Uteuzi wa Bashe kuongoza kamati Maalum ya CCM ni Ushindi Mkubwa wa Mafisad ,Washerekea usiku kucha

Haya sasa oneni wenyewe, utaahira wa viongozi wa Chama Cha Majambazi, tukisema sisi oh wanataka kupindua nchi. Hivi kweli kuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye si mnufaika wa ufisadi unaofanywa na hawa mafia ambaye anaiunga mkono CCM? Walala hoi mnaoiunga mkono CCM wahini Loliondo mnaumwa kweli.
 
Kila aliyetolewa kwa mizengwe au kwa manufaa fulani, mkwere atamzawadia/anamzawadia ulaji mwingine ili chama chake ''kiendelee kuwa na umoja''. Nape, vuai, Bilal, Bashe, na wengine wanafuata

maana yake ni kwamba ....Ridhiwani in hardship? CCM nawafananisha na Marekani hawana rafiki/adui wa kudumu...hawa jamaa ni zaidi ya kinyonga
 
quote_icon.png
Originally Posted by Pdidy
SIMJUI MMILIKI WA DOWANS, SIJUI KWA NINI TANZANIA NI MASKINI. BY JAKAYA KIKWETE.

mi sijiui kwanini ni mtanzania@@@



'' The most important human endeavour is the striving for morality in our actions. Our balance and even our existence depend on it. Only morality in our actions can give beauty and dignity to life'' Dr. Martin Luther King (Jr)
 
Wanajua wanalofanya, maana wakati mwingine hata kama humtaki mbwa lakini kumfungia bandani ni muhimu ili uwe na uhakika kuwa hawezi kuuma watu huko nje.

Hata Maalimu kule Zenj kafungiwa bandani, ndio maana Shein hawezi kuja kwenye vikao vya Serikali huku bara, hasije akashika mafaili na kufanya kazi wakati ni mfungwa.
 
huyu safari yake ni fupi, 2015 CDM inashika nchi Rostam na wafuasi wake wote wataswekwa ndani tuone atakimbilia wapi huyo.
 
vibaraka wa EL na RA wanazidi tumiwa kila kona.kuna wanao pewa nafasi mbalimbali za uongozi ili walinde maslahi yao na wengine wanawatetea kwenye mitandao kama hii.
nina imani na watanzania kuwa wamekomboka akili kujua nyeupe na nyeusi.
 
Sisiem siku zote wapo substandard! Wanabadilika kama vinyonga kulingana na mahitaji ya kimazingira.

Mbona wameshindwa kubadilika kwa kile tunachokiitaji?? hawana jipya.... mimi hata Dr. Slaa akiamia huko... langu moja tuuuuuu SIHIITAJI CCM TENAA period
 
SIMJUI MMILIKI WA DOWANS, SIJUI KWA NINI TANZANIA NI MASKINI. BY JAKAYA KIKWETE.

mi sijiui kwanini ni mtanzania@@@

.
Hayo yote ya kina Jk, Makamba, Rz1, Mkuchika,RA na wengineo kufuta kauli zao tatanishi dhidi ya Bashe hayajafanyika. Ila kulingana na mila na desturi za ccm za kuienzi rushwa kama tuzo iliyotukuka ndani ya chama, juzi ktk mkutano wa uvccm zilitembea bahasha za rushwa ya sh. 50.000/= kwa kila mjumbe. Na inasemekana ndani ya kikao kulikua na wajumbe 107 akiwemo Bashe. Inasadikika kuwa rushwa hii waliopewa uvccm ni kwa heshima ya Bashe kwamba amerudishwa kundini kwa sherehe ya kukabidhiwa charter ya chama, yaani bahasha ya khakhi. Hivyo baada ya sherehe hiyo maalum kwa ajili yake, Bashe amesahau ya nyuma na yupo tayari kutumiwa na kundi lolote lenye kisu kikali(chapaa) chamani.
Ni hivyo tu, unakuwa kama huifahamu sisiem banaa??
.
 
