Utoh na njia mpya kumsafisha Jairo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utoh na njia mpya kumsafisha Jairo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lokissa, Aug 23, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wanajF, nimesikitika sana kusikiza habari ya TBC mchana huu kuwa jairo hakuomba hela kuwahonga wabunge bali aliziomba idara zilizo chini yake kuchanga hela kufanikisha bajeti na hakuna ushahidi wa wabunge kuhongwa na pia anasema hakuziagiza idara hizo bali aliziomba.Ukisoma habari hii inajichanganya changanya na haina mwelekeo wa kiakili.kwani kuomba au kuagiza sii mwanzo wa rushwa? hilo ombi alitoa la nn??? hizo hela ziende kwa nani?? naona kuna mchezo mchafu unachezwa.kwa mliosikiza news hebu tujuzeni vema na mwenye hiyo tarifa aiweke kwa kina hapa.samahani kama itakuwa imeshatolewa hapa ila sijaiona.natanguliza.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  rotten system..all system!
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna la zaidi lilitegemewa? Jairo hakuwa peke yake kwenye hiyo issue - angetoswa pengine angevujisha siri.
   
 4. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jairo alijua tangu mwanzo kuwa hakuna lolote......ndio maana akawaita Wabunge ze comedi.

  Welcome back comrade Jairo. Nafasi ya Luhanjo (baada ya kustaafu) ni yako, kama ilivyopangwa awali.

  Nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya haki na uhuru, si kwa jazba kama walivyofanya wabunge. Wenye wivu wajinyonge.
   
 5. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Huu ni upuuzi! Kama hii haikuwa rushwa;
  - Je gharama za kuandaa budget ya 2011 hazikuingizwa kwenye budget ya 2010?
  - Fedha zilizoombwa kwenye hizo idara zilitolewa kwenye fungu gani?
  - Malengo yaliyokusudiwa kwenye idara hizo yatakamilishwa na fedha gani?
  - Payment vouchers za malipo haya huko kwenye idara zinaonyesha yalikuwa malipo ya nini?
  - Hizo fedha zimefanikishaje hiyo budget?
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  like the father,,,,,,,,,,,,,,,,, like the son!!!
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Very simple......zimetoka kwenye fungu(mafungu) ya ukarimu (Hospitality).
   
 8. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kwanza : alejeshe ile ela kimya kimya kama ya EPA hatutamchukilia hatua.
  Pili: hakuhusika kwenye Budget Iliyopitishwai je yeye atashiriki vipi kuitekeleza kama katibu mkuu?
  Tatu: Kama kweli ndo hivyo Wanaweza kutwambia kuwa Mh Waziri Kiongozi alipitiwa kutoa kauli ile Bungeni ya kumfukuza kazi immediately?
  Nne: Je uhusiano wake na Wabunge na watendaje wenzake serikali utakuwaje baada ya kuwa ameishapata doa ila limesafishwa na amepona?
   
 9. H

  Heri JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Palikuwa hakuna haja ya CAG kuchunguza kama ilikuwa straight foward. Katibu kiongozi angeita press conference siku ileile na kutueleza haya. Ina maana PM hajui serikali inaendeshwa vipi mpaka atoe kauli ile? CAG na Katibu Kiongozi mnamuweka PM in a very difficult corner and situation. Hana meno.
   
 10. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  barua aliyoandika Jairo haiwezi kumtia hatiani yule mbunge ilitakiwa awe kimya mpaka apate ushahidi wa kutosha mbunge alikurupuka
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  wote ni wezi na wanafikiria kwa kutumia masaburi.
   
 12. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  basi PINDA ni MWONGO, MZUSHI, MSINGIZIAJI WA WENGINE, HAJUI ANACHOSEMA, HAJUI SERIKALI INAENDESHWAJE... KATUELEZA JINSI GANI ASIVYOWEZA KUFANYA KAZI NA JAIRO...KWA HIYO ANAPASWA KUJIUZULU KWA ALISEMA ANGEKUWA YEYE ANGESHAMTIMUA JAIRO....AIBU YAO. WANA IGUNGA KAZI KWENU!
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwani hiyo TBC si ya mafisadi? Jairo ni fisadi, serikali ya JK ni ya Mafisadi sasa kwa nini mafisadi wabaguane? Ni sawa na kumshika ngedere na kwenda kumshitaki kwa nyani.
   
 14. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Nchii hii inaongozwa kiswahili swahili, huko ndani wanawaza mdundiko, shughuli na kumtoa mwali huku ubwabwa kwa wingi.
  Wajanja wanachomeka dili zao humo ili angalau wasife bila kuendesha vogue na V8!
  Utumishi wa umma kwao ni msamiati wako pale kuangalia kwenye akaunti zimeingia ngapi.
  Ukosefu wa umeme hawaoni kama ni janga la taifa; hawanunui lulu, hawanunui mafuta ya magari yao wala kulipia bill za maji kwa pesa zao - wanatumia pesa za walipa kodi.
   
 15. m

  mams JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  halafu muendelee kusema serikali ya ccm haichukui maamuzi magumu. Chama gani kingeweza kumsafisha mtu kama huyo na kumrejesha?
   
 16. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Banana republic bandugu,,la kuvunda halina ubani
   
 17. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du!this is too much.ila ninachoamini makusudi ya bwana hayazuiliki.mwisho wao utafika.magumashi waliyoyafanya kusafishana hta mtoto mdogo huwez kumdanganya.
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hajaona aibu kutangaza kumrejesha kazini...hivi kawaona watanzania ni majuha kama enzi zile za ujamaa??? kazi ipo inabidi kuamka sasa upuuzi huu wa kudanganywa kama watoto uishe.sasa tuone PM atasemaje alh kwenye maswali na majibu huenda akasingizia kuumwa au kusafiri gafla..lazima kieleweke alisema atamfukuza katibu mkuu kamsafisha nani mwenye power zaidi yeye Pinda au Luhanjo??? inauma sana.
   
 19. W

  We can JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii yanikumbusha habari ya kina Masaku. MMoja wao alikuwa akituhumiwa kwa wizi na akakana. Jinsi alivyojitetea, iikuwa hivi:

  Mtuhumiwa: Kama nimeiba, nilikuwa nimevaaje?
  Mwongoza mashtaka wa serikali: Ulikuwa umevaa nguo nyekundu,
  Mtuhumiwa: Umekosa, nilkuwa nimevaa nguo nyeusi!

  Hivi kweli nchi hii inamsafisha mtu mwenye EVIDENCE kama hii? Huu ni mtaji mkubwa sana kwa wapinzani walio makini. Ni gear namba 1 hiyo ya kubadilisha nchi hii. Nimekata tamaa kabisa.
   
 20. S

  Singo JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Mimi ningekua waziri mkuu ningejiuzuru sababu aibu ya kudharaulishwa ni kubwa. Bora niwe huru bila kuwa na mali kuliko kuwa na mali na cheo chenye kuniondolea utu wangu. Kazi kwako pinda kama unafikiri kama the most effective people.
   
Loading...