Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,449
- 574
Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala mbalimbali na ni wazi kuwa kuna mvutano mkubwa sana kati ya Habari za Kashfa ya Lowasa na ya Pinda katika kitu kinachoitwa Ufisadi. Nahisi kama Watanzania wengi tunadanganywa sana kwenye mitandao ya Kijamii.
Najua kuna watu wanakaa kazi yao ni kupiga propaganda ili kujenga imani kwa watu kumuamini mtu wao na kumchafua mtu ambaye wanadhani ni mpinzani wa mtu wao. Hili jambo lazima tuliseme ili kila mtu ajue. Tusitumiwe kudanganya watu kwa manufaa ya mtu mmoja, acheni uma wa watanzania uamue, msiwalazimishe wamuamini mtu ambaye anawalazimisha mumsafishe
Kwa akili yangu ya kawaida nadhani Lowasa ana timu kubwa sana kwenye mitandao ambayo inaeneza Propaganda na kuudanganya uma kuhusu kukubalika kwake na mpaka imefikia hatua watu wengi wanamuamini na kujua ana influence kubwa. Upande wa Pinda kimya chake kinamponza nadhani pia kutokuwa na mtandao wa propaganda pia kunasababisha hayo yote.
Lowasa
Kashfa kubwa ya Lowasa ni Kuhusu Richmond ambapo alijiuzuru kwa kuonekana HAPA NDIYE MUHUSIKA MKUU
Mizengo Pinda
Kashfa kubwa ya pinda ni kufahamu suala la Escrow na kutowawajibisha mawaziri wake HAPA SIO MUHUSIKA MKUU
Kinachokuja kuelezwa kwenye mitandao ni kuonekana kama Escrow ni ya Pinda ilihali hata kwenye Mgao jina lake halipo. ila tu mawaziri wake ndio walihusika. Anaeunda Baraza la Mawaziri ni Rais na sio Waziri mkuu. Anaetakiwa kumuwajibisha Waziri mkuu ni Rais ila tu, waziri mkuu anaweza akapeleka maoni yake kwa rais kuwa waziri fulani kafanya Uzembe. Nini kosa la Pinda katika suala la ESCROW?
Suala la Richmond halikuwa na mjadala wa kuwajibishwa kwa waziri bali Waziri alihusika moja kwa moja na ndiye alikuwa Staring wa Movie ile. Na ukiangalia sana, kwa sasa Pinda ndiye anaechokonolewa sana na kuchafuliwa sana ili tu aonekane hafai, lakini haya yote yamekuja baada ya Kutangaza nia BBC kuwa anaweza kuwania uwaziri mkuu.
Watanzania, ifike mahali tufanye vitu kwa kufikiri. Hawa CCM wakituwekea mtu ambae ana mtandao mkubwa na tukamchagua basi tujue tumekwisha. Kuna watu wanasubiri fulani aingie madarakani ili wao wanufaike kwa dili zao haramu, ndio maana wanamwaga pesa kwa sasa ili waonekane wasafi na wakichaguliwa tu, watarudisha pesa zao na watasababisha wawekezaji feki waingie kwani ndio wanaotoa sapoti kwao.
Sisemi nani anafaa na nani hafai, ila kiongozi anaetumia pesa nyingi na nguvu nyingi kutafuta madaraka ni wazi atatuumiza. kuna watu wana stress zao, tusiwaruhusu kumaliza stress zao kwenye Urais.
Sio kila habari ya kumsifu mtu au kumchafua mtu tunayoiona kwenye mtandao basi tuiamini, tunapaswa kuamini kitu kilichothibitishwa. Mfano ESCROW na RICHMOND hata ripoti zake humu JF zipo, lakini suala la SUKARI sijaona Mwenye taarifa kamili zaidi ya kuhusisha watu wawili ambao ni wapinzani wa wapiga propaganda wa Lowasa.
Vijana wa Lowasa mnatuharibia Watanzania wetu kwa kuwaaminisha vitu vya Uongo huku mkimkweza mtu ambae baadhi ya watanzania walishamuona ni Fisadi, Tusijisafishe kwa kuwachafua wengine.
Hata leo HUNIJUI akisema anagombea urais najua Timu Lowasa watamtengenezea habari tu
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Usimbariki Fisadi yeyote achukue nchi.

Last edited by a moderator: