Vijana walelewe kwenye chipukizi huko na JKT kuna kazi kibao.Rais anateua kwa nafas yake, kulingana na changamoto za sehemu husika, ni jambo jema kuteua afisa wa jeshi, rais kama kiongoz anatakiwa aandae kizaz cha baadae kitakacho irithi inchi hii, na sio kweli vijana waililia hii nafas ila wana bidii ya kufikambali ktk nafas za uongozi mbalimbali inchini
Kwani kusema serikali itakua ya viwanda unataka wastaafu wakafanye kazi kule? Kilimo kwanza wastaafu wakazalishe sio?Du mkuu hoja yako sio rafiki sana na mazingira ya Tanzania kwani unemployment rate ipo juu na serikali ndio mmoja wa wadau wakuu wa ajira. Hao wastaafu walishafanya kazi na uwezo wao kiutendaji umepungua ndio maana wamestaaf.
Lakini pia kuna nguvu kazi kubwa imesomeshwa na serikali ipo mtaani otherwise ni upotevu wa fedha, hivyo Rais ateue yeyote walau wasizid umri wa miaka 55 wapewe nafasi.
Ombi kwa rais hizi nafasi ni nyeti kwa sababbu zinasimamia wataalamu na wanasiasa hivyo elimu na weledi uzingatiwe wakati wa uteuzi itasaidiia kuondoa mgongano na wadau kwenye wilaya ama tasisii husika.
Waliostaaf waende wapumzike wacheze na wajukuu, watoe ushauri kwa viongozi chipukizi, wajengeee uwezo vyama vyao, au hata kusoma zaidi.
Nawakilisha
Unajua jeshini wanastaafu kwa umri gani?Kwa nini wateuliwe wastaafu?? Hawa graduates wanaozurura na vyeti mitaani waende wapi?? Kama hili limewashinda then warudi kwenye mfumo wa zamani ambapo makatibu tarafa ndiyo walikuwa wanapandishwa vyeo na kuwa wakuu wa wilaya kwani tayari wanakuwa na uzoefu wa utawala.
Mkuu uko sahihi lakini mimi nazungumzia kwa sasa ambapo nafasi hizi hazikwepeki kwa mujibu wa katiba mbovu ya tuliyonayo.Kwa hiyo unataka cheo cha DC kiwe cha wastaafu?
Pole sana ndugu yangu.
Wakati watu wenye Akili na Hekima tunapendekeza hivyo vyeo VIFUTWE kabisa kwa sababu havina tija yoyote katika maendeleo yetu.
Embu fikiri kwanza, katika wilaya kuna Mkuu wa Polisi, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Wabunge nk. Kuna haja gani tena ya kuleta DC ambaye anaweza kuteuliwa Kiushabiki, Kiundugu, Kirafiki, Kimapenzi nk.
BORIS YETSINNadhani wewe utakuwa Afisa msatafu pole sana ,umekula kiinua mgongo chote kwakua unanyumba ndogo nyingi sana pole Mh Raisi,jenga kizazi ambacho kitakuwa kama cha Marehemu Melesi Zenawi,na comrade Hugo Chavez, na Yoris Bostin ili wafate misingi bora yako ndio jambo muhimu,samaki mkunje angali mdogo,nyinyi wazee hamkunjiki tena
Vijana wengi kwa nchi zilizoendelea hupelekwa jeshini, hawa wa kwetu waende site kule kulima pamba na tumbaku badala kukalia matamko ya ovyo ovyo na kujipendekeza.Wazo la hovyo kabisa hili, nasema hivi kwa sababu ukianza kufanya hivyo watendaji wa vyombo hivyo wataanza kujionyesha waziwazi kuwa wanatenda kwa lengo la kufulahisha chama kilichopo madarakani, lakini pia utapunguza ajira kwa vijana
Unajua jeshini wanastaafu kwa umri gani?