Kinga kingdom
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 769
- 847
Nimejaribu kufuatilia maneno ya Rais Magufuli kuwa mwanafunzi atakaebeba ujauzito kufukuzwa shule.
Kwa ninavyojua mimi hakuna mwanafunzi atakaekubali kufukuzwa shule, akipata ujauzito lazima autoe ili aendelee na masomo.
Hali hii inaweza kuleta madhara yafuatayo siku za mbeleni;
1:Kusababisha vifo kwa wanafunzi wengi wakati wa kutoa mimba, hasa ukizingatia watakua wanatumia njia zisizo salama.
2:Kutengeneza idadi kubwa ya wanawake watakaokuwa na matatizo ya kutopata ujauzito au kutoka kwa mimba kunakosababishwa na kizazi kulegea(abortion result)
3:ONGEZEKO la laana itokanayo na umwagaji wa damu zisizo na hatia.
4:NA IKIWA SERIKALI itaendeleza kuwafukuza wasichana wabebao mimba basi tunatengeneza kizazi cha mabinti au kina mama wajinga wasio na elimu madhara yake tutashindwa kumkomboa mwanamke.
PENDEKEZO: MH.RAIS NAKUOMBA SANA UJARIBU kubadili msimamo wako huo ili itokeapo watoto wetu wamekumbana na ujauzito wasifutiwe haki ya elimu.
Kwanini moja ni ngumu sana kupambana na nature, ikiwa watu wazima wameshindwa kuacha ngono vipi kuhusu vijana wanao balehe na kuvunja ungo?
Hiki kipindi ni kigumu sana kwa vijana wengi hivyo wanahitaji msaada wetu na sio adhabu zetu!
Elimu na guidance ni nguzo ya kuwaokoa mabinti zetu.
Tuwakinge, tuwalinde na tuwalehe na sio kuwatelekeza.
Nawakilisha.
Kinga kingdom.