Utumiaji usahihi wa dawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumiaji usahihi wa dawa

Discussion in 'JF Doctor' started by Che Kalizozele, Oct 29, 2008.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kutujalia afya njema kwa tuliobarikiwa hilo.Nimeamua kuliongelea hili la utumiaji sahihi wa dawa kwa sababu nahisi ni miongoni mwa vitu muhimu ambavyo avijapewa kipaumbele ukilinganisha na nchi za wenzetu,inawezekana tatizo ni elimu ndiyo maana nami nimeamua nianzie hapo.

  Hapa utumiaji sahihi wa dawa namaanisha kutumia dawa kulingana na maelekezo uliyoyapata kutoka kwa wahudumu wa afya na yale nitakayoyasema hapa.

  Umuhimu wa kutumia dawa kwa usahihi.

  v Dawa ni sumu
  Dawa inakuwa dawa pale tu inapotumika ipasavyo,kinyume chake dawa uweza kusababisha madhara makubwa wakati mwingine kusababisha kifo na ndo maana tunasisitiza dawa itumike kwa usahihi bila ya makosa YANAYOWEZA KUZUILIKA
  v Ili kupata matokeo unayoyatarajia.
  Lengo la kutumia dawa ni kutibu maradhi yanayokusumbua,ili linawezekana pale tu dawa husika zitakapotumika ipasavyo na inavyotakiwa kulingana na maelekezo,la sivyo utabaki kulalamika tu,ooooh malaria yangu haisikii dawa kumbe unatumia dawa ndivyo sivyo.  ILI UWEZE KUTUMIA DAWA KWA USAHIHI.
  Sikiliza kwa makini na fuata maelekezo kutoka kwa wahudumu wa afya
  Hii itasaidia kupunguza makosa wakati unatumia dawa husika,usijifanye Kujua wakati haujui lolote.Dawa hazina uzoefu na wala Hakuna haja ya kujifanya una haraka Kiasi cha kukosa japo dakika mbili za kusikiliza maelekezo ya jinsi ya kutmia dawa zako.Sehemu ambayo haujaelewa uliza,kwani Hakuna kitu cha hatari kama kutumia dawa kwa kudhani tu utakuja kujidhuru.
  Utawasikia wengine,"we nipe bwana,hizi dawa tunatumia kila siku"
  Wakina sie,"Usiandike,najua jinsi ya kuzitumia" Wewe unafikiri karanga hizi.

  Heshimu na fuata maelekezo ya daktari wako.
  Uzoefu unaonesha wengi wetu hatuwaheshimu madaktari wetu Kiasi cha kufanya tofauti na maelekezo yao.Kwa mfano utakuta mtu akumaliza dozi,au hakutumia zile dawa alizoandikiwa na daktari wake,halafu anarudi kwa daktari wake au daktari mwingine na kuanza kulalamika kuwa ameshatumia dawa na bado hajapata nafuu,kumbe tatizo ni yeye.Ni vizuri ukawa wazi mapema kwa daktari wako kwamba dawa alizokupa hautoweza kuzitumia kwa sababu kadhaa wa kadha,kuliko ukaenda kubadilisha dawa juu kwa juu,utakuwa haumtendei haki daktari wako.Hivyo ni vizuri ukatoa maelezo yaliyokamilika kwa daktari wako na pia ukafuata maelekezo yake kwa ukamilifu,na pale unapotaka kufanya tofauti na maelekezo yake kama kuna uwezekano wa kumtaarifu,ni vizuri ukafanya hivyo.

  Siku zijazo nitachokoza kuhusiana na mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza kutumia dawa,nasubiri michango yenu katika uchokozi huu wa leo
   
Loading...