Uteuzi wa Raia wa Uganda kuongoza NSSF: Ombeni Sefue, Eric Shitindi & Jenista Mhagama wajiuzulu

AbasMzeEgyptian

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
407
312
28538c6b-335c-4a34-a732-0e9f74e8d244.jpg

Mheshimiwa Rais,

Naomba urejee taarifa kwenye vyombo vya habari, SIKU TANO ZILIZOPITA.

Waziri wako wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama alikutana na baraza la uwezeshaji wananchi wa Tanzania kiuchumi (NEEC) ambalo majukumu yake ni kuwawezesha wa Tanzania kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira Tanzania. Na Akasisitiza na kutoa amri kuwa serikali ya awamu ya tano inapenda kuona kazi inafanyika kwa vitendo na matokeo yananufaisha wananchi na si vinginevyo.....

Hii vinginevyo aliyosema waziri Mhagama alikuwa akimaanisha kuwawezesha Raia/ Wananchi wa UGANDA (Jana alimteua Raia wa Uganda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF).

Naamini kuwa Waziri Mhagama kafanya maamuzi hayo baada ya kupata ruhusa toka kwa katibu mkuu kiongozi Ikulu, Ombeni Sefue ambaye amekuwa akituhumiwa kuwa anakubambikia majina ya watu ambao hawakidhi viwango vyako kama Eric Shitindi na Jenista Mhagama.

Pia tusisahau kuwa Katibu mkuu wizara ya kazi na ajira, Eric Shitindi ndiye aliyempigia chapuo huyu Mganda kupata kazi SSRA.

Kutokana na unyeti wa nafasi hii ya mkurugenzi mkuu NSSF, naamini kuwa OMBENI SEFUE, ERIC SHITINDI & JENISTA MHAGAMA hawana nia njema na Kipenzi chetu, Rais John Pombe Magufuli,PHD.

Ombi kwa Mheshimiwa Rais, wawajibishe hawa watu na wengine wote waliohusika kukuhujumu, kuhujumu nchi hii.

Mheshimiwa Rais tunakuomba uombe ma faili ya hawa watu watatu niliowataja (ERIC SHITINDI, OMBENI SEFUE & JENISTA MHAGAMA)

Ikumbukwe kuwa ulipoanza awamu yako ulikuwa hujagusa maslahi yao lakini leo ulipoanza kugusa maslahi yao wameamua kwenda kinyume na misimamo yako ya kuweka watanzania mbele.

Na kukumbusha tuu Mheshimiwa Rais, huyu waziri JENISTA MHAGAMA ulibambikiwa na haendani na viwango vyako kwa maana teuzi zako zilikuwa zimejaa watu wasomi waliobobea. Iweje leo umeenda kumteua JENISTA MHAGAMA kusimamia Wizara nyeti hii amabayo anapanga sera, mambo mambo ya bunge, kazi na ajira wakati hata degree moja hana.

Mheshimiwa Rais, ukitaka Ushaidi katika hili tafadhali mheshimiwa Rais wasiliana Katibu wa Bunge Ndugu Kashilila akupe mafaili na vyeti vyake vya elimu.
balozi%2Bombeni%2Bsefue.jpg

Ndugu wa Tanzania.

Kufuatia Waziri Jenista Mhagama kumteua raia wa Uganda kuwa Mkurugenzi mkuu wa NSSF pasipo kufuata sheria za kazi,uhamiaji, usalama na kadhalika, kambi ya GANG OF 5 inazidi kuparaganyika na sasa wameanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe kuwa walichemsha wapi na kwa nini siri zao zinazidi kumwagwa kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa za hivi jioni ni kuwa mmoja wao ameamua kujiondoa kwenye hii conspiracy kwani anaamini maamuzi ya haraka yaliyofanywa jana na Waziri wa Kazi Jenista Mhagama ya kumpa Ukurugenzi raia wa UGANDA hayakuzingatia matters of national interest and security.

Lakini siri zinazidi kuvuja kuwa Katibu Mkuu kiongozi bwana Ombeni Sefue na Katibu Mkuu wizara ya Kazi na Ajira kwa kusudi waliamua kuvunja bodi ya NSSF kinyemela ili kuharakisha zoezi la kumwajiri huyu raia wa Uganda.

Katika mazingira ya kawaida bodi ya NSSF ambayo ina wawakilishi wa wafanyakazi, serikali,sekta binafsi na waajiri. Hakuna mTanzania ambaye anaamini kuwa bodi ingekubali uteuzi huu wa raia wa Kigeni kuongoza shirika la umma kubwa kama NSSF.

