Uteuzi mpya CCM wavuruga wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi mpya CCM wavuruga wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 12, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Uteuzi mpya CCM wavuruga wabunge

  Mwandishi Wetu Machi 11, 2009
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


  BAADHI ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wana matumbo joto kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na chama chao katika utaratibu wa kuteua wagombea yanayoweza kuwatupa nje kwa kushindwa kutetea nafasi zao.

  Miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na baadhi ya mawaziri ambao sasa wanayaona mabadiliko hayo kuwa yanayowachonganisha na wapiga kura wao kwa kuwa wengi wao hawakuwahi kurejea majimboni kushukuru kwa kuchaguliwa.

  Mabadiliko hayo yamefuta utaratibu wa zamani wa upigaji kura za maoni katika kuwapata wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani. Utaratibu wa zamani uliwapa fursa hiyo wanachama wachache, tofauti na sasa ambapo wagombea watapigiwa kura na wanachama wote, kuanzia ngazi ya tawi.

  Katika kufanikisha utaratibu huo, wagombea wote wa nafasi husika watafanya ziara ya pamoja na kutumia usafiri ulioandaliwa kwa gharama za chama hicho, lengo likiwa ni kuhakikisha kila mgombea anapata haki sawa.

  Taarifa za kichunguzi zinasema baadhi ya wabunge, licha ya kutimiza takriban miaka mitatu ya ubunge katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Nne, hawajahi kutembelea maeneo yote ya majimbo yao na hata katika maeneo waliyokuwa wakitembelea wamekuwa na uhusiano wa karibu zaidi na viongozi wa chama hicho kuliko wanachama wa kawaida.

  Kwa sasa CCM ina wabunge wa majimbo 205, lakini taarifa kutoka katika majimbo hayo, zikiwanukuu baadhi ya viongozi wa chama hicho na baadhi ya wananchama, zinaonyesha kuwa hali ni mbaya kwa baadhi ya wabunge wa sasa.

  Kwa upande mwingine taarifa hizo zinabainisha kuwa utaratibu huo mpya wa kura za maoni utawasaidia mno baadhi ya wabunge, hususan katika majimbo ambayo viongozi wa chama ngazi ya wilaya (jimbo) walikuwa wakiwapiga vita lakini idadi kubwa ya wanachama wa kawaida wameonyesha mapenzi yao kwao.

  Inaelezwa kuwa karibu katika kila mkoa wa Tanzania Bara, baadhi ya wabunge wa CCM wataumizwa na utaratibu huo mpya.

  Mwezi uliopita, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aliwaonya wabunge kuwa wanarejea majimboni kwao pengine kutokana na kubaini kuwa baadhi yao waliyatupa majimbo yao baada ya kura za nwaka 2005.

  Kikwete alitoa onyo hilo wakati anahutubia katika maadhimisho ya miaka 32 ya CCM katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

  “Ingawa imebaki miaka miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu, ni wakati sasa kwa wabunge ambao wametelekeza majimbo yao kuwatembelea wananchi, kabla wananchi hao hawajaamua kutowapigia kura,” alisema Kikwete na kuongeza:

  “Kutembelea jimbo ni jambo muhimu katika kujihakikishia kuwa wewe mbunge unaendelea kubaki madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao.”

  Inadaiwa kuwa wabunge wengi wamekuwa hawafiki majimboni wakitoa sababu ya kubanwa na shughuli za Kamati za Kudumu za Bunge.

  Lakini hata kwa sababu hiyo Rais Kikwete alisema: “Kutumia sababu kuwa umebanwa na shughuli za kamati hakuwezi kukusaidia katika Uchaguzi Mkuu ujao.”

  Lakini wakati baadhi ya wabunge wakiwa wamebanwa na utaratibu mpya tofauti na ule wa zamani ambao mbinu kubwa ya ushindi ilikuwa ni kuwa karibu (hata kwa kusaidia shida binafsi) na viongozi na wajumbe wa mkutano husika katika kupiga kura za maoni kumpendekeza mgombea, utaratibu huu mpya pia unatarajiwa kuingiza wanachama wengi katika CCM, hususan wakati wa kusaka wagombea.

