Uteuzi wa Dr. Ndalichako unahusiana na JamiiForums...

Bugududu Sududu

JF-Expert Member
Apr 19, 2014
594
691
Habari zenu wakuu, miongoni mwa wizara zilizo kuwa zimeachwa kiporo uteuzi wa Waziri wake ni wizara ya elimu, kabla ya uteuzi uliofanyika jana kuna uzi ulipatikana humu ikidai wizara ya elimu apewe aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la mitihani (necta) Dr. Joyce Ndalichako, jana tumeshuhudia wenyewe mambo yamefanyika kama ilivyo ombwe.

Je, JamiiForums kuna makachero? Kama sivyo basi Nimeamini kweli JamiiForums "The home of great thinkers "
 
JF ina influence kubwa
CHADEMA ilipata nguvu hapa JF kabla ya kupata nguvu uraiani

Mawaziri watatu now wapo humu
kiongozi wa upinzani bungeni
mwenyekiti wa PAC na kadhalika
 
JF ni mtandao wa kijamii. Yapo mawazo mazuri yanatolewa kupitia humu. Kumbuka JF ni forum ya watu wasio na pa kusemea. Kama tulivyong'ang'ana humu ili Magufuli awe Rais, ndivyo inavyotokea kwa baadhi ya ishu
 
Jamii forum ni uwanja wetu waTanzania wa kusema na kujadiliana...wapo wakuu wengi Sana humu so ya Ndalichako ni mojawapo tu ya impact ya JF Kuna mengine mengi. Viva JF
 
JF ni tofauti sana na social network zingine za kipuuzi hapa ni 'the home of great thinkers' ila wengine daaah eeeeh
 
Viongozi wa nchi hupitia JF; sio ya Ndalichako tu hata ya yule Msemo wa Oceon Road cancer Hospital yaliandikwa humu humu !!
 
Jamii forum ni uwanja wetu waTanzania wa kusema na kujadiliana...wapo wakuu wengi Sana humu so ya Ndalichako ni mojawapo tu ya impact ya JF Kuna mengine mengi. Viva JF

Viva forever!
 
Kuna haja ya kuirudisha jf kwenye hadhi yake ikiwa hata rais anaweza kuchukua mawazo ya wadau humu.

Jambilo mkuu uko sahihi. Kama serikali inapita humu na members 3 ni ministers ina maana jf is now part and parcel of tanzanian society. Tunachotakiwa kufanya ni kutoa michango yenye viwango.
 
JF ni chanzo bora kabisa cha habari zinazosomwa na watu wengi.

Pia viongozi wengi tuko nao humu.


Ushauri wetu mwingi wanaufuata.
 
Back
Top Bottom