Utumishi, chunguzeni Interviews za UDOM

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Majuzi kati ya June na July UDOM wali tangaza nafasi za kazi kada mbalimbali. Baada ya muda wa maombi kuisha utumishi waka chapisha tangazo la kufuta nafasi ya Kazi hizo Hatujui tatizo ni nini.

Baada ya wiki 2 hivi kazi hizo zili tangazwa upy a na utumishi wa umma. Kwa sababu maombi ni online na mfumo una tunza taarifa, walio omba mara ya kwanza hawakuweza kuomba tena upya, coz system ilikuwa ina onesha tiyari umeomba nafasi hiyo. Hivyo huwezi kuomba upya.

Maajabu ni uwazi wa chuo hiki katika Ajira zake tofauti na vyuo vingine. Miongozo ya utumishi mipya ina vitaka vyuo vikuu, Institutes, Ministries, LGAs na Agencies zote za serikali kazi zake kutangazwa na kusimamiwa mchakato wote na utumishi wa umma.

Vyuo vyote majina ya kuitwa either Written or Oral interview huwekwa website ya Utumishi wa Umma, kwa ajili ya watanzania wote kujua na for fairness na transparency.

Ila maajabu ya UDOM mwezi huu wana pigia baadhi ya watu simu kuhudhuria interview chuoni kwao bila ya Tangazo la kuitwa Interview kuwekwa hadharani either ktk website ya chuo au website ya utumishi!! Kuna mtu wa Kada ya Education kaitwa interview UDOM kwa simu (J5 to Thursday ijayo) baada ya mtu wake wa karibu kufuatilia.

Tuta amini vipi kuwa walio itwa ni hao walio pata hiyo kazi? Tangazo uliweka public, why ulio waita interview ufiche? Je ambao hawajaitwa na wana sifa zote na Notification system ya Ajira portal iko silent kuwa interview bado watajua vp mapungufu ya maombi yao? Je tuachaje kuhisi harufu ya upendeleo au rushwa ktk nafasi hizi adimu za umma?

Tuna omba utumishi: Wafute Ajira hizo. Na watu wote wenye sifa waitwe upya kwa uwazi. Yaani taratibu zote za utumishi zifuatwe.

Simu hufanywa na Private Organizations/Companies. Watu 1000 huwezi piga simu!!

Pia, mitihani isi tungwe wala kusimamiwa na vyuo bali zoezi zima lote liwe chini ya utumishi.
utumishi na @ajiraportal na @PCCB. Nafasi 215 ni nyingi.
View attachment 2351700
 
Hata mkiitwa wote usaili, watakaopita kwenye written ni hao waliopigiwa simu, wengine mtakadiriwa alama chini ya 50 na huna Cha kuwafanya
Utumishi wata simamia zoezi upya. Kuita written na ku fanyisha usaili. Mnapigwa wote pepa matata (written). Afu, wenye bahati yao wata toboa kwa haki na uwazi.
 
UDOM ni chuo kikuu ila wanafanya mambo kihuni. Wana fundisha vitu ambavyo wao hawa implement. Baada ya mm kuanzisha huu uzi mapema tarehe 9/9/2022 na wao usiku huo huo wametoa orodha ya majina yao (cooked) ya watu walio itwa interview ( kwa ajili ya interview).

Bado nasimamia msimamo ili kujenga nidhamu, uwazi na haki ktk taasisi. Nina omba utumishi futeni hayo majina yote na Selection pamoja na mchakato mzima wa interview ufanywe na utumishi. Hayo majina tiyari yako na Interest zao ndani. Pia HR wa UDOM na DVCs wa Administration, Academic UDOM wawajibishwe. View attachment 5632_attachment_457 (1).pdf
 
Pia uki linganisha Tangazo la Nafasi za Kazi na Tangazo lao la kubumba la kuita watu Interview (9/9 usiku) , uta gundua kuna kada nyingi sna hawajaita watu. (Kwa nini? )
Je wameweka haya majina baadhi tu, kama sample ya kutuhadaa umma eti procedures zimefuatwa?

UDOM acheni uhuni wa kitoto. Do what you Preach in Classes.
 
Back
Top Bottom