Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,629
- 2,288
Kwa sasa serikali imehakiki vyeti vya sekondari kwa watumishi wa umma! Vyeti vyenyewe ni vya sekondari yaani form four na form six! Hapo hapo, wanatueleza eti ajira mpya zinaziba pengo la watumishi wenye vyeti feki! Hivi, tofauti na kazi za udereva na walinzi ni kazi gani nyingine inayotangazwa na serikali inayomhitaji MTU awe na cheti cha form four au form six? Kama utumishi mnataka kutoa ajira kwa watanzania, mjitahidi mhakiki watumishi wenye digrii feki! Naamini hawa wapo wa kutosha!