Utulivu wa nafsi na akili

Utulivu wa nafsi na akili

Noe_wenc87

Member
Joined
Oct 25, 2018
Posts
8
Reaction score
5
Habari zenu wakuu, kuna kitu kinanitatiza na nahisi kwangu kina umuhimu. Suala la utulivu wa akili yaani Meditation.

Nimesoma kwenye post tofauti zilizopita humu na katika blogs kadhaa lakini bado sijajua naweza vipi kufanya meditation.

Tafadhari mwenye uelewa juu ya hili msaada naomba kwa lugha nyepesi ambayo naweza kuelewa.

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
habari zenu wakuu ...kuna kitu kinanitatiza na nahisi kwangu kina umuhimu ...suala la utulivu wa akili yaani Meditation .
Nimesoma kwenye post tofauti tofauti zilizopita humu na katika blogs kadhaa lakini bado cjajua naweza vipi kufanya meditation ..Tafadhari mwenye uelewa juu ya hili msaada naomba kwa lugha nyepesi ambayo naweza kuelewa .ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app

TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia - JamiiForums
P
 
Kuna jamaa flani Wakorea wako wanakaaga Kwenye baadhi ya maeneo na vipeperushi, kuna vituo vyao wanaelekeza namna ya kufanya Meditation, tena njia zao nzuri na fupi kiasi cha kuona matokeo mapema!
Kuna kulipia lakini !
 
Ila kuna baadhi ya meditation zinapelekea ukiri wa wale waanzilishi wa hiyo kitu Kama Mungu flani,
Ambapo nikifikaga hapo huwa najitoa !
Ukiri wa mambo flani ina impact kubwa sana Kwenye Ulimwengu wa kiroho na huu wa nyama!
 
Yani hii kitu ingekuwa intergrated na maombi ya kanisani ingekuwa nzuri zaidi!
Ni Kama ilivyoandikwa " mtwikeni Yesu fadhaa zenu zote"
Kwa hiyo Mtu unakaa sehemu ya utulivu kisha unaanza kutupa kila fadhaa na tukio toka ulivyoanza kijua jema na baya hadi hapo ulipo sasa!
 
Utaanza kuona binadamu wote ni Sawa , utawapenda Watu wote bila kujali udhaifu na makosa yao!
Hutakuwa mwepesi wa kuwaka hasira!
Utakuwa mwepesi wa kusema ukweli hata Kama umefanya makosa!
Hutatafuta kujitetea!
 
Hutatafali utajiri au mafanikio ulonayo!
Huyajiona bora kuliko mwingine!
Hutakuwa na hofu yoyote ile !
Utajiona mwepesi na kufurahi na kila Mtu hadi watesi wako!
Hadi wale ambao umethibisha pasipo Shaka kuwa hawakupendi na wamekufanyia mabaya lakini Wewe utawapenda tu na kuwaachilia!
 
usitake kufanya kila hatua kama wao lengo lako umeshajua kua unataka utulivu wa nafsi na akili bhasi

ni rahisi wakati naanza nilipata shida sana kwa kua nilitaka kufanya exactly kama wao ila baadaye nilikuja kuona ni ngumu kutokana na utofauti wetu wa nafsi akili na mazingira.

Leo nafanya meditation popote hata bar nikilewa naweza kutafuta dakika tano tu na kuzingatia amani ya akili na nafsi yangu na kufurahia sana.

kwa maneno marahisi meditation ni kupata utulivu wa nafsi na akili na kuufurahia wakati uliopo.

unaweza kufanya popote na vyovyote kikubwa ni kuifundisha akili yako kuazimia kuanza

nakutakia kila la kheri katika kujaribu tafuta namna yako ya kuanza pata kujifahamu kwanza
 
Indeed inafaa kwa Watu wa imani zote !
Uwe Mkristo au Muislam n.k meditation inafaa sana!
Na unaweza kukuta Mtu Kama yuko na idea ya imani Yake basi during meditation kiwango chako cha imani kinaweza imarika kidogo!
 
Yani fahamu zinatakiwa kuwa Kama za watoto!
Tunapaswa kuwa simple and innocent muda wote!
Kuanza ku argue kwa kila la kitu ni shida Kwenye nafsi ya Mtu!
Things like curiosity and canning havishauriwi kabisa Ili kuweza kuwa na utulivu wa akili na nasfi ya Mtu!
 
Uwezo wa kupata usingizi wenye ubora Walau kwa Masaa 8 nakuendelea ni mojawapo ya vitu muhimu kwa afya!
Kupata haja ndogo na kubwa kwa Siku mara ni mihimu sana kiafya!
N.k
 
Utaanza kuona binadamu wote ni Sawa , Utawapenda Watu wote bila kujali udhaifu na makosa yao!

Hutakuwa mwepesi wa kuwaka hasira! Utakuwa mwepesi wa kusema ukweli hata Kama umefanya makosa! Hutatafuta kujitetea!

Ee Mwenyezi Mungu niwezeshe kuyatenda na kuakisi haya kwa mwaka 2019 na kuendelea. Amen.
 
Kuna jamaa flani Wakorea wako wanakaaga Kwenye baadhi ya maeneo na vipeperushi, kuna vituo vyao wanaelekeza namna ya kufanya Meditation, tena njia zao nzuri na fupi kiasi cha kuona matokeo mapema!
Kuna kulipia lakini !
Sh.ngapi?
 
Hivi vitu tunavichukulia theoritcal sana. Hizi meditation ni imani za mashariki ya mbali huko. Lakini JAPAN na KOREA wanaongoza kwa matatizo ya sonona na suicides. Kimsingi lifestyle is the key. Ndio maana vijijini watu hawana hela ila wana furaha. Hana ada, hajaacha hela nyumbani lakini amani bado anayo!! TAFAKARI!
 
Back
Top Bottom