Utumishi: Kwanini uhakiki wa vyeti haugusi vyeti vya digrii?

Ni kwa sababu watu wengi walifoji vyeti vya O/A level na kuvitumia kujipatia degree isivyo halali kupitia hivi vyuo vya mtaani. Mfano mmoja hai kabisa ni Davido Alberto Bashite almaarufu kama Paul C. Makonda
 
Vyeti vya digrii vinapatikana kirahisi kadiri mtu anavyopanda ngazi za kielimu.Kule unapata digrii unaiona hivihivi.Vyeti vya sekondari ni shughuli pevu kuvipata.mitihani yake yataka usome kwa bidii na kutunza kumbukumbu vizuri kwa mambo uliyofundishwa.Ukifeli hupati cheti na elimu uliyoipata haitambuliwi na waajiri utajitambua mwenyewe na kujiajiri mwenyewe.Digrii unafanya kazi nyepesi kuipata
Huna digrii wewe! Au una cheti feki cha digrii
 
ndio unapata! ila utapata cheti feki kama yule ambaye hakusoma sekondari lakini ana cheti cha sekondari. uliza swali lingine
. UDSM na SUA wako makini sana na wameshawambua wengi waliotaka kuleta ujanja wengine walilazimika kukimbia vituo vyao vya kazi baada ya kubainika wamefoji vyeti vya taaluma.
 
vyeti feki vya degree ni vingi sana mtaani.sijui watawezaje kuvibaini,maana Tcu wamelala usingizi wa pono.
 
Mazingira ya kupata digrii ni rahisi sana no matter ni digrii gani na chuo gani. Hii ni tofauti na vyeti vya elimu ya kawaida hasa sekondari ya chini. Ndiyo maana mikasa mingi ya vyeti vyenye utata ni vya sekondari.Sekondari ndiyo lango la kutokea kwenda kwenye elimu ya juu.Wanaosoma elimu ya ni watu wazima na wana uzoefu wa mambo mengi wanayojifunza huko.Kuipata digrii ni rahisi si sawa na kupata cheti cha sekondari
 
Hakika inatisha sana.Tunaiomba Wizara ya Utumishi ianze Uhakiki Wa Digrii Kwa Watumishi Wa Umma kwani nako kuna MADUDU ya kutisha.kuna mtumishi Ana kamaliza kidato cha 4 Ana Certificate ya Uchoraji lakini anaruhusiwa kuchukua DIGRII ya Mipango Miji.Hao ni wengi sana.Tunamwomba Waziri husika afanye Uhakiki Kwa wote wenye DIGRII.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Sasa si bora hata huyo mwenye setifiketi ua uchoraji akapata digrii ya mipango miji ataweza kuutumia ujuzi wake wa kuchora kutuchorea namna ya kupangika kwa mji
 
Kwa sasa serikali imehakiki vyeti vya sekondari kwa watumishi wa umma! Vyeti vyenyewe ni vya sekondari yaani form four na form six! Hapo hapo, wanatueleza eti ajira mpya zinaziba pengo la watumishi wenye vyeti feki! Hivi, tofauti na kazi za udereva na walinzi ni kazi gani nyingine inayotangazwa na serikali inayomhitaji MTU awe na cheti cha form four au form six? Kama utumishi mnataka kutoa ajira kwa watanzania, mjitahidi mhakiki watumishi wenye digrii feki! Naamini hawa wapo wa kutosha!

Nafikiri hii ndio Prof. Shivji aliita wenye vyeti halali lakini elimu fake. Na hao wapo tu kwani kuna mchezo fulani ulikuwa unafanyika katika chuo fulani miaka fulani wa kupandisha alama za ufaulu kwenye transcript wakati kwenye taarifa za ndani alama zipo chini na sio rahisi mtu kufatilia kutokana na hicho chuo husika ambacho kinajigamba kuwa chuo cha kwanza Tanzania na bora zaidi.

Na kwa mfumo huo alama halisi za ufaulu uhifadhiwa kwenye idara na kitivo ambako ule mchezo wa kubadili kwenye kile chumba cha kutolea transcript pale floor ya pili sijui kwenye jengo lao la utawala, wale wamama wachapishaji ndio walikuwa vinara wa mchezo huo. Sijui kama computerisation imeodoa hilo tatizo.
 
Hivi aliyewaambia degree ni rahisi ni nani.Kama ni rahisi si kila mtu angepata.Mnajifariji.
Mkuu Degree first year mnaanza 80 mnagraduate 70 O level form one wanaanza 80 wanaopata cheti 40 huoni hapo secondary wengi wanapotea.Secondary mazingira pia magumu Chuo ni kugumu lakini at least mazingira yanaruhusu.
 
Uhakiki wa vyeti vya Taaluma unapashwa kufanywa na chuo husika tuu, kwakuwa wao ndio waliokitoa cheti hicho.Nitofauti na vyeti vya secondari ambavyo hutolewa na Baraza la mitihani tuu.
 
Kwa sasa serikali imehakiki vyeti vya sekondari kwa watumishi wa umma! Vyeti vyenyewe ni vya sekondari yaani form four na form six! Hapo hapo, wanatueleza eti ajira mpya zinaziba pengo la watumishi wenye vyeti feki! Hivi, tofauti na kazi za udereva na walinzi ni kazi gani nyingine inayotangazwa na serikali inayomhitaji MTU awe na cheti cha form four au form six? Kama utumishi mnataka kutoa ajira kwa watanzania, mjitahidi mhakiki watumishi wenye digrii feki! Naamini hawa wapo wa kutosha!
Mkuu unapokuwa enrolled kwa degree ni lazima uwakilishe vyeti vya Form IV na VI.Halafu hata kama ni mature entrant system yake ya scrutiny v
Mkuu Degree first year mnaanza 80 mnagraduate 70 O level form one wanaanza 80 wanaopata cheti 40 huoni hapo secondary wengi wanapotea.Secondary mazingira pia magumu Chuo ni kugumu lakini at least mazingira yanaruhusu.
Kijana unazungumzia mazingira mawili tofauti kabisa ambayo hayako comparable.Kwa sababu ya umri mdogo:-
1.Sekondari vijana hawajitambui.
2.Hawana malengo
3.Hawana commitment,kwa hiyo ni lazima wafeli.
On the other hand Chuo Kikuu kwa sababu vijana wamekomaa,wana malengo,wanajitambua na kuna commitment, ni lazima wafanikiwe!
 
Uhakiki wa vyeti vya Taaluma unapashwa kufanywa na chuo husika tuu, kwakuwa wao ndio waliokitoa cheti hicho.Nitofauti na vyeti vya secondari ambavyo hutolewa na Baraza la mitihani tuu.
Ni kweli
 
Back
Top Bottom