Misungwi Yetu
Senior Member
- Oct 7, 2017
- 103
- 39
NBS walitangaza nafasi za kazi kada ya Udadisi katika Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (Household Budget Survey - HBS), jumla ya nafasi 450 kwa nchi nzima.
Utaratibu kwa waombaji, pamoja na mambo mengine, sifa za msingi alipaswa kuwa na Elimu ya kuanzia kidato cha IV na pia awe mkazi kutoka katika eneo husika (mkazi ama mzaliwa wa kijiji au mtaa husika).
Kwa uthibitisho wa barua ya mtendaji wa kijiji au mtaa ambapo utafiti utafanyika.
Sisi katika kijiji chetu hapa Misungwi, waombaji tulikuwa NANE (8) TU, hadi siku ya mwisho kutuma maombi (12/ 08/2017). Nakala za Barua zetu hadi leo Mtendaji wetu wa Kijiji anazo.
Cha ajabu kati yetu hao waombaji nane, HAKUNA HATA MMOJA ambaye amewahi kutumiwa MESEJI wala KUPIGIWA SIMU kuitwa kwenye usaili unaosemekana kuwa ULIKWISHAFANYIKA.
Tumejaribu kufuatilia kwa Mtendaji wa Kijiji HAKUNA TAARIFA YEYOTE, hata yeye anashangaa tu. Tumeenda kuuliza kwenye Ofisi za TAKWIMU Mwanza, wanasema TUSUBIRI MATANGAZO YATATOKA TU, simu wakipigiwa HAWAPOKEI (0282502500).
Tetetsi mitaani inasemekana Watu walishapigiwa simu siku nyingi, inamaana Kijiji chetu WAMEKIRUKA? Au kuna WATU WATAPELEKWA TU?
Baba yetu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, tunakuomba ufuatilie hili jambo ili mchakato wake uwe kama wa Dar es salaam. Majina ya waombaji wote waliofaulu usaili yabandikwe, katika Mkoa wa Mwanza tumeomba wengi sana, ni kama Dsm tu.
Tunaomba mchakato uwe wa wazi ili turidhike na matokeo. Haya mambo ya kufanyia gizani yataleta malalamiko mengi na pia kuna harufu ya RUSHWA NA KUJUANA.
Karibuni Misungwi.