Utumishi, Usahili wenu kufanyikia Dodoma, ni mzigo kwa waomba ajira. Wanatakiwa wawe na pesa ndefu ya kujikimu karibu laki tatu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Sijui waziri husika hajaliona hilo au vipi.

Vijana wetu wanaoomba ajira ni dhahili serikali haina huruma nao kabisa.

Sera za ajira siyo rafiki kwa wasaka ajira.

Leo hii unamuita kijana kwenye interview Dodoma, nafasi moja (one post) unaita watu 200 wakagombanie nafas moja kutoka mikoa ya mbali!

Gharama za nauli ni kubwa, mfano tuchukulie mtu anaetoka Dar to Dom au Kigoma/Mwanza to Dom kuja kufanya usahili!
  • Nauli peke yake anatakiwa awe na 30000/= na Chakula 10,000/=
  • Kulala guest 25000/= tangu siku ya kwanza hadi siku ya usahili wa mchujo,kusubili majibu ya mchujo siku 4-5, jumla 125000/= guest
  • Kula na nauli kwa siku tano elfu 10000 kwa siku hivyo ni 50000/=
  • Matokeo ya mchujo yanapotoka hayumo au yumo hupangiwa tarehe nyingine ya usahili wa mahojiano! Siku 10 au 14 mbele!
  • Hivyo atatakiwa kurudi kwao Dar/Kigoma au mwanza nauli 30000 na kula 10000 jumla 40,000/=
  • Halafu siku usahili wa mahojiano kuja tena 40000/= nyingine na kulala siku mbili jumla 50000 na kula 20000
  • Na kurudi kwao mkoa 40000 nyingine kusubiri kama atapangiwa kituo cha kazi au Kukosa kazi!
JUMLA KUU ni kama 405000/= atakayoitumia kuhudhulia huo usahili

Waliopitisha utaratibu huu huenda walifanya vikao na kujilipa posho per DM ya laki tano hadi million kupitisha utaratibu huo!

Hawakufikilia kabisa anaeomba hiyo ajira atalala wapi, siyo wote wana ndugu Dom.

Kibaya zaidi hata vijana wetu wapo hatarini kuwekwa unyumba kwa siku hizo ili kujikimu.

Serikali ilikuwa na uwezo wa kufanya Usahili kwa kanda ili kuepusha usumbufu kwa vijana.

Utumishi ilitakiwa wawe na mfumo wa kikanda ili wa kusini wafanyiwe usahili wkusini hukohuko na wa kaskazini wafanyiwe usahili huko huko halafu katika majumuisho ya maksi wachukue mshindi apewe kazi.

Au kama hilo ni gumu! Warudishe kazi ya kuajili kwa wakurugenzi wa wilaya! Ili watu waombe kwenye halimashauli kuondoa usumbufu!

Lakini utaratibu wa sasa ni wa hovyo sana labda kama wanafaidika wao na Posho per DM! lakini vijana wetu ndiyo wanaoumizwa.

Yanafanyika hayo waziri yupo!

Yanafanyika hayo katibu wa wizara yupo!

Sijui Hawaoni au hawajui?

Wasahili wenye mishahara wanaitwa kwa kupewa posho, nauli na Malazi LAKINI Wasahiliwa wanakuja kwa kuuza chakula na michango ya ndugu ili wakafanyiwe usahili!

Si ajabu kijana aliyetokea Dar kwenda Dom akafanyiwa usahili na Msahili aliyepanda nae Bus kutoka Dar!

WATAWALA SIJUI HUWA MNAAMUA HAYO KWA MASLAHI GANI
Updates
Hatimaye kilio chetu wana jamii forum kimesikika! Tunashukuru
 
"Ni sawa na Tff wapange mechi ya timu za mtwara zikafanyikie kigoma!" Na mashabiki watoke nao mtwara kwenda Kigoma!
 
Kwani wapi ambako hatutumii hiyo laki 3? Utumishi wafanye usaili kwa kanda Ili kutupunguzia mzigo.
Yaan kijana kuliko kutumia pesa yote hiyo bora imsaidie kufungua genge ajiajiri! Kuliko kuliko kumiizwa na serikali kwa usumbufu usiyo na tija.
 
Kwani wapi ambako hatutumii hiyo laki 3? Utumishi wafanye usaili kwa kanda Ili kutupunguzia mzigo.
Mkuu, Mimi nafikiri kwanza watengeneze Mfumo wa mtandao kwa ajili ya kuwafanyia watu Aptitude test Mara Moja kwa Mwaka kwa kada mbalimbali za serikali kwa njia ya mtandao. Matokeo hayo yanatumika pamoja na mtihani wa mchujo ambao nao ufanyike kwa njia ya mtandao na kisha, Interview Mchujo wa kwanza unafanyika kwa njia ya simu.

