Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 8, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Shamba la Mbunge Kimaro lazua balaa

  Charles Ole Ngereza

  Zaidi ya wakazi 3,000 wa Kijiji cha Singisi, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamevamia shamba linalodaiwa kumilikiwa na Mbunge wa Vunjo Aloyce Kimaro (CCM) na kuchoma moto nyumba 19, matrekta matatu, kufyeka ekari zaidi ya 100 za shamba la migomba na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

  Wanakijiji hao wakiwa na silaha mbalimbali, yakiwemo mapanga, sime, mikuki na silaha za jadi, walilivamia shamba hilo linalodaiwa kuwa na ukubwa ekari zaidi ya 500 kwa madai kuwa Mbunge huyo alimilikishwa kisheria lakini katika mazingira ya kutatanisha.

  Tukio hilo lilisababisha mapambano kati ya polisi na wanakijiji hao lakini polisi walizidiwa nguvu na kulazimika kukimbia eneo hilo.

  Waandishi wa habari walishuhudia polisi hao wakifyatua mabomu ya kutoa machozi na wanakijiji hao wakiwa na chupa za maji ambayo walitumia kunawa uso na kuwakabili askari kwa mawe.

  Katika mapambano hayo yaliyodumu kwa takriban saa sita, wanakijiji hao walifunga barabara zinazoingia katika shamba hilo kwa mawe na magogo na kuendelea na uharibifu wa mali.

  Waandishi wa habari pia walishuhudia watoto kadhaa wa kijiji hicho waliodhurika na mabomu na kukimbizwa katika zahanati iliyo karibu kwa matibabu.

  Wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao walidai kuwa wameamua kuchukua sheria mikononi baada ya jitihada zao za kutafuta haki kugonga mwamba katika vyombo vya serikali mkoani Arusha.

  Kisale Simba, alisema walilifikisha suala hilo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkoa wa Arusha, lakini hakuna kiongozi aliyeweza kulishughulikia.

  Alisema wanakijiji wanakabiliwa na uhaba wa ardhi na kushindwa kuweka miundo mbinu ya huduma za jamii, zikiwamo zahanati na shule.

  “Hatuna hata eneo la kujenga shule ya sekondari, yeye anamiliki ardhi kubwa na ni ya mababu zetu, tumehangaika kila mahali tumepuuzwa acha tufe leo,” alisema huku akishangiliwa na wenzake.

  Mwananchi mwingine, Juma Ndewario, alisema kwa sasa hawana hata maeneo ya kuweka makabauri kutokana na uhaba wa ardhi katika kijiji chao na kwamba walitarajia kuwa walau wale wasio na ardhi wangepewa eneo dogo.

  Ndewario alidai kuwa eneo lingine la shamba hilo wameuziwa mafisadi ambao hata hivyo, hakuwataja akidai kuwa serikali inawafahamu. Aliongeza kwamba, wanatakiwa kuhamia Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kupata maeneo mengine, lakini wamekataa kuondoka kutokana na mgogoro huo.

  “Wanatuambia eti twende huko tukafe na malaria. Hatuondoki ni lazima tufie hapa kwetu,” alisisitiza.

  Akizungumzia kuhusu vurugu hizo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mecy Silla, alisema wanawatafuta viongozi wa jamii hiyo ili wawaamuru wanakijiji hao wasitishe uharibifu wa mali na kutafuta muafaka.

  Hadi kufikia jana, zaidi ya magari saba ya polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), yalikuwa yakizunguka eneo hilo huku wanakijiji hao wakiwa juu ya vilima vinavyopakana na Mlima Meru uliopo karibu na kijiji hicho.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, pamoja na kukiri kuwepo kwa tukio hilo, pia alisema hali ya usalama imeimarishwa.

  "Tutawapa taarifa baadaye kwa sasa tuna ugeni wa Waziri Mkuu lakini hali ya amani itarejeshwa kwa vyovyote vile, “ alisisitiza Kamanda Matei alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu.

  Kwa upande wake, Mbunge Kimaro alithibitisha kupata taarifa za kuvamiwa shamba hilo juzi usiku na kusisitiza kuwa suala hilo anaviachia vyombo vya usalama na serikali kuchukua hatua.

  "Sielewi nia ya hao watu...sijui nini kinachotokea), sina uhakika nipo Dar es Salaam, taarifa nami nimepata kama ulivyopata wewe," alisema Kimaro.

  Alisema shamba hilo liko katika eneo ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya uwekezaji na kwamba linamilikiwa na kampuni ya Nakara ambayo na yeye ni mmoja wa wawekezaji.