  Inaelezwa kuwa kutokana na utaratibu huu kutoa nafasi kwa wanachama kupiga kura za kupendekeza mgombea, baadhi ya wagombea wapya au wa zamani watalazimika kuingiza wanachama wapya kwa wingi kwa lengo la kujiongezea idadi ya wapiga kura.

  Hatari iliyopo katika hatua hiyo inatajwa kuwa ni pamoja na chama hicho kupata wanachama mamluki, wasio na malengo ya kukitumikia chama hicho, wakiwa na malengo ya kukidhi maslahi binafsi ya mgombea husika na ya kwao.

  Inaelezwa pia ya kuwa chini ya utaratibu huu, viongozi watalazimika kupigana vikumbo kufungua matawi mapya ya chama na kununua kadi nyingi ili kuzitoa kwa wanachama wapya matawini. Wachambuzi wengine wa masuala ya siasa wanaeleza kuwa kuna hatari ya wagombea kuhodhi matawi, hali inayoweza kusogeza mpasuko wa kitaifa wa chama hicho hadi ngazi ya matawi.

  Faida kubwa ya mabadiliko hayo inatajwa kuwa ni kupunguza kile kinachoweza kuitwa mashindano ya kutoa rushwa, kwamba aliyetoa rushwa kubwa zaidi ndiye mshindi.

  Hata hivyo, faida hii inaangaliwa kwa tahadhari kubwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa, wakisema utaratibu huo hauwezi kuwa na tija au kufikia malengo yanayotarajiwa kama usimamizi wake hautazingatia misingi ya haki na badala yake kutumika kufanikisha malengo binafsi.

  Raia Mwema ilizungumza na baadhi ya wanachama wa kawaida wa chama hicho ambao wengi walifurahia utaratibu huo kwa kile walichoeleza kuwa wakati wa viongozi na wajumbe wa iliyokuwa mikutano ya kupendekeza wagombea kutamba kuwa wamepata fedha (rushwa) nono mitaani umefika ukingoni.

  Na wengine walikwenda mbali zaidi wakisema wakati wa wagombea kuteka wajumbe wa mkutano na kuwaficha hotelini ili kuwaweka sawa (kwa rushwa) ili wawape kura umekwisha na kwamba wanaamini kuwa hawatapata wakati mgumu kunadi wagombea kwa kuwa wagombea watakaopatikana watakuwa wanakubalika na sehemu kubwa ya wanachama na wananchi wa eneo husika.

  CCM ilipitisha utaratibu huo mpya katika mkutano wake wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
   
 2. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kila mmoja atavuna alichojipandia.
   
 3. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo ninapokubali kwamba sasa tunakwenda kwenye transition kwa maana sauti za watu wengi ndio zitasikika na sio wazushi wachache wanaodanganyika na chai za maziwa, pilau, kanga, mashati na elfu 10 kwenye bahasha za Kaki.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wafuasi wa SUltani CCM wanashangilia mauti ,ila kitu kimoja mbali ya utaratibu huo ambao utazaa mapambano kama yaliyotokea Pemba na kuwaondoa mashehe na wachungaji wa CCM ,ni kuzidi kusambaratika kwa wafuasi au vigogo ,sasa kama walikuwa wanatembeza bahasha kwa wajumbe ,yanayofuata ni kuwajengea nyumba wapiga kura ,system ambayo wanachama feki wa CCM Zanzibar waliweza kuitumia fursa hiyo kujikusanyia feza ,kigogo anatoa feza kumpa wakala ambae anatafuta wapiga kura kwa bei poa na adabu yake hao wanaopatiwa fedha hawazipeleki kura zao CCM wanazihamishia upinzani ambako kwa Zanzibar ni CUF,ndio ikabidi wafuasi wa CCM wenye kulewa na madaraka kukodi mamluki wakiwemo majeshi na mapolisi na wengine kutoka msumbiji ili kuwasaidia kuwapigia kura ,maana hata magari ya kuwahamisha kutoka kituo kimoja hadi kingine yalikuwa yanaonekana yakipishana njiani bila ya aibu ,sasa ninachokiona ambacho kinakaribia ni hapa Tanganyika itawabidi wafuasi wa CCM wakodishe ndege kuhamisha mamluki ,Sultani CCM kama hajawahi kupata upinzani wa nguvu kama ule uliomuangusha Pemba basi safari hii maji atayaita m'ma.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi Mwenyekiti wa CCM, Rais, unaweza kusema maneno hayo hadharani kuhusu wabunge kwamba waanze sasa hivi kujali majimbo? What about the lost 3 years? Yani waanze kwenda majimboni kabla ya uchaguzi?

  You know, sijawahi kufanya kazi ngumu kama ya Kikwete lakini sometimes Kikwete anasema vitu vinakufanya useme kama Urais ndo vile then any old Ally Pandu can fill the job of president of Tanzania and he can be just fine. The least you can do Rais hata uwe incompetent vipi ni kutoa propaganda. Sasa hapa hata propaganda Kikwete zinamshinda.

  Utasemaje wabunge waanze kujali kwa sababu uchaguzi unakuja? Yani unawapa silaha wapinzani waseme kwamba hata Mkuu wao CCM kasema wabunge wao walikuwa derelict the past three years! Kikwete anaharibu sijapata ona. Makes you wonder, is this the kind of careless thinking he brings to the desk of president?
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu, Mh Rais hapa anajaribu kuwa honest. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa wapiga kura huwa wanatumiwa tu kama daraja la kuupata ubunge/uwaziri, na maana ya raisi ni kuwa katika miaka hiyo mitatu ni kuwa kuna wabunge ambao hawa-kudeliver. Wapo wanaotembelea majimbo mara moja au mbili kwa mwaka, na kuwatembelea waheshimiwa wawili tu au watatu na kuwaacha wengine wanateseka. Hii ni fact, naona sytem mpya itakuwa ni ya mbunge kuvuna anachopanda.
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuhani, utterly, with reference to this man 'JK' any shit can hold the position and surely it'll make no difference. Have you listened at his speech posted with title ''Kwani budget ya Tanzania ni kiasi gani?''. He was advocating the need for America to continue giving aid despite of the economic down turn. I felt so shy to hear his speech.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pamoja na uamzi huu wa Sisi. M. Japo watu wanatetea kuwa elimu sio kigezo cha mtu kuweza kuongoza, nivizuri kiongozi akawa na uwezo wakuchambua mambo. Inasikitisha baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa Sisi. M. ni dalasa la saba. Kisa wanapesa kiasi na wameweza kuwainfluence wapigakura wao. Nasema hivi kwa sababu viongozi wa Sisi.M wanatokana na viongozi hawa. hivyo kama hakuna cream ya viongozi wenye uwezo wakupambanua mambo toka ngazi ya mwenyekiti wa wilaya au mkoa ni dhahili hata kiongozi wakitaifa atakuwa ni reflection ya hao wenzie.
   
 9. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Bm21,

  Si hata Pinda alikuwa Sweden majuzi nae akawaambia hivyo hivyo, waendelee kutoa misaada kama walivyoahidi wakati recession haijaja. Sasa, mimi kama Mtanzania natambua kwamba ni sisi ndio wanatupigania wanapo push matajiri waendelee kutoa, kwamba hatutaki kusikia cha recession wala cha depression. The thing is, though, sijui kama kina Pinda wanajua maana ya recession.

  Ndio maana naombea siku tupate kiongozi ambae amewahi kuishi nje.

  I am not talking about Mkapa types and Salim Salim na wazee wa generation Nyerere waliokwewnda nje na scholarship za John F. Kennedy wakalala mabwenini Columbia University wakisubiri kwenda nyumbani kuwa ma embassador and what not. Not the Lau Masha's of the world waliokwenda kiwanja utotoni wakamaliza high school Marekani wakaingia mitini, no no no. Mtu aliyewahi ku mantain maisha ya jujitegemea nje miaka kadhaa.

  Anaejua umuhimu wa employment vis a vis unemployment (atafikiria kubuni njia za ku create jobs Tanzania), akapiga mi overtime ikalimwa tax (angejua misaada ya wahisani inatoka wapi) akala mzigo wa shuruba usiolipa at some point (angejenga appreciation ya hali ya wananchi na wafanyakazi wa kipato kisichotosha Tanzania), akaleta uzembe kazini akawa fired (angejenga work ethic ya kutouza na kunywa chai na maandazi kazini all day), akakaa juu ya mawe kipindi anatuma job applications (angejifunza kudharau katabia ka kutegemea vi memo na vi connection kupata kazi) akavunja sheria hapa na pale akapigwa mi summons na wazee wa Interstate 95 (angejifunza kuheshimu sheria), akakutana na ubaguzi (hatachutama tena mbele ya some sleak "Mzungu" from a Guatemala aliyejichanganya kwetu anafukuzia some venal government contract), akahangaika na nyodo za wazee wa nondo (asingenyenyekea tena mbele ya wahindi na wageni wanaotunyanyasa nyumbani kwetu, that's right, Mzungu akija ofisini kwako Tanzania you ask to check his freaking immigration papers too, kumtingisha almuradi tu), aka split paycheck yake between the credit union and Western Union for his mother back home (ange appreciate umuhimu wa Wabongo walioko in the diaspora). The quintessential generation maboxi lifer. That kinda hardscrabble bootstrap background. Huyo ndiyo aina ya kiongozi tunayemhitaji pale Bongo.Wangekoma kuringa walahi!

  Kina Pinda na Kikwete wale bado wana ile panhandling mentality, house negro world view ya kubembeleza wazungu, supplicants, alivyosema Bob Geldof kwenye mkutano wa IMF Dar juzi. Sasa tajiri mwenyewe kachoka, kila siku wana jidedisha ma stock value yaki plummet, we bado unasubiri akupe kashilingi. To hell with that!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu unasomeka in bold aisee;

  Tatizo pamoja na ccm kurusha hilo taulo kwenye hii boxing match, hakuna idadi ya wapinzani tosha kupambania kila jimbo...

  Lets hope the change is gonna come
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jamani wabeba mabox tumo humu, for those who are ready physicaly, mentally and psychologically. Those who do not care about their financial status and are ready to start afresh with all the anticipated hardships. Mimi narudi.


  Change gonna come sooner or later, but some starting point have to be set. Yes we can if we stand together. Solidarity forever.
   
  Last edited by a moderator: Mar 15, 2009
 12. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Watoke wapi wakati wote wameamua kukumbatia mfumo ili wapate mkate wao? Kwani wapinzani ni nani? Nilidhani kwa yeyote anayekerwa na hali iliyopo na mwenye lengo la dhati la kujaribu kurekebisha. Tatizo ni pale watu wanapojali maslahi yao kwanza. Itafika wakati kila mmoja atakuwa mpinzani kwa hiari yake, wakati huo litakuwa ndio suluhisho pekee ili uendele kuishi na kuondokana na huu unafiki.
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Kuhani mku, you never cease to surprise me, kumbe you are a critical thinker, tena sana! sasa ulikuwa unamlaumu nini dada Aisha wa CNN alipomwuliza swali JK na rais wetu alichemsha wakati mwenyewe umekiri hapa kuwa hata Ally Pandu anaweza kuwa kuendesha nchi vyema zaidi kuliko JK?
  Never mind mkuu, I feel your pain, sometimes we cling to hope and invest it in people, but unless you are doing something yourself don't expect someone else to do it right. Mimi nakushauri Kuhani mkuu, uchukue hatua ya kuingia siasa na kuleta mabadiliko!
   
Loading...