KWA KIPIMO CHA BUSARA ZA MZEE WARIOBA HAWA UVCCM KUPIGA VITA SAUTI HURU
NDANI CCM NA LIAZIMA UFISADI UHAI MWINGINE TENA NDIO TUSEME
WANAFIKIRI KAMA WAZEE ZAIDI AUI VIJANA KWA USAHIHI WAKE???
Usemi moja wa Ki-China hutuambia kwamba hata safari ya umbali wa kilometa 6,000 sharti uanze na guu la kwanza. Sasa mpaka hivi sasa tunatakiwa kuuliza kama guu la kwanza la UVCCM limeelekezwa kuleta uhai mpya kwa chama chao au kukiua kabisa??
Tunajiuliza hili kwa sababu hapo baadaye kidogo tungependa tuwe na CCM kama chama cha upinzani IMARA zaidi ya jinsi ndugu yake KANU kilivyo kule nchi jirani Kenya. Maendeleo ya nchi huwa yanapata msukumo bora zaidi ndani ya nchi ple kukiwepo chama imara cha upinzani hivyo binafsi nisingependa kuwa na idadi ya wabunge kama TLP NCCR-Mageuzi hivi sasa bungeni.
Hata hivyo uamuzi na chaguo la ama kufanyia palizi zaidi na kunyunyizia maji na mbolea safi au kuung'oa kabisa UFISADI na mizizi yake yote ndani ya chama chao yote ni haki yao. Lakini tusisahau kwamba kila watakalolitenda litakua na faida au gharama kubwa kubwa sana kwao na kusaidia kuchonga sura halisi ya hatima yao.
Kwa mfano kampeni za kung'oa sauti pinzani ndani ya CCM ni udhaifu wa mwaka kudiriki kufanya na kizazi cha Doti Kom ambao wanapashwa kuelewa fika kwamba katika ulimwengu wa sasa KILA KITU HUENDESHWA KIUSHINDANI IKIWAMO SIASA na kwamba ukibahatika kumpata wa kukukosoa kama Samuel Sitta, Mwakyembe na wengine wengi tu basi unapashwa ujihesabu ni mwenye bahati kubwa kuwa nanafasi zuri zaidi kuboresha uongozi wako kwa kutumia ukosoaji wao ule wa kujenga.
Lakini kwa kuwa kumbe lenu ni kuwaangusha akina Sitta, Magufuli, Mwakyembe, Anna Kilango na wengine wengi tu na basi ujue wenzio majiranni kina TLP wanajiuliza utamaliza lini kukata tawi tegemeo la mti ulilolikalia??
Mbali na vitabu vya dini kutufundisha kwamba mwanamke mpumbavu huharibu nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, usemi ambalo UVCCM hawatokua mbali sana nalo hivi sasa, kinachonitia hofu zaidi kwa vijana wenzetu hawa ni kule kujidhihirisha ndani ya busara za Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba kwamba pindi utembeleapo kijiji fulani na ukakuta vijana mawazo yao hayana tofauti na mawazo ya wazee kijijini hapo basi moja kwa moja ujue kuna tatizo kubwa sana limejificha mahala.
Je, katika hiki kijiji cha CCM wadau mnawatazama vipi hawa UVCCM na kule kupinga kwao sauti huru ndani ya chama chao??????????