Uteuzi wa Arther Mwambene kuwa mkurugenzi wa MAELEZO

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
BAADHI ya watu watakuwa wamepongeza uteuzi wa Arther Mwambene, kuwa mkurugenzi wa MAELEZO kwa kuzingatia kuwa ni kijana na labda ataleta mabadiliko fulani kwenye tasnia ya habari.

Lakini nataka nitoe angalizo dogo - uteuzi wa Mwambene unatokana na kikao ambacho Benard Membe alikifanya na Rais Kikwete cha kulifungia MwanaHalisi.

Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe. Infact, pale wizarani watu wakiwa wanamsema vibaya Membe halafu ghafla Mwambene akitokea, wote wananyamaza kimya! Uteuzi wake ni sehemu ya majadiliano aliyofanya Membe siku ile anajadiliana na JK kuhusu MwanaHalisi. Hii sehemu ya strategies zake kuelekea 2015. Kwa sisi tunaojua nini kinaendelea kwenye teuzi hizi, tunasema ngoja tusubiri tuone.....
 
Kafiribangi,
Ungeongezea kidogo mnofu kwenye mfupa. Umetupa hamu ya kutaka kujua zaidi.
 
BAADHI ya watu watakuwa wamepongeza uteuzi wa Arther Mwambene, kuwa mkurugenzi wa MAELEZO kwa kuzingatia kuwa ni kijana na labda ataleta mabadiliko fulani kwenye tasnia ya habari.

Lakini nataka nitoe angalizo dogo - uteuzi wa Mwambene unatokana na kikao ambacho Benard Membe alikifanya na Rais Kikwete cha kulifungia MwanaHalisi.

Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe. Infact, pale wizarani watu wakiwa wanamsema vibaya Membe halafu ghafla Mwambene akitokea, wote wananyamaza kimya! Uteuzi wake ni sehemu ya majadiliano aliyofanya Membe siku ile anajadiliana na JK kuhusu MwanaHalisi. Hii sehemu ya strategies zake kuelekea 2015. Kwa sisi tunaojua nini kinaendelea kwenye teuzi hizi, tunasema ngoja tusubiri tuone.....

Sasa kama ninyi mnaojua nini kinaendelea mkisubiri na kuona, sisi tusiojua ndio tufanyeje sasa?
 
Wala sina shaka naye na ninamfahamu vizuri kibnafsi na hata kiutendaji.Huyo bwana Okololo aliyekuwepo kama mkurugenzi habari maelezo ndiye aliyekuwa mtu wa kutukuza mfumo na hata kudiriki kusema anapokuwa anahutubia rais au akiwa uwanja wa maonyesho kama uwanja wa bibi basi wakazi wote wa dsm, twende tukamsikilize.Tafakari
 
''Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe''

Kuwa karibu na waziri ndo mwake, atakuwaje mbali na mwenye wizara? . Uzuri mmoja jamaa ni kijana na yuko vizuri sana kichwani. Tumtakie kila la heri katika kazi yake mpya
 
Siyo kila kitu au uteuzi ni lawama. apewe nafasi na akishindwa basi tufanye judgement, hata hajaanza kazi tayari tunalaumu. Lipi au nani mwema kwetu watanzania? mlitaka nwambene asimsikilize Membe wakati yeye ndiye bosi wake? mabosi wenu wamekosea mara ngapi na mko kimya ili kuwalinda? mbona sisi hatusemi?
 
Hahahaaa, niliwaza sana inakuaje yule dakitari wetu asiikomentie hii issue??
 
Back
Top Bottom