Utofauti wa plopaganda na uongo ni ipi?

Nashindwa kuwatofautisha hao watu
Tofauti ya msingi kati ya propaganda na uongo iko kwenye lengo, mfumo, na uenezaji wake. Ingawa propaganda mara nyingi hutumia uongo, si kila uongo ni propaganda.

Hizi hapa ni tofauti kuu:
1. Propaganda

.Propaganda ni mfumo maalum wa kueneza habari (ambazo zinaweza kuwa za kweli, za uongo, au zenye chumvi) kwa lengo la kubadili mtazamo au tabia ya kundi fulani la watu.Lengo:

.Kushawishi itikadi, siasa, au imani ya watu ili waunge mkono upande fulani (mfano: wakati wa vita au kampeni za kisiasa).

.Muundo: Huandaliwa na taasisi, serikali, au vikundi vyenye nguvu. Ni jambo lililopangwa kwa muda mrefu.

Mbinu: Hutumia hisia (kama hofu au uzalendo) badala ya mantiki.

2. Uongo (Lies)

Uongo ni kusema jambo ambalo unajua si la kweli kwa lengo la kudanganya.

.Lengo: Kuficha ukweli, kukwepa adhabu, au kupata faida ya haraka na ya kibinafsi.

Muundo: Unaweza kuwa wa mtu mmoja mmoja na wa papo hapo. Haukusudii lazima kubadili mfumo mzima wa fikra wa jamii.

Mbinu: Kugeuza ukweli uwe kinyume chake.
 
Huaga najiuliza je wanasiasa ni waongo au wanapropaganda kupitia nyie nikagundua wanasiasa wengi waongo
 
Huaga najiuliza je wanasiasa ni waongo au wanapropaganda kupitia nyie nikagundua wanasiasa wengi waongo
Propaganda=focus ni kushawishi watu, iwe kwa ukweli, nusu ukweli, au uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…