Uteuzi wa Sioi batili - Wajumbe UVCCM Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa Sioi batili - Wajumbe UVCCM Arusha

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Feb 22, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  SIKU moja baada ya wanachama wa CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki kumpendekeza Sioi Sumari kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo ujao, baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani humo, wamepinga uteuzi huo wakidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mizengwe.

  Juzi, mkutano Mkuu wa Jimbo hilo ulimchagua Sioi, mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361 akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elishilia Kaaya (176), Elirehema Kaaya (205), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11).

  Lakini jana, baadhi ya wajumbe hao wa UVCCM wakiongozwa na Mjumbe wa Baraza la Umoja Mkoani wa Arusha, Kennedy Mpumilwa walidai kwamba uchaguzi huo ni batili kwa kuwa ulitawaliwa na misingi ya rushwa.

  Mpumilwa alidai kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa kila kona. Hata hivyo, hakuweka bayana kama walihongwa ili wamchague nani kati ya wagombea hao sita.

  Alidai kwamba kigogo mmoja wa UVCCM ngazi ya mkoa aliyeongozana na kada mmoja wa jumuiya hiyo, walikuwa ndani ya gari karibu na eneo la uchaguzi wakigawa rushwa kwa wajumbe.

  "Huu uchaguzi haufai kabisa baadhi ya wajumbe walihongwa. Ilikuwa ikitolewa 150,000 kwa kila mjumbe atakayekubali. Sasa hii CCM gani kama uteuzi tu hadi ufuate rushwa," alidai Mpumilwa.

  Alisema kwa jinsi mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika, ni dhahiri chama hicho kimeingia katika mpasuko mkubwa ambao kama usipoangaliwa kwa makini, unaweza kukiathiri.

  Mpumilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, alisema baadhi ya wanachama wa umoja huo wilayani humo wamechukizwa na mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi huo huku wengine wakitishia kuhamia upinzani wakati wowote.

  "Nakwambia vijana wamechukizwa kabisa na kilichofanyika katika mchakato wa uchaguzi, sasa wengine wametishia kwenda upinzani wakati wowote," alieleza Mpumilwa.

  Aliutaka uongozi wa CCM taifa kuingilia kati suala hilo na kulipa uzito akidai kwamba lisipoangaliwa huenda likazua mpasuko mkubwa ndani ya CCM wilayani humo na kusababisha kulipoteza jimbo hilo wakati wa uchaguzi.

  Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi ya wa CCM Mkoa wa Arusha, Loota Sanare alisema hadi jana hakuna mgombea yoyote kati ya hao sita ambaye alikuwa amepinga matokeo ya uchaguzi huo.

  Alisema ushindi wa Sumari katika uchaguzi wa ngazi ya jimbo, siyo mwisho wa uteuzi na kwamba kuna vikao vya kamati ya siasa ya Wilaya ya Arumeru na baadaye vikao vya mkoa na Kamati Kuu (CC) ya CCM Taifa, ambayo ndiyo itakayomtangaza mgombea.
  "Tumezipokea hisia za wana-CCM, Sioi ameongoza ni nafasi nzuri kwake lakini siyo mwisho wa uteuzi wake. Bado kuna mchakato mrefu mbele yake," alisema Sanare.


  Vigogo watimua mbio

  Katika hatua nyingine, kushindwa kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) wa Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya katika kura hizo za maoni juzi, kuliibua huzuni kubwa kwa vigogo wa chama hicho huku baadhi yao wakiondoka ukumbini kabla ya matokeo.

  Kaaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), alikuwa anaungwa mkono na kundi la viongozi wa juu wa CCM na Serikali ambao wamejipambanua kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Mjumbe huyo wa Nec alishika nafasi ya nne baada ya kupata kura 176, nyuma ya Sumari, Sarakikya na Elirehema Kaaya.

  Dalili za kubwagwa kwa kigogo huyo, zilianza kuonekana mapema nje ya ukumbi ambako baadhi ya madiwani na wana-CCM vijana, walikuwa wakiendesha kampeni nzito ya kutaka mgombea kijana ambaye ataweza kupambana na mgombea machachari wa Chadema, Joshua Nasari endapo atapitishwa na chama chake.

  Pia, katika ukumbi wa kupigia kura, mara baada ya wagombea wote sita kujieleza, Sumari alikuwa akishangiliwa zaidi na kundi la vijana hali ambayo iliwasukuma baadhi ya vigogo kuanza kuondoka mapema ukumbini.

  Gazeti la Mwananchi.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Acha wafarakane!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  pamoja na vuguvugu lote hili la kuelimishana juu ya kupiga vita kununuliwa bado kuna watu wanauza?

  sasa kuna tofauti gani kati ya wanaouza kura na wanaouza pale ohio?
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Watamalizana wenyewe kwa wenyewe
   
 5. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbaya sana hii
   
 6. j

  janejean Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli ubunge ni deal. Huyo mtoto wa sumari anatafuta nini tena huko? Badala ya kulia kifo cha baba yake. Au na yeye ndio vile.........?
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Mpumilwa?..... atawaambia nini kina Akyoo, Sarakikya, Kitomari,Nko.... et al.?
  Wameru wapo very sensitive na kabila na ardhi yao, hawa kina Mpumilwa, Chacha sijui Mwita, Masanja... I don't know.
  They should just step aside for a min.
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sisiem safiiiiiiiii!!!

  Hili litakuwa fundisho.
   
 9. Simon Lupondo

  Simon Lupondo Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana CCM manake wanazidi kujichimbia kaburi ubunge wa Arumeru, na waendelee kufarakana ili CHADEMA tupate nafasi zaidi, Kaaya wote watapigia Nassari
   
 10. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndoto za alinacha
   
 11. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  alinacha ni kiongozi gani wa magambaz
   
 12. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Ni fundisho na wao kuwa na mpasuko ni mtaji kwa wengine
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini CCM hawajifunzi kutokana na kura za maoni zilizo acha makundi ndani na nje ya CCM, baada ya chama hicho kulazimisha wagombea ambao sio chaguo la wananchi

  Leo hii tena wamerudia kosa lilelile kwa kulazimisha mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.kwa upande wangu na nadhani bado CCM haija pata somo
   
 14. data

  data JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,743
  Likes Received: 6,514
  Trophy Points: 280
  Hainihusu...
   
 15. M

  Mkolakumwezi Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni faida kwetu CDM wacha waendelee kuraruana sisi tunasonga mbele zaidi
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo mchizi akatizi popote. Nguvu ya umma itamshangaza!
   
 17. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Dont interrupt you enemy when he is making mistakes.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Watu wenye mawazo ya hovyo hovyo, hasa ya ukabila wanazidi kuongezeka kila kukicha.

  Sasa wewe una tofauti gani na Kaburu wa afrika ya kusini!? shame on you dude!!!
   
 19. blea

  blea JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ndugu wakigombana chukua jembe kalime wakipatana we kavune ,,, mnnnnn GOOD
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kama zilivo ndoto za rais wako kuifanya Kigoma kuwa Dubai..hahaaaaa...
   
Loading...