Utumishi mtuangalie na sisi wa mikoani!

PASSIONATE

Member
May 20, 2015
69
27
Nitangulize salamu,
Habari wana JF, nimepata nafasi ya kuitwa kwenye written interview ya WCF pale DUCE, namshukuru Mungu kwa hilo, ningependa kutoa maoni yangu kwa hawa wawezeshaji a.k.a utumishi kutuangalia kwa jicho pevu sisi watu wa mikoani, walau usaili wa kwanza uwe unafanyika kwenye ofisi ya kila mkoa then unaofuata ndio sasa mtuite huko Dar es Salam.

Kwa kweli umekua mwiba mchungu sana kwa sisi tulio mkoani kwa kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa sana za kiusafiri hasa ikitegemewa ni haki ya msingi kwa kila aliyeomba na kuitwa.

N.B: Wakuu mlioshika makali chukulieni hili suala kama changamoto kwani Tanzania sio Dar es salam tu, hivi asilimia kubwa ya wanaoishi huko sio wazawa ni watu wa mkoani, hivo msijisahau kila mtu ana haki katika hili, naandika hivi kwa uchungu mkubwa kwani hii ni mara ya pili kushindwa kuhudhuria interview kwa changamoto za nauli ili hali sifa ninazo na nimeitwa.
Tulihubiri haki, mungu ibariki Afrika, mungu ibariki Tanzania.
Mungu wape upeo walioshikilia vyombo vya maamuzi ya wengi, Amen.
 
Hivi post za compliance officer maswali yake yanakuaje mwenye kujua atusaidie
 
Tuwe tunafanya aptitude online then hatua zinazofuata ndio mtuite huko Dar es salaam, naomba kama wanaweza ku design kanzudata kwa ajili ya aptitude itatusaidia sisi tulio huku mikoani
 
Watu 800+ nafasi 2, hii ina tofauti gani na uhamiaji. Tena bora ile ilikuwa watu 140+ wanashindania nafasi moja, hii watu 400,nafasi moja
 
Hapo kweli ni kama kule lilikoungua jembe na mpini ukabaki maana waweza unguza nauli, bado mtihani, sijui ndo mnaitwa Written Interview ukafeli na huku nyumbani mmeuza mbuzi ili upate nauli na ukirudi hujafaulu ndugu watakuona kilaza hivyo mwishoni utabaki palepale yaani Msomi Masikini.
Lakini kama unajishughulisha na unajitegemea waweza kujitegemea uende na uwe positive kwamba utaweza pasi na kujali marefarii maana Mungu akiamua kukupa unaweza kufunga goli kwa kisogo licha ya kuwa na kidonda kichwani.
Pamoja na hayo, hii serikali ya majipu na viwanda ione namna ya kuwasaidia wanyonge kwa kusogeza huduma kwenda kanda badala ya kulazimisha Dar es salaam au kwa kuwa kuna daraja la Nyerere?
 
Dar es salaam bana kila kitu ndo huko huko, mtufikirie tusiokua wa Dar es salaam, wakuu wa vitengo mbona online aptitude ni jambo rahisi tu.
 
Nitangulize salamu,
Habari wana JF, nimepata nafasi ya kuitwa kwenye written interview ya WCF pale DUCE, namshukuru Mungu kwa hilo, ningependa kutoa maoni yangu kwa hawa wawezeshaji a.k.a utumishi kutuangalia kwa jicho pevu sisi watu wa mikoani, walau usaili wa kwanza uwe unafanyika kwenye ofisi ya kila mkoa then unaofuata ndio sasa mtuite huko Dar es Salam.

Kwa kweli umekua mwiba mchungu sana kwa sisi tulio mkoani kwa kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa sana za kiusafiri hasa ikitegemewa ni haki ya msingi kwa kila aliyeomba na kuitwa.

N.B: Wakuu mlioshika makali chukulieni hili suala kama changamoto kwani Tanzania sio Dar es salam tu, hivi asilimia kubwa ya wanaoishi huko sio wazawa ni watu wa mkoani, hivo msijisahau kila mtu ana haki katika hili, naandika hivi kwa uchungu mkubwa kwani hii ni mara ya pili kushindwa kuhudhuria interview kwa changamoto za nauli ili hali sifa ninazo na nimeitwa.
Tulihubiri haki, mungu ibariki Afrika, mungu ibariki Tanzania.
Mungu wape upeo walioshikilia vyombo vya maamuzi ya wengi, Amen.
kiongozi ebu yaweka hapa majina kidogo kasimu changu ni kadogo
 
Watu wa utumishi ktk hili jambo wamekosa ubunifu kabisa, na wamekosa shabaha!. Nadhani wanahitaji wafanyiwe maombi mle ofisini kwao ili akili na fahamu zao zifunguliwe kuhusu kipengele cha watu watokao nje ya dar es salaam hasa ktk written interview. Sisi wengine tumebakiza kwenda interview ktk nafasi ambazo hazina written interview otherwise sio lazima wote tufanye kazi serikalini. Mpaka sasa sijahudhuria wito wa kwenda kufanya written interview idadi imefikia 18 na bado sichoki kuwatumia applications pale ninapoona nina sifa ya kuomba ktk tangazo watakalolitoa. ha ha haah! wewe mara mbili mbona bado sana!, (assumptions: unaenda written interview ktk masafa kama haya; songea_dar, Sumbawanga/mby_dar, Kigoma_dar, geita/mwz_dar, musoma_dar etc hapo nimekuonyesha city centres, fikiria unatokea madongo kuinama unakuja city centre then unaelekea dar, hapo ndpo hesabu za nauli zitakukaa vizuri)
 
Back
Top Bottom