Mpaka sasa hakuna Ajira yoyote mpya kwa JWTZ, Polisi wala Madaktari iliyotolewa na sserikali
Ajira sio suala la siri, serikali inapoajiri kila mtu anaweza kujua hata kama wasipotangaza.
Kilichofanyika hasa ni hiki..
-Kuna Askari wa Polisi waliomaliza mafunzo yao kwenye chuo cha polisi na kwenda moja kwa moja kwenye vituo vyao vipya vya Ajira na wakaanza kulipwa mishahara, lakini mara tu zoezi la uhakiki lilipoanza wakaondolewa kwenye mfumo wa utumishi, kwa sasa wanalipwa Posho tu.
-Kuhusu MUHAS kule Mluganzira, Muhimbili waliomba kuajiri jumla ya Watumishi 1500 na zaidi, lakini watumishi wote hao ni wale ambao tayari wapo serikalini(Maana yake ni UHAMISHO) lakini serikali ikazuia hiyo kitu juu kwa juu na baadaye imekuja kutangaza kutaka kuajiri watumishi 150 tu badala ya 1500 lakini haijajulikana kama watakuwa ni watumishi wapya kabisa au ni wale wakuhamishiwa tu(yaani tayari wako na ajira serikalini).
Mpaka sasa hakuna hata Mtumishi mmoja iwe Daktari au mlinzi aliyeajiriwa pale Mluganzira MUHAS hospital mpaka dakika hii toka tangazo la serikali litolewe.