Tusisahau kuwa Bodi ina Mwenyekiti ambaye ni Mteule Wa Rais, sasa nani kampa madaraka Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue kutemtengua Mteule wa Rais? Kwa nini Ombeni Sefue, Eric Shitindi na Waziri wa Ajira Jenista Mhagama walikataa kuwapatia wanachama wa NSSF wapewe maelezo kwa nini bodi yao imevunjwa na Ombeni Sefue kinyemela?

Huyu huyu Sefue ndiye aliuvurunda MSD.
 
Kulikuwa na haraka gani ya kumteua na kumtangaza huyo Mganda bila kujiridhisha! hizi nafasi kubwa za Ukurugenzi wa mashirika ya Uma ziwe zinatangazwa wazi watanzania washindanishwe apatikane mtu kwa elimu na uwezo wake badala ya kupewa kama shukrani.
 
huyo aliyeteuliwa vipi ni member wa mfuko wenyewe au ni member wa pspf hapohapo ni kiongozi wa NSSF
 
JPM timu yako imekuangusha...
Nilishawahi kuona kwenye taarifa ya habari siku 1 kuna dada 1 nae ni raia wa hizi nchi za jirani akawa amefanikiwa kushika nafasi moja tena senior level katika wizara zetu.
Huyu wa NSSF Uraia wake uchunguzwe kwa maslahi ya taifa tuweke tofauti za vyama na udini pembeni.kuna watanzania wazalendo wengi tu wana sifa ya kuongoza.
 
Hili ni jipu kuu kati ya yote....anataka aseme hakuna watanzania wenye uwezo wa kushika hii nafasi,
Je huko Uganda Watanzania wanawezeshwa?
 
Nashangaa mnaoshobokea sirikali ya CHICHIEM kwamba inafanya vizuri, ikumbukwe kuwa sera zote imekopi kutoka upinzani.
 
28538c6b-335c-4a34-a732-0e9f74e8d244.jpg

Mheshimiwa Rais,

Naomba urejee taarifa kwenye vyombo vya habari, SIKU TANO ZILIZOPITA.

Waziri wako wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama alikutana na baraza la uwezeshaji wananchi wa Tanzania kiuchumi (NEEC) ambalo majukumu yake ni kuwawezesha wa Tanzania kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira Tanzania. Na Akasisitiza na kutoa amri kuwa serikali ya awamu ya tano inapenda kuona kazi inafanyika kwa vitendo na matokeo yananufaisha wananchi na si vinginevyo.....

Hii vinginevyo aliyosema waziri Mhagama alikuwa akimaanisha kuwawezesha Raia/ Wananchi wa UGANDA (Jana alimteua Raia wa Uganda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF).

Naamini kuwa Waziri Mhagama kafanya maamuzi hayo baada ya kupata ruhusa toka kwa katibu mkuu kiongozi Ikulu, Ombeni Sefue ambaye amekuwa akituhumiwa kuwa anakubambikia majina ya watu ambao hawakidhi viwango vyako kama Eric Shitindi na Jenista Mhagama.

Pia tusisahau kuwa Katibu mkuu wizara ya kazi na ajira, Eric Shitindi ndiye aliyempigia chapuo huyu Mganda kupata kazi SSRA.

Kutokana na unyeti wa nafasi hii ya mkurugenzi mkuu NSSF, naamini kuwa OMBENI SEFUE, ERIC SHITINDI & JENISTA MHAGAMA hawana nia njema na Kipenzi chetu, Rais John Pombe Magufuli,PHD.

Ombi kwa Mheshimiwa Rais, wawajibishe hawa watu na wengine wote waliohusika kukuhujumu, kuhujumu nchi hii.

Mheshimiwa Rais tunakuomba uombe ma faili ya hawa watu watatu niliowataja (ERIC SHITINDI, OMBENI SEFUE & JENISTA MHAGAMA)

Ikumbukwe kuwa ulipoanza awamu yako ulikuwa hujagusa maslahi yao lakini leo ulipoanza kugusa maslahi yao wameamua kwenda kinyume na misimamo yako ya kuweka watanzania mbele.

Na kukumbusha tuu Mheshimiwa Rais, huyu waziri JENISTA MHAGAMA ulibambikiwa na haendani na viwango vyako kwa maana teuzi zako zilikuwa zimejaa watu wasomi waliobobea. Iweje leo umeenda kumteua JENISTA MHAGAMA kusimamia Wizara nyeti hii amabayo anapanga sera, mambo mambo ya bunge, kazi na ajira wakati hata degree moja hana.

Mheshimiwa Rais, ukitaka Ushaidi katika hili tafadhali mheshimiwa Rais wasiliana Katibu wa Bunge Ndugu Kashilila akupe mafaili na vyeti vyake vya elimu.
Jipime kwanza kwa ulichoandika...only one word litafanya post yako yote ionekane kinyaaa...anywei Hakuna aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF....huaminiki ww
 
Back
Top Bottom