JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,966
Pamoja na kuwa na nguo nzuri, kuwa na mwili mzuri wa kukaa nguo (kuna watu hata umvalishe nguo nzuri namna gani bado hatopendeza), nimekuwa nikiboronga katika uvaaji, jinsi ya kujua nguo gani iendane na ipi, mara chache sana ninapatia na nikipatia basi nakuwa nasifiwa sana, oh! leo umependeza sana, hasa wanawake wananimwagia sifa sana, ni katika muktadha huu nimegundua nikijua kuvaa vizuri basi itakuwa siraha ya maangamizi kwa wanawake. Kwa kuwa mtandao huu una kila aina ya wataalamu, hebu nipeni elimu hii.