurupuka kwenda kwenye majimbo kutaka mchaguliwe. Mkisimama kwenye majukwaa mnawatukana na kuwakejeli wananchi kwa kuwaambia ni wajinga kwa nini wanakipigia kura Chama cha Mapinduzi kilichojaa mafisadi! Mnaenda Mwembe Yanga mmetaja mafisadi 10 tu!
Chama cha Mapinduzi nasi tukienda kwa wananchi tunatoa uongo mwingi ili mradi tu tuchaguliwe na kuwafanya wananchi na wana-CCM wenzetu wa ngazi za chini wapumbavu fulani.
MwanaFalasafa, Elimu ya Uraia ni jambo muhimu sana iwapo kweli tuna nia ya kuleta mabadiliko ya kweli na yenye manufaa nchini mwetu. Vinginevyo tutaendelea na nyimbo zetu za kuwahamasisha wananchi tuchukiane wenyewe kwa wenyewe ama tuvichukie vyama ambavyo vina wanachama wengi safi ukilinganisha na waovu wachache.
Wapinzani wa CCM, hakitaeleweka chochote kwenye sanduku la kura mpaka mjipange vizuri, muwe na malengo ya pamoja yanayoeleweka na si kila mtu na agenda yake, mjitoe muhanga, mshirikiane, msibaguane, la sivyo Chama cha Mapinduzi kitaendelea Kudumu! Jifunzeni kutoka kwa Waasisi wa chama cha TANU, hawakuwa na elimu wala uwezo kifedha lakini kwa moyo wa kizalendo, walijituma na kujitoa muhanga wakaweza kuwafikia wananchi vijijini, na lengo lao lilikuwa linaeleweka. Sisi wazee tusio na meno hivi sasa, tunakumbuka kwamba tuliijua TANU tukiwa vijijini hata kabla nchi haijapata Uhuru na kwamba chama hicho kilikuwa ni chama cha kupigania Uhuru, sera kuu ilikuwa kuwaunganisha wananchi wote kuwa kitu kimoja ili mafanikio yaweze kupatikana.