Duhu!! Ndio kamati ya Bashe imeanza na Sita? by 2015 tutaona Mengi, Mungu niepushe na hiki chama cha Mafisadi,CDM Tumewasoma na tunasonga mbele na operation sangara Mbeya ,Rukwa, Ruvuma ,Sumbawanga mjitayarishe tunakuja kuwashi..iii...kaaaaa!! This time lazima tumngoe mbayuwayu na pinda anayetushutumu sisi CDM ni wadini wakati yeye ziara yake ya Mkoa wa Kagera alitumia muda mwingi kuongea na maaskofu zaidi ya kujishughulisha na shughuli za kiserikali
 
Tanzania bila CCM inawezekana...hebu vijana wazamani na ninyi wa sasa tujipange 2015 waondoke hawa!!
 
Kamati Maalum inafanya kazi gani mpaka mafisadi wanasherehekea? Sisi tunajua Jembe na Nyundo tu si hizi Kamati wataziunda, na kuzibadilisha kila kukicha ila wakae wakijua Chama ni cha Jembe na Nyundo tu.
 
Kulikuwa na mtawala kule Uganda,Dk milton obote,aliponzwa na kaka yake R.aziz na kilichompata ni historia mpaka leo.na ktk mazishi yake familia ya RÄ hata sina kumbukumbu kama walituma rambirambi.
 
KWA KIPIMO CHA BUSARA ZA MZEE WARIOBA HAWA UVCCM KUPIGA VITA SAUTI HURU
NDANI CCM NA LIAZIMA UFISADI UHAI MWINGINE TENA NDIO TUSEME
WANAFIKIRI KAMA WAZEE ZAIDI AUI VIJANA KWA USAHIHI WAKE???


Usemi moja wa Ki-China hutuambia kwamba hata safari ya umbali wa kilometa 6,000 sharti uanze na guu la kwanza. Sasa mpaka hivi sasa tunatakiwa kuuliza kama guu la kwanza la UVCCM limeelekezwa kuleta uhai mpya kwa chama chao au kukiua kabisa??

Tunajiuliza hili kwa sababu hapo baadaye kidogo tungependa tuwe na CCM kama chama cha upinzani IMARA zaidi ya jinsi ndugu yake KANU kilivyo kule nchi jirani Kenya. Maendeleo ya nchi huwa yanapata msukumo bora zaidi ndani ya nchi ple kukiwepo chama imara cha upinzani hivyo binafsi nisingependa kuwa na idadi ya wabunge kama TLP NCCR-Mageuzi hivi sasa bungeni.

Hata hivyo uamuzi na chaguo la ama kufanyia palizi zaidi na kunyunyizia maji na mbolea safi au kuung'oa kabisa UFISADI na mizizi yake yote ndani ya chama chao yote ni haki yao. Lakini tusisahau kwamba kila watakalolitenda litakua na faida au gharama kubwa kubwa sana kwao na kusaidia kuchonga sura halisi ya hatima yao.

Kwa mfano kampeni za kung'oa sauti pinzani ndani ya CCM ni udhaifu wa mwaka kudiriki kufanya na kizazi cha Doti Kom ambao wanapashwa kuelewa fika kwamba katika ulimwengu wa sasa KILA KITU HUENDESHWA KIUSHINDANI IKIWAMO SIASA na kwamba ukibahatika kumpata wa kukukosoa kama Samuel Sitta, Mwakyembe na wengine wengi tu basi unapashwa ujihesabu ni mwenye bahati kubwa kuwa nanafasi zuri zaidi kuboresha uongozi wako kwa kutumia ukosoaji wao ule wa kujenga.

Lakini kwa kuwa kumbe lenu ni kuwaangusha akina Sitta, Magufuli, Mwakyembe, Anna Kilango na wengine wengi tu na basi ujue wenzio majiranni kina TLP wanajiuliza utamaliza lini kukata tawi tegemeo la mti ulilolikalia??

Mbali na vitabu vya dini kutufundisha kwamba mwanamke mpumbavu huharibu nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, usemi ambalo UVCCM hawatokua mbali sana nalo hivi sasa, kinachonitia hofu zaidi kwa vijana wenzetu hawa ni kule kujidhihirisha ndani ya busara za Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba kwamba pindi utembeleapo kijiji fulani na ukakuta vijana mawazo yao hayana tofauti na mawazo ya wazee kijijini hapo basi moja kwa moja ujue kuna tatizo kubwa sana limejificha mahala.

Je, katika hiki kijiji cha CCM wadau mnawatazama vipi hawa UVCCM na kule kupinga kwao sauti huru ndani ya chama chao??????????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom