Utofauti wa watoto wa Jana na leo

Utofauti wa watoto wa Jana na leo

Kitangiri15

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
352
Reaction score
767
Juzi nilikuwa nafatilia tabia za binti yetu mdogo hasa katika kipengele cha maadili ya salamu na chakula ukizingatia kwamba kwa sasa wana likizo inayotupa fursa wazazi kukaa nao kwa mda mrefu. Tukiwa na wife katika eneo la biashara alikuja mtu akanunua pipi na kumpa BINTI yangu,dakika chache mbele fundi cherehani alinunua chipsi na kumwita binti yangu mdogo wakala pamoja na baadae kuna kibinti kilikuwa kinakula mihogo pia walikula pamoja.
Jambo hilo limenifanya nifikirie na kukumbuka zamani tulipokuwa wadogo ilikuwa sio rahisi kupokea chakula kwa mtu yeyote bila maelekezo ya mzazi au mlezi.
Nimewiwa kushare nanyi kisa kilichonitokea miaka kadhaa kijijini kwetu.fuatana nami.........
Mama yangu alikuwa amepiga marufuku kula kwa watu hovyo na ikitokea hivyo basi ujue ni kwa idhini yake. Mara nyingi tulipoambatana pamoja hata mkikaribishwa chakula nitakataa kula lakini yeye atakwambia kula nakusubiri na nikimtizama usoni najua kabisa hapa nile au nisile.
Siku moja mimi na mdogo wangu wa kike tulikuwa tunacheza nyumba ya jirani na walikuwa wanapika wali( chakula adimu na cha heshima kwa watoto kijijini) walipokaribia kuivisha kumbe mdogo wangu alishausoma mchezo na kukimbia home mie mchezo ulikolea hadi chakula kikatengwa mezani.to be honest nilikataa kula japo moyoni niliutamani ule msosi.Baadae nikaamua kula kwa kujua kuwa hakuna wa nyumbani wa kuniona.baada ya msosi tuliendelea kucheza na jioni nilirejea home. Dada yangu alienda kuniosha kisimani na niliporejea home walikuwa wanapika wali (moyoni nikafurahi) kilichotokea baadae ndicho kimenifanya niandike hapa Leo.
Niliona furushi la fimbo pembeni ya mlango nikaanza kunusa kitu cha tofauti, kaka yangu kabla sijatoroka alinishika mkono na kunipeleka kwa mama sebuleni. Mmoja alinishika miguu miwili na mwingine mikono as if wanabanika kuku matako juu mama alinisomea mashtaka yangu kisha bila hata kujitetea nilipokea adhabu Kali. Nilichapwa sana mpaka ikafikia hatua nikawa si sense maumivu.kutokana na fimbo zile mama alinipasua tako LA kushoto na kuanza kuvuja damu nilipakwa chumvi na kuachwa nikiugulia maumivu .nilijilaza juu ya kochi nikisikilizia maumivu. Kwa kuwa nilikuwa mroho wa wali na kushindwa kufuata maagizo ya mama nilitengewa sinia la wali nile peke yangu.kwa kweli sikuwa na hamu na wali ila kadiri nilivyo jitahidi kula niliona sijapunguza kitu. Mungu hamtupi mja wake. Kuna ndugu yetu mmoja alikuwa na tatizo la akili na usiku ule alitoroka kituo cha tiba alipofika pale kwetu chakula kiliisha isipokuwa sinia langu la adhabu ilibidi nile nae na ndio ikawa pona pona yangu.
Toka siku hiyo hali ile ni kama iliniathiri kisaikolojia nikikaribishwa chakula huwa nahisi mama yuko pembeni na atanichapa.
 
mkuu mkanye mwanao hiyo tabia sio nzuri atakuwa nayo, kuna jamaa nimesoma nae chuo kila tulichokua tunakula na yeye anataka tena anaweza kukirukia bila kunawa
kuna siku tupo kwenye harusi fulani tukapewa cake nzima kubwa watu kama 5 tukaikata vipande tukawa tunakula kidogo kidogo na yeye akiwemo,ghafla akainyanyua akaanza kula peke yake kama ugali
 
Kuna utofauti mkubwa wa watoto wa zamani na sasa.
Naona ananielewa sasa kile ninachomwambia mie mzazi japo anaelewa taratibu labda sababu ya umri(2yrs)
Hii tabia siipendi hata kidogo
 
Kama hujawahi kumkanya kuhusu kupokea vyakula hovyo hovyo utalaumu kizazi bure kumbe tatizo ni wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mkanye mwanao hiyo tabia sio nzuri atakuwa nayo, kuna jamaa nimesoma nae chuo kila tulichokua tunakula na yeye anataka tena anaweza kukirukia bila kunawa
kuna siku tupo kwenye harusi fulani tukapewa cake nzima kubwa watu kama 5 tukaikata vipande tukawa tunakula kidogo kidogo na yeye akiwemo,ghafla akainyanyua akaanza kula peke yake kama ugali
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah aisee umenichekesha sana hasa hapo uipoona mzigo wa fimbo!
Kiukweli enzi tunakuwa ilikuwa kosa kubwa kula kwa watu bila ruhusa ya wazazi kipigo chake usingekaa usahau na hii ilisaidia sana kutengeneza nidhamu wkt tunakuwa!
Jaribu kumkanya na kumfundisha kukaa anapoitwa au kupewa na yeyete isipokuwa ndugu Wa karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna utofauti mkubwa wa watoto wa zamani na sasa.
Naona ananielewa sasa kile ninachomwambia mie mzazi japo anaelewa taratibu labda sababu ya umri(2yrs)
Hii tabia siipendi hata kidogo
kumbe ni mdogo hivo, basi itakuwa huwa hashibi, akikisha mkiwa mnakula nae ashibe vizuri,asicheze wakati wa kula,maana kuna watoto hula kidogo sana na
Mkuu jitahidi kumkanya sasa hivi, akikua na tabia hiyo watakuja kuwa wanamtega na chips anagawa uroda!
dah!!! mbona leo nitatoa simulizi za maisha kama zote
kuna binti fulani ni age yangu nilikutana naye tukawa marafiki sanaa akaanza kunipa stori ya maisha yake ,mama yake alimchapa sana utotoni kisa alikuwa na tabia ya kupenda kwenda kwa watu anakatalia huko mwanzoni niliona huyo marehemu mama yake ni katili sana
lakini baadae nilipokuja kuijua tabia ya binti nikajisemea bora mama yake asingekufa angemfunza tabia nzuri,yule binti anapenda show off yani yupo tayari achukue kitu kizuri cha mtu akatalie yani alipenda maisha yasio yake that explains why alipokua mdogo alikatalia kwa watu,matokeo yake wana walijichapia kwa kutoa pesa
 
Hawa wote wanaoomba hny ninunulie chips au nitumie vocha ndio hao hao
walipitia miaka miwili pia kwa kukubaliwa kula vya watu na wamekuwa nayo tabia hiyo

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwa jirani nilikuwa nakula ila Yule ambae anakuwa family friend haswa.. na nyumbani nilikuwa napakia haswa Tena nakumbuka utotoni nilishawahi kula pilau mpaka nafasi ya kupumua nikakosa😂😂
Nikawa nalalamika sipumui😂😂
Dah! Sijui hata nilitokaje kwenye ile shibe kenge Mimi😜😂
 
"mama Yan kanikataza kula kwa watu" Ndo lilikuwa jibu langu .....hata mpike nini ...
Maana nlionjeshwa Chloroquine (kichapo Siku nilipokula kwa kina Juma Toka Siku hiyo ......Nikaacha kula kwa watu
 
Kwa jirani nilikuwa nakula ila Yule ambae anakuwa family friend haswa.. na nyumbani nilikuwa napakia haswa Tena nakumbuka utotoni nilishawahi kula pilau mpaka nafasi ya kupumua nikakosa[emoji23][emoji23]
Nikawa nalalamika sipumui[emoji23][emoji23]
Dah! Sijui hata nilitokaje kwenye ile shibe kenge Mimi[emoji12][emoji23]
Hahahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom