Utii kwa Mwanaume ni lazima

Utii kwa Mwanaume ni lazima

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
73,323
Reaction score
103,594
Kutii ni jambo la muimu sana kwa mjibu wa ndoa. Hata kabla ya dhambi kuingia katika ulimwengu, kulikuwa na kanuni ya ukubwa/uongozi (1 Timotheo 2:13). Adamu aliumbwa kwanza, na Hawa akaumbwa kuwa “msaidizi” wa Adamu (Mwanzo 2:18-20). Kwa wakati huo huo, kwa vile hakukuwa na dhambi, hakukuwa na utawala mwanadamu kutii ila tu ni utawala wa Mungu.

Wakati Adamu na Hawa walimuasi Mungu, dhambi ikaingia ulimwengu, na hapo mamlaka yakahitajika ili yatekeleze sheria za nchi na pia kutupa kinga tunayohitaji. Kwanza, tunastahili kumtii Mungu, ambayo ndio njia pekee tutakayo mtii (Yakobo 1:21; 4:7). Katika 1 Wakorintho 11:2-3, tunapata kuwa, mwanamume anastahili kumtii Kristo, vile Kristo alivyo mtii Mungu. Tena aya hii yasema kuwa mke anastahili kufuata mfano wake na kumtii mume wake.

Kutii ni jukumu la kimaumbile kwa uongozi wa kupendeza. Wakati mume anampenda mke wake vile Kristo analipenda kanisa (Waefeso 5:25-33), kwa hivyo kutii ni jukumu la kimaumbile kutoka kwa mke hadi kwa mume wake. Neno la Kiyunani ambalo limefasiriwa “kutii,” hupotasso, ni uendelezo wa kitenzi. Hii yamaanisha kumtii Mungu, serikali, au mume si tendo la mara moja.

Ni nia inayoendelea, ambayo itakuwa mtindo wa tabia. Utiifu unaozungumziwa katika Waefeso 5 sio wa sehemu moja kunyenyekea kwa mtu mchoyo anayetaka kutawala. Utiifu wa Kibibilia umepangwa kuwa Wakristo wawili wamejazwa kwa Roho Mtakatifu ambao wamejitolea kwa wao wenyewe na kwa Mungu. Utiifu ni wa namna mbili, kupokea na kupatiana. Utiifu ni hali ya heshima na ukamilifu. Wakati mwanamke amependwa vile Kristo alivyolipenda Kanisa, utiifu sio jambo ngumu.

Waefeso 5:24 yasema, “Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” Aya yasema kuwa mke anastahili kumtii mume wake kwa kila jambo ambalo ni njema na la kisheria. Kwa hivyo, mwanamke kwa vyovyote vile hana chaguo lingine la kutomtii sheria au Mungu kwa kisingizio kuwa anatii.

Matthew Henry aliandika: “Mwanamke aliumbwa kutoka kwa ubafu wa Adamu. Hakuumbwa kutoka kwa kichwa chake ili amtawale, au kutoka kwa miguu yake ili akanyagigwe chini, lakini kutoka kwa ubafu wake ili awe kiwango kimoja naye, chini ya mabawa zake ilie akingwe, na karibu na moyo wake ili apendwe.” Wakristo wanastahili kuwa na utiifu kwa wao wenyewe kwa kumcha Kristo (Waefeso 5:21). Katika mkudhata huo kila kitu katika Waefeso 5:19-33 ni kwa mjibu wa kujazwa kwa Roho.

Wakristo waliojazwa kwa Roho wanastahili kuwa watu wa kuabudu (Waefeso 5:19), wenye shukrani (Waefeso 5:20) na watiifu (Waefeso 5:21). Paulo baadaye anayafuatisha mawazo yake kuwa katika kuisha maisha ya kujazwa kwa Roho yanawapasa mume na mke katika aya ya 22-23. Mke lazima amtii mume wake, sio kwa sababu hivyo ndivyo Mungu alipanga uhusiano wa ndoa uwe ukifanya kazi hivyo.

Utiifu sio mwanamke “kushinda kwa nyumba” kwa sababu ya mume wake. Ile hali kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu, mwanamke anamtii mume wake na mwanamume kwa juhudi zote anampenda mke wake
 
Pengine mimi nina mtazamo tofauti, kwakweli sioni sababu ya kugombana na mwanamke nilie kutana nae ukubwani tena akiwa tayari anafikra zake na tabia tofauti na mimi.
Nakumbuka zamaaaani mama yangu aliwahi kuniuliza kwamba kwanini naacha wanawake hata pengine hatuja gombana..... nilimjibu kwamba, hiyo ndio namna yangu ya kuepuka kugombana na mwanamke ambae sina uwezo wa kumbadilisha tabia.
 
Hii ndio inatakiwa, kama hamna maelewano bora kila mtu ashike 50 zake. Amani ya moyo ni muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi vitu viwili utii na kupendwa vinaendsna Kwa asilimia [emoji817]

Angalia huyu mke ambaye ni mpole anasikiliza Kila anachoambiwa na mume wake yaani hata ombi la mume wake kwake ni kama amri.

Huyu mke atapendwa mpaka atachanganyikiwa Kuna uchawi mkubwa kwenye utii.

Biblia yenyewe inasema “Ni Bora utii kuliko Sadaka”.

Mtu anayetoa Sana sadaka lakini hataki kutii Sheria ya kuacha dhambi ni Bora anayetoa sadaka kidogo na anatii Sheria ya Mungu Kila siku.

Mke anayetoa penzi lakini hataki kutii Bado hajakamilika.Utii ndyo Kila kitu.

Mwanamke ambaye anamtii mume wake huyo mwanaume anauwezo wa kumvumilia mengi.
 
[emoji817][emoji3581]
 
Back
Top Bottom