DissDotCom
JF-Expert Member
- Mar 31, 2014
- 395
- 271
JIHADHARINI NA TAPELI HUYU ANAYEZUNGUKA HASA MAENEO YA VYUO (DAR)
Ilikua siku ya Jumatatu asubuhi nikiwa maeneo ya chuo (IAE) Posta, akatokea jamaa amevaa smart sana, akaniambia kaka natafuta mteja aweze kununua Laptop, akazidi kusema kuwa yeye ni mfanyakazi wa bandari hivyo ameipata katika moja ya magari yaliyopo bandari na ikiwa mpya katika box lake, kulingana na hali ilivyokuwa mbaya na bei aliyonitajia ya laki 200,000 tena unaweza kulipa kwa awamu nikapata tamaa ya kuinunua ili niuze nipate cha juu, nikajikuta namuamini ila kama kuna kitu kilinistua kwa wakati huo, nilikua na begi la laptop, smartphone na pesa cash kama laki 3, nikaona niviache vyote kwa mtu ili niende mweupe kama ni matepeli wagonge mwamba. Basi tukaanza safari ya kwenda bandari mguu kwa mguu huku huyo jamaa akiendelea kusifia kuwa ni mpya na vilevile kuna digital camera huwa wanaziokota hivyo atanijulisha baada ya kuinunua hiyo laptop. Tukiwa njiani akaniambia kuwa tununue mfuko wa rambo ili tuwekee hiyo laptop, nikatoa ile 500 tukanunua mfuko.Baada ya kufika bandari akaniambia nisubiri kwa nje kidogo pale kwenye jengo ta TRA, baada ya dk 5 akanipigia simu akasema sababu walinzi wanaijua hiyo issue basi wanabana kutoka nayo hivyo kuna ugumu, baada ya mda akaja niliposimama bila mzigo akaniambia kwakua tumepatana ni 200,000 basi wale walinzi wanahitaji 60,000 tu ili waweze kunyamaza mzigo ukitoka, kwakuwa sikuwa hata na shilingi nilimwambia yeye atoe yake tutoke na mzigo zen nikampe chuoni, jamaa akasema hana hata mia, akasema mwambie huyo wa chuoni akutumie ili tuwalipe tuondoke na mzigo tukamalizane chuoni, bahati nzuri au mbaya nilikua nishamstukia kuwa ni tapeli na mimi mwenyewe ni mtoto wa mjini. Jamaa akasema ngoja niende ndani nikipata mtu akiniazima natoka nayo, nikamwambia sawa. Alikaa kama nusu saa hivi akanipigia simu akasema samahani kwa kukuchelewesha na masomo we nenda chuoni ninauhakika nitapata hiyo hela nichukue mzigo nikufate. Nikwamwambia sawa, nilikaa hadi jioni sijapata simu yake tena. Yote kwa yote alifanikiwa kunitapeli 500 ambayo tulinunua mfuko.
NDUGU ZANGU HUYU JAMAA ANAZUNGUKA MAENEO YA VYUONI NAMBA YAKE YA SIMU NI (0687975576 Aliniambia anaitwa Daniel -Ila ukiangalia namba Airtel Money amesajiri kama Dastani Lwiza)