Uteuzi wa Wabunge 10: Jicho la kisheria

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
  • Nikiri kusoma na kufuatilia mjadala unaohusu Rais kuteua Wabunge sita wa kiume kati ya kumi anaopaswa kuwateua kwa mujibu wa katiba. Inasemwa kuwa Rais amevunja katiba kwa kuteua hivyo.Niseme mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni mtanzania wa kawaida, Msomi wa Sheria, ninayewiwa kuchangia mjadala huu. Nitachangia kisheria.
  • Nikiri pia kuwa Dr. Makongoro Mahanga, aliyekuwa Mbunge wa Ukonga na mwanachama wa CHADEMA, ndiye mwanzilishi wa mjadala huu. Mwanzoni, Dr. Mahanga aliuweka mjadala huu kama suala la kikatiba. Lakini leo, Dr. Mahanga ameliweka suala hili kama suala la kisiasa kwa 'kulipeleka' jambo hilo Bungeni.
  • Ni wazi kuwa Bunge linaanza vikao vyake huko Dodoma mnamo tarehe 31/1/2017. Tarehe hiyo inatazamiwa kuwa Wabunge wawili wateule: Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi na Abdallah Bulembo wataapishwa. Nianze sasa kuwasilisha mada yangu kwa kuweka wazi masuala ambayo tunakubaliana:
  • Tunakubaliana kuwa Rais ana mamlaka ya kuteua Wabunge 10 kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (iliyofanyiwa mabadiliko mara kwa mara). Nitaiita Katiba.
  • Tunakubaliana kuwa hadi sasa kwa mujibu wa Katiba, Rais tayari ameshateua Wabunge nane. Kati ya hao, Wabunge sita ni wanaume: Dr. Abdallah Posi, Dr. Phillip Mpango, Dr. Augustine Mahiga, Prof. Makame Mbarawa, Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi na Abdallah Bulembo. Katika nafasi kumi, zimebaki mbili.
  • Tunakubaliana kuwa hadi sasa Wabunge wanawake walioteuliwa na Rais ni wawili tu mmojawapo akiwa ni Dr. Tulia Ackson.
  • Tunakubaliana kuwa kimahesabu, hata kama nafasi mbili zilizobaki zitajazwa na wanawake, Wabunge wanawake wa kuteuliwa na Rais hawatafika watano.
  • Kama nilivyotangulia kusema, Katiba yetu imefanyiwa mabadiliko mbalimbali. Pia, katiba yetu ina matoleo mbalimbali. Mfano, kuna Toleo la 2000 na hata la 2005 (ya Kiswahili na Kiingereza)
  • Iliamriwa na kuamuliwa na Mahakama ya Rufani Tanzania, kwenye shauri la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Daud Pete, Rufaa ya Jinai Nambari 28/ 1990 kuwa Toleo rasmi la Katiba ni toleo la Kiswahili. Toleo la mwisho la Katiba kwa Kiswahili ni toleo la mwaka 2005 ambalo lina mabadiliko hadi yale ya 14 yaliyofanyika mwaka huo.
  • Mabadiliko ya 14 ya Katiba (kupitia Sheria Nambari 1/2005) ndiyo yaliyoingiza takwa la 'angalau' Wabunge watano wanawake kati ya Wabunge wanaoteliwa na Rais chini ya Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba. Kwa maana nyingine, maneno : 'angalau watano kati yao wawe wanawake' yaliingizwa kwenye Ibara tajwa kwa mabadiliko ya 14 ya Katiba niliyoyataja.
  • Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza iliyoandaliwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Toleo la Pili, 2014) neno 'angalau' linamaana ya 'at least'. Humaanisha, kiasi kisichopungua lakini kinachoweza kuzidi.
  • Ndiyo kusema, Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba kama ilivyo sasa (Toleo la 2005) inataka Wabunge wanawake wa kuteuliwa na Rais wasipungue watano ingawa waweza kuzidi. Hilo ni takwa la lazima la Katiba.
  • Kwa kilichotokea, yaweza kuwa ni makosa ya kisheria yanayorekebishika. Muda bado upo wa kurekebisha (kwakuwa kuapishwa kwa Wabunge wateule ni tarehe 31/1/2017 au baada ya hapo)
  • Kwakuwa Rais ana mamlaka ya kuteua, anayo mamlaka ya kutengua. Rais anaweza kutengua uteuzi wa Mbunge mmojawapo mteule ili kufanya idadi ya Wabunge wanaume aliowateua isizidi watano. Rais wetu ni msikivu, atafanya jambo.
 
...Ndiyo kusema, Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba kama ilivyo sasa (Toleo la 2005) inataka Wabunge wanawake wa kuteuliwa na Rais wasipungue watano ingawa waweza kuzidi. Hilo ni takwa la lazima la Katiba.
Mkuu Petro; kwenye mijadala humu humu JF kumekuwa na another "school of thought" kwamba kipengele hiko kitakuwa kimekiukwa endapo tu Rais atamaliza nafasi zake zote 10 za uteuzi bila "angalau" nafasi 5 kuteua wanawake. Lakini as long as bado hajamaliza zote, it is still safe kisheria. By the way halazimishwi na Katiba kuteua zote 10. Hili unalisemeaje Mkuu?
 
Zipo tetesi (tetesi lakini) kuwa yule waziri wa huko nje aliyeteuliwa ubunge na uwaziri wa huko nje anamwagwa!! Sasa sijajua ni lini! Na inasemekana pia hiyo nafasi ikachululiwa na mmoja wa hao wateule wa juzi!! Hata hivyo tayari rais kashavunja katiba na kikatiba, rais aliyevunja katiba huwa anaondolewa na bunge!! Je bunge letu litaweza kumuondosha rais Magufuli?
 
Hiki ni kipimo halisi. Tuone Katiba ya wananchi na Rais nani yupo juu.

Kwa hiyo Mkuu Petro Ni kwamba Mheshimiwa Rais amekiuka kiapo chake? Na kama itakuwa kweli adhabu yake ni nini?
 
Mkuu Petro; kwenye mijadala humu humu JF kumekuwa na another "school of thought" kwamba kipengele hiko kitakuwa kimekiukwa endapo tu Rais atamaliza nafasi zake zote 10 za uteuzi bila "angalau" nafasi 5 kuteua wanawake. Lakini as long as bado hajamaliza zote, it is still safe kisheria. By the way halazimishwi na Katiba kuteua zote 10. Hili unalisemeaje Mkuu?
Hiyo idadi na mgawanyo hujadilika pale ambapo nafasi zote zimeshajazwa. Lakini, kama wanaume au wanawake wameshazidi idadi yao, pia kuna mjadala kama huu wa sasa.
 
Hiyo idadi na mgawanyo hujadilika pale ambapo nafasi zote zimeshajazwa. Lakini, kama wanaume au wanawake wameshazidi idadi yao, pia kuna mjadala kama huu wa sasa.
Ningekuwa mimi ndio mwenye mamlaka na hayo yameshatokea ningekomea 9 na mchezo ungekuwa umeishia hapo. Kwa ufupi tukubali hiki kipengele (kama vilivyo vingine kadhaa) kina mapungufu makubwa. Waliokitunga au waandishi hawakuwa makini. Kama lengo lilikuwa kweli USAWA WA KIJINSIA kilitakiwa kisomeke "at least half" badala ya kutaja idadi. Hapa Rais angekuwa amebanwa na asingekuwa na justification yoyote.
 
Back
Top Bottom