  Kimaro alisema kampuni hiyo ilipanga kujenga hoteli ya kitalii katika shamba hilo na kwamba madai ya wanakijiji hao kwamba wao wamegawiwa katika mazingira ya kutatanisha, si ya kweli.

  Alisema hadi sasa hajajua hasara waliyopata kutokana na magari na nyumba hizo kuchomwa moto.


  NIPASHE
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Matatizo ya kuishi nyumba ya vioo then unakua bingwa wa kurusha mawe, kawapiga makombora wenziwe sasa yamebackfire. Pole Mzee Kimaro.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Matatizo ya kuishi nyumba ya vioo then unakua bingwa wa kurusha mawe, kawapiga makombora wenziwe sasa yamebackfire. Pole Mzee Kimaro. Nguvu ya umma au fitina ya umma
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kimaro awagawie tu hapo ardhi hawa wananchi..kama ana heka 500 awpe hapo 300 yeye abaki na 200!
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Henheee,heee! Mkuu umeona watu kule kwenye thread ya utabiri wa mwalimu watu wanavyopotea badala ya kujadili utabiri wenyewe!
  Ndiyo haya sasa, kwa sababu dola imeshindwa kusimamia haki hata watu
  hovyo kama Kimaro wanajifanya wapinga maovu!! Heka miatano...TEREKITA tatu! nyumba ngapi.... duh!
  Alikopa wapi, kwa taratibu gani? hapo kaishia kuwa mbunge tu.... angekuwa waziri au President angekuwaje??....
  Alafu eti anamlipua Mkapa bungeni Kiwira!!, hana lolote anaona wivu tena yeye ndio Bepari mbaya zaidi!
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Alighani MRISHO MPOTO... Migodi sita yooote ya kwangu... Ekari 100 Najiandaa kustaafu nipate mahali pa kupumzika...
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kimaro ni tajiri wa kutupwa ana mahoteli ya nguvu ya Kitalii mlima Kilimnanjaro (KINAPA)..n.k. Swahiba wake Sumaye ndo alimpiga tafu!
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watu wa aina ya kina Kimaro, Mengi, Mwakyembe,....wachohubiri ni kwamba kama ni kuiba, kufisadi,kutajirika,... awe ngozi nyeusi( mzawa?). Akiiba RA, Subash, Manji huyo ni fisadi papa!
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Mzee hapo umeshindwa kutofautisha kati ya "kuharisha na kutapika!"
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu ulisomea chuo gani cha kujua kutoa majibu namna hii? umenikuna!
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Yanafanana. Tofauti ni njia yanakopita.
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Usipindishe mada,hoa ni Wameru,Kimaro haelewani na Mmeru mwenzao(EL) Fisadi sasa ngoja na wao watimuliwe kokote walipo waone raha yake.Huu uchochezi wa mafisadi mara ufamizi,mara ajali za kutatanisha,mara miswada ya ajabu ya sekta ya habari yatajaigharimu TZ Serikali isipochukua hatua.Kimaro hakuiba fedha za kupata shamba hilo kama mafisadi walivyofanya,walikuwa wapi tangu hapo hadi vita ya ufisadi ianze,Mmeru fisadi mkuu aache uchochezi,akiendelea tutang'oa kila kilicho chake hata kama ameandika majina bandia.
   
 13. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kuna tetesi kuwa kumetokea vita hapo nyumbani. Kwa waliopo hapo tafadhali tujulisheni.


  MAHOJIANO YA MWANAKIJIJI NA MHE. ALOYCE KIMARO

  Bonyeza Hapa Kusikiliza
   
  Last edited by a moderator: Jun 9, 2009
 14. I

  Idda Member

  #14
  Jun 8, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyumbani wapi?
  Toa hints ndugu,.
   
 15. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Maeneo ya Meru - njia ya kwenda Moshi ukitokea Arusha mjini. Naambiwa kama kilometa 8 kutoka Arusha mjini na watu zaidi ya watatu wameshapoteza maisha. Ni vita kati ya kabila la wameru, wenyewe kwa wenyewe. Any update so far.
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Wananchi hawa wameonyesha mfano, mafisadi kaeni tayari subira ya wenye nchi inaelekea kikomo.
   
 17. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tupeni data au ni ile ya uvamizi wa Shamba la Kimaro?
   
 18. g

  grandpa Senior Member

  #18
  Jun 8, 2009
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna civil war. Ni wananchi wameshambulia mashamba. Na shamba mojawapo ni la Mbunge Kimaro
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ndio hizo hebu kwanza niulize
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  waswahili kwa tetesi hamjambo
   
Loading...