Baada ya hapo wakishapata wale Best of the Best Ndo wanawaalika kwa ajili ya Final Interview kwa ajili ya Selection ambapo wanaweza kuwafanyia Review ya Aptitude test, Mtihani wa Mchujo, na maswali ya telephone interview ndani ya siku moja.Matokeo yao yanunganishwa na matokeo ya final interview na any other credentials. Maisha yanaendelea.

Kama kazi ni ya halmashauri hatua ya mwisho ifanyike katika halmashauri husika. Kama ni ya taasisi flani vivyo hivyo.Inawezekana na teknolojia zipo na watu wanao uwezo wa kufanya hivo ila kwa sababu ya kuendekeza wizi na upigaji hawatafanya hivo.
 
Wale wapuuzi wanakuaga wameshandaa mtu wao ile inakua ni angaisha bwege tu.

Nakumbuka mimi na rafiki yangu tulijisitiri hostel UDOM kwa dogo janja hadi usahili unamalizika mwisho wa siku hata kazi yenyewe hatuku bahatika kupata.
 
Wale wapuuzi wanakuaga wameshandaa mtu wao ile inakua ni angaisha bwege tu.
Nakumbuka mimi na rafiki yangu tulijisitiri hostel UDOM kwa dogo janja hadi usahili unamalizika mwisho wa siku hata kazi yenyewe hatuku bahatika kupata.
Duh
 
mleta mada umenimumbusha interview zangu kama 3 nilizofanyaga nje ya mkoa sikuambulia hata moja sema zote nilihakikisha nakula kimasihara.

Maana kama ukienda kwenye usahili wa style hyo ile sku moja kabla kama ukkwa mjanja kama utakutana na mwenzio ambae mnafanya nae usaili sku inayofata kumbeba ni very easy
 


Dodoma ipo katikati ya nchi kwa hio hii itasaidia sana, Hii ndio haki, Watu wa Dar wanahisi wameumizwa ila hili lilibidi lifanyike kwa manufaa ya watu wengi wanaoishi mbal sana na dar ili nao waweze kuondokana na kero za safari ndefu, kufika usiku sana, nauli ndefu, n.k

Kusubiri majibu ya mchujo !! hivi unazijua au ubazisikia interview za serikali?? majibu ya mchujo wa kwanza yanaweza kutoka hata baada ya wiki 2 au mwezi, Ukimaliza interview kesho yake unarudi kwenu mkuu, utayapata majibu huko huko kwenu, ubaki kusubiri majibu una babu yako kakuambia utakuwa shortlisted au 😂😂

hii iko poa
 
Mie kila nikienda usaili lazima niwagonge wasailiwa wenzangu. Semina yoyote lazima nusu ya hela nigongee.


Sitasahau nilipomgonga polisi mwaka jana kwenye kituo teule cha kuhifadhi "makaratasi'.


Hata hajajifuta akabeba gobore lake. Nilicheka sana
 
We jamaa siku zote huwa hutafakari! Unakimbia mvua unajitupa bwawani halafu unajisifu
 
Mbona mimi nilitoka mwanza kuja kufanya usaili dar. Tatizo mtoa mada unadhani kila mtu anandugu dar au anakaa dar. Bora hata saivi dodoma ni kati kati
 
Mbona mimi nilitoka mwanza kuja kufanya usaili dar. Tatizo mtoa mada unadhani kila mtu anandugu dar au anakaa dar. Bora hata saivi dodoma ni kati kati
Hayo ni maoni yako! Ya kwangu hapo bayana kwenye Uzi, usahili ufanyike kikanda! Zone au warudishe kwa wakurugenzi wa wilaya
 
Hiyo idara haijui concept ya equal opportunity in employment
Walaji wa rushwa kupitia unequal opportunity in employment
 
Wakati unafanyika Dsm watu wa dsm hakukua na kelele,, Kama unataka kazi choma hiyo nauli asee
 
Serikali ipo nyuma sana kiteknolojia, sjui hawana watalaamu au waliopo hawafanyi kazi zao. Yaani hata website ya wizara tuu kuupdate katibu mpya mpaka baada ya miezi.
 
Serikali ipo nyuma sana kiteknolojia, sjui hawana watalaamu au waliopo hawafanyi kazi zao. Yaani hata website ya wizara tuu kuupdate katibu mpya mpaka baada ya miezi.
Memkwa ndo walioshikilia vyeo
 
Serikali ina watu wazembe sana. Halafu kila siku wanalilia nyongeza ya mishahara. Unakuta wizara au taasisi ina website ila hata kuapdate au kuweka vitu hawaweki
 
Serikali ina watu wazembe sana. Halafu kila siku wanalilia nyongeza ya mishahara. Unakuta wizara au taasisi ina website ila hata kuapdate au kuweka vitu hawaweki
Tabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…