UTURUKI: Serikali yatangaza kuiondoa hali ya hatari iliyowekwa baada ya jaribio la mapinduzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita.

Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni miongoni mwa waliokamatwa.

Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao.

Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari pekee hakuwezi kbadili hatua kazli za kisiasa zilizochukuliwa ambazo ziliibadili nchi hiyo na kuifanya inayokandamiza haki za binadamu.

Mapema mwezi huu Rais Erdogan aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, wagombea wa upinzani walisema kuwa kitu cha kwanza watakachokifanya iwapo watashinda uchaguzi ni kumaliza amri hiyo ya hali ya hatari iliyowekwa.

Wengi ya waliokamatwa kipindi hicho ni wale waliokuwa wakidaiwa kuwa wafuasi wa mpinzani wa Rais Erdogan anayeishi uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen, ambaye awali alikuwa mshirika wa Rais wa nchi hiyo.

Uturuki ilimlaumu yeye na wafuasi wake kuwa ndio waliopanga mapinduzi ya kutaka kuiangusha serikali ya nchi hiyo. Lakini hata hivyo mwenyewe alikana taarifa hizo.
 
Back
Top Bottom