Uturuki yafanya kweli kuelekea European Union

Bongolander kama una siasa za ki SISIEM bongo,huwezi kuelewa jambo hili bila ya kutembea na kusoma mada mbalimbali.True,Ulaya hawasali sasa ,lakini huwezi kukataa imejengwa katika
Christian principles.
Utasema udini,lakini ni facts!

Ukoloni ulitupumbaza sana sie Waafrika! Hizi dini zilizoletwa kwetu zimetufanya vipofu na kudumaza uwezo wetu wa kufikiri. Sikatai watu kuwa na imani za kidini lakini huu upuuzi wa kuiona 'dini yangu ni bora kuliko dini yako' huwa unanikera sana! Magaidi wanatumia dini kufikia malengo yao; kwa mfano magaidi hupatikana karibia kila dini. Kuna magaidi wa kiislamu kama vile akina Osama na wafuasi wake na kulikuwa na magaidi wa kikiristo kama kule Northern Ireland. Adolf Hitler alitumia ukiristo kama kisingizio cha kuwaua watu wa mataifa mbalimbali na hasa hasa 'Jews'! Ukitaka kujua mojawapo ya sababu za watu kutokwenda kanisani ulaya, pitia historia ya vita kuu ya pili ya dunia. Kwa upande wa Afrika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda yalihusisha watu kulaghaiwa kwenda makanisani na wakauawa huko. Lakini hiyo haimaanishi kuwa ukiristo unahimiza ugaidi wa namna hiyo! Tuache ushabiki wa kidini usioleta tija!
 
Back
Top Bottom