UTUMISHI MMETUSAHAU SOCIAL WELFARE II?

UTUMISHI MMETUSAHAU SOCIAL WELFARE II?

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
25,284
Reaction score
40,902
Habari wanaJF,

Nimekuja kwenye jamvi hili kujaribu kufikisha ujumbe kwa Secretariati ya Ajira (PSRS),kuna usaili wa AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II ulifanyika tarehe 02/12/2017 wa mchujo pale Mwalimu Nyerere Kiganmboni,na baada ya mchujo tukapita 53 na kisha kufanya usaili wa mahojiano tarehe 06/012/2017,nakumbuka siku ile tulikuwa na Mawakili wa Serikali wengi sana ambao pia walikuwa na usaili wao wa mahojiano.

Cha kushangaza tangu mwaka jana hadi leo hakuna watu walioitwa kazini,japo wenzetu Mawakili walishapangiwa vituo muda mrefu ila kwa post ya AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II ni kimya hadi leo.Jambo hili linakatisha sana tamaa,angalau wangechukuliwa watu kadhaa lakini hadi leo ni karibia mwezi wa tatu hakuna dalili yoyote.

Naomba mjaribu kupitia taarifa zenu,tunateseka sana tunaotoka Mikoani kuja hapo Dar kila wakati na hatupati mrejesho wowote.

Nawasilisha:
Ndumbula Ndema
 
Back
Top Bottom