Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mara binti kapata mimba. Alikuwa anapendwa kweli na licha ya kuwa mara kwa mara walikuwa wanatumia kinga wakati fulani walikuwa hawatumii. Ahadi ilikuwa hata "ukipata mimba tutamtunza mtoto". Sasa binti kapata mimba. Hawako tayari kuwa na mtoto, hawana uwezo wa kulea mtoto kwa wakati huu. Mahali halipo kumtoa mtoto alelewe (adoption) ni kama halipo kabisa.
Binti anapewa pressure kubwa kwamba ni bora atoe mimba ili maisha yao yarudi kama zamani. Na pressure inaongezwa kuwa kama "kweli unanipenda"... binti anapiga mahesabu na kujiona hana "ujanja". Wanaenda kliniki na mimba inachopolewa japo kwa huzuni. Binti moyoni alitamani awe na mtoto wake lakini alijua ingekuwa vigumu sana kuweza kumlea mtoto huyo. Na mimba ilotolewa ilikuwa ni ya pacha.
Ndio mwanzo wa huzuni ulipoanza. Na machozi. Na aibu, na uchungu...
Miezi michache yule binti akashindwa kuendelea na kijana akaamua waachane. Upweke.
Miaka imepita binti kaolewa na yupo na mume wake kwa miaka. Hawajajaliwa kupata mtoto. Na hajawahi kumuambia kuwa amewahi kuwa na ujauzito... na Siri ikaongezeka.
Maskini, miaka inavyokwenda anatamani arudi siku ile .. siku ile.. ile siku ya machozi. Aombe msamaha.
Akasikia niliko.. kaomba ushauri.. amwambie mumewe ili awe na amani..? au aendelee kuombea wajaliwe..
Yakaanza kunilenga machozi... maskini rafiki yangu wa utotoni....