Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,098
- 34,914
UTENZI WA MAUTI.
1.Nipeni wino mweusi.
Pamoja na karatasi.
Niandike kwa upesi.
Mambo nalowandalia.
2.Ninataka kwa haraka.
Yote nipate andika.
Kabula sijaondoka.
Nikaiaga dunia.
3.Kwa yote niyaandike.
Inshallah yahifadhike.
Ili yaje yatumike.
Wajao kuyatumia.
4.Wajuwe kuna mauti.
Kwetu sisi ni sharuti.
Ameweka Jabaruti.
Mola ametuekea.
5.Wazi hayaepukiki.
Ni njia ilo ya haki.
Kwetu sisi ni tariki.
Sote tutaipitia.
6.Hakika kukumbushana.
Ni jambo lenye maana.
Ndio leo ninanena.
Utenzi kuwatungia
7.Ni mambo yenye na hofu.
Yalo na umaarufu.
Juu ya Mola Latwifu.
Illahi Mola Jalia.
8.Ni mambo yalo mazito.
Kwa mkubwa na mtoto.
Sote tuko kwa mapito.
Hili litatufikia.
9.Kutufikia mauti.
Kwenye wowote wakati.
Kujikatia tikiti.
Ya kurudi kwa Jalia.
10.Mwanzo nianze na kisa.
Vyema nitowe kabisa.
Mukipate hivi sasa.
Imani kitatutia.
11.Ni kisa chenye uzito.
Ni kisa chenye na joto.
Ni wakati wa mpito.
Mja anapojifia.
12.Palitokezea mtu.
Alojawa utukutu.
Mambo yalio na kutu.
Mengi alijifanyia.
13.Alifanya udhalimu.
Akipenda kudhulimu.
Kufanya yaso nidhamu.
Alokataza Jalia.
14.Mambo yenye uharamu.
Kwake yalikuwa tamu.
Yote ya Tumwa Hashimu.
Ni aliyapuzilia.
15.Tukija kwa familia.
Alikuwa nayo pia.
Ya mke watoto pia.
Mola alimjalia.
16.Alikuwa na watoto.
Na mke alo mzito.
Mzuri mithili ya kito.
Cha dhahabu nawambia.
17.Na aliwapenda sana.
Watoto wake nanena.
Na mke mwenye kufana.
Moyoni waliingia.
18.Na mali aliyapenda.
Akizidi kuyaunda.
Kila siku yuwapanda.
Mambo mengi ya dunia.
19.Hata ilipofikia.
Siku ilipowadia.
Ya kurudi kwa Jalia.
Kuagana na dunia.
20.Mwanzo ni alishikika.
Kwa maradhi kumshika.
Na ikawa pata shika.
Nyumbani kote sikia.
21.Hakika ilimbwaga.
Homa iso na muanga.
Akaingiwa uwoga.
Kuona hivyo sikia.
22.Hata alipozidiwa.
Ndipo wakamchukuwa.
Hosipitali kutuwa.
Matibabu kuzengea.
23.Kuzengea matibabu.
Kwa daktari swahibu.
Ili apate jitibu.
Maradhi yalomngia.
24.Hata ikaisha wiki.
Yani bado hatibiki.
Kwa maradhi hayatoki.
Hayataki kusikia.
25.Maradhi yalomshika.
Kwa wengine metibika.
Ela kwake kwa hakika.
Yamekataa sikia.
26.Ndio kumbe matibabu.
Ni Mola wetu Wahabu.
Anayetibu swahibu.
Shufaa kutujalia.
27.Lakini tunapoona.
Ni dawa zenye kufana.
Ndio juwa ni Rabana.
Sio dawa nambia.
28.Kama dawa zenye kupona.
Wagonjwa wangekosekana.
Chemistry zimejana.
Wagonjwa wazidi pia.
29.Na ndio kwa hali hini.
Yule mtu kwa yakini.
Illahi Mola Manani.
Shufaa hakumjalia.
30.Akazidi kuteseka.
Kwa maradhi kushika.
Hakika alikabika.
Taabani nawambia.
31.Ndio siku moja pia.
Alizidiwa sikia.
Akawa aelekea.
Kutaka aga dunia.
32.Mke wake kwa ukweli.
Washinda nae hosipitali.
Na watoto kulihali.
Wanalala nae pia.
33.Pia mujuwe kabisa.
Yuwalishwa hivi sasa.
Maradhi yamtokosa.
Kwa mwingi ulo udhia.
34.Huku yuwanyishwa uji.
Mara yuwanyishwa maji.
Hata hapati fajari.
Mara ajitapikia.
35.Na ndio ujuwe wewe.
Lokuwa ala mwenyewe.
Sasa yote afanyiwe.
Hata kuogeshwa pia.
36.Kwa kweli hini dunia.
Si kitu cha kujivunia.
Hivi watoto walia.
Mke na jamaa pia.
36.Machozi yanawatoka.
Baba leo aondoka.
Yuwaitwa na Rabuka.
Amuhitari Jalia.
37.Na mke nae halali.
Hata kula pia hali.
Leo Illahi Jalali.
Mume amuhitajia.
38.Kwa kweli alizidiwa.
Hata hawezi jijuwa.
Akhera yuwazengewa.
Na hayupo kwa dunia.
39.Nikizidi kutamka.
Kitandani kanyooka.
Angiyae na kutoka.
Hamjui nawambia.
40.Akikumbuka amali.
Hakufanya kwa ukweli.
Yuwajuta kulihali.
Kutenda yenye udhia.
41.Yuwaomba kwa hakika.
Japo kwa moja dakika.
Amrudishe Rabuka.
Kumpa yake afia.
42.Atende njema amali.
Zimfae kwa ukweli.
Endapo kule mahali.
Kaburini nawambia.
43.Hapo vyazidi viliyo.
Vya watoto siku hiyo.
Wanalikosa pumbao.
Baba awaondokea.
44.Nikizidi kupa picha.
Vilio hapo vyachacha.
Baba leo watuacha.
Wanao tutaumia.
45.Watuachia na nani.
Wanao sisi yakini.
Baba yuko kitandani.
Amri aisubiria.
46.Huku yuwaza sana.
Yale mambo yaso mana.
Yuwaoneshwa bayana.
Na Maika sikia.
47.Mambo yalo na uovu.
Mambo yenye upotevu.
Hivi sasa hana nguvu.
Baba za kujitetea.
48.Huku yake familia.
Kwa aliyojifanyia.
Hawajui nawambia.
Aliyofanya sikia.
49.Hawajui ni haramu.
Mali yake muadhamu.
Alolala kwa nidhamu.
Kitandani nawambia.
50.Ni wanazidi kulia.
Kwa mwingi ulo udhia.
Baba awaondokea.
Yuwaiaga dunia.
1.Nipeni wino mweusi.
Pamoja na karatasi.
Niandike kwa upesi.
Mambo nalowandalia.
2.Ninataka kwa haraka.
Yote nipate andika.
Kabula sijaondoka.
Nikaiaga dunia.
3.Kwa yote niyaandike.
Inshallah yahifadhike.
Ili yaje yatumike.
Wajao kuyatumia.
4.Wajuwe kuna mauti.
Kwetu sisi ni sharuti.
Ameweka Jabaruti.
Mola ametuekea.
5.Wazi hayaepukiki.
Ni njia ilo ya haki.
Kwetu sisi ni tariki.
Sote tutaipitia.
6.Hakika kukumbushana.
Ni jambo lenye maana.
Ndio leo ninanena.
Utenzi kuwatungia
7.Ni mambo yenye na hofu.
Yalo na umaarufu.
Juu ya Mola Latwifu.
Illahi Mola Jalia.
8.Ni mambo yalo mazito.
Kwa mkubwa na mtoto.
Sote tuko kwa mapito.
Hili litatufikia.
9.Kutufikia mauti.
Kwenye wowote wakati.
Kujikatia tikiti.
Ya kurudi kwa Jalia.
10.Mwanzo nianze na kisa.
Vyema nitowe kabisa.
Mukipate hivi sasa.
Imani kitatutia.
11.Ni kisa chenye uzito.
Ni kisa chenye na joto.
Ni wakati wa mpito.
Mja anapojifia.
12.Palitokezea mtu.
Alojawa utukutu.
Mambo yalio na kutu.
Mengi alijifanyia.
13.Alifanya udhalimu.
Akipenda kudhulimu.
Kufanya yaso nidhamu.
Alokataza Jalia.
14.Mambo yenye uharamu.
Kwake yalikuwa tamu.
Yote ya Tumwa Hashimu.
Ni aliyapuzilia.
15.Tukija kwa familia.
Alikuwa nayo pia.
Ya mke watoto pia.
Mola alimjalia.
16.Alikuwa na watoto.
Na mke alo mzito.
Mzuri mithili ya kito.
Cha dhahabu nawambia.
17.Na aliwapenda sana.
Watoto wake nanena.
Na mke mwenye kufana.
Moyoni waliingia.
18.Na mali aliyapenda.
Akizidi kuyaunda.
Kila siku yuwapanda.
Mambo mengi ya dunia.
19.Hata ilipofikia.
Siku ilipowadia.
Ya kurudi kwa Jalia.
Kuagana na dunia.
20.Mwanzo ni alishikika.
Kwa maradhi kumshika.
Na ikawa pata shika.
Nyumbani kote sikia.
21.Hakika ilimbwaga.
Homa iso na muanga.
Akaingiwa uwoga.
Kuona hivyo sikia.
22.Hata alipozidiwa.
Ndipo wakamchukuwa.
Hosipitali kutuwa.
Matibabu kuzengea.
23.Kuzengea matibabu.
Kwa daktari swahibu.
Ili apate jitibu.
Maradhi yalomngia.
24.Hata ikaisha wiki.
Yani bado hatibiki.
Kwa maradhi hayatoki.
Hayataki kusikia.
25.Maradhi yalomshika.
Kwa wengine metibika.
Ela kwake kwa hakika.
Yamekataa sikia.
26.Ndio kumbe matibabu.
Ni Mola wetu Wahabu.
Anayetibu swahibu.
Shufaa kutujalia.
27.Lakini tunapoona.
Ni dawa zenye kufana.
Ndio juwa ni Rabana.
Sio dawa nambia.
28.Kama dawa zenye kupona.
Wagonjwa wangekosekana.
Chemistry zimejana.
Wagonjwa wazidi pia.
29.Na ndio kwa hali hini.
Yule mtu kwa yakini.
Illahi Mola Manani.
Shufaa hakumjalia.
30.Akazidi kuteseka.
Kwa maradhi kushika.
Hakika alikabika.
Taabani nawambia.
31.Ndio siku moja pia.
Alizidiwa sikia.
Akawa aelekea.
Kutaka aga dunia.
32.Mke wake kwa ukweli.
Washinda nae hosipitali.
Na watoto kulihali.
Wanalala nae pia.
33.Pia mujuwe kabisa.
Yuwalishwa hivi sasa.
Maradhi yamtokosa.
Kwa mwingi ulo udhia.
34.Huku yuwanyishwa uji.
Mara yuwanyishwa maji.
Hata hapati fajari.
Mara ajitapikia.
35.Na ndio ujuwe wewe.
Lokuwa ala mwenyewe.
Sasa yote afanyiwe.
Hata kuogeshwa pia.
36.Kwa kweli hini dunia.
Si kitu cha kujivunia.
Hivi watoto walia.
Mke na jamaa pia.
36.Machozi yanawatoka.
Baba leo aondoka.
Yuwaitwa na Rabuka.
Amuhitari Jalia.
37.Na mke nae halali.
Hata kula pia hali.
Leo Illahi Jalali.
Mume amuhitajia.
38.Kwa kweli alizidiwa.
Hata hawezi jijuwa.
Akhera yuwazengewa.
Na hayupo kwa dunia.
39.Nikizidi kutamka.
Kitandani kanyooka.
Angiyae na kutoka.
Hamjui nawambia.
40.Akikumbuka amali.
Hakufanya kwa ukweli.
Yuwajuta kulihali.
Kutenda yenye udhia.
41.Yuwaomba kwa hakika.
Japo kwa moja dakika.
Amrudishe Rabuka.
Kumpa yake afia.
42.Atende njema amali.
Zimfae kwa ukweli.
Endapo kule mahali.
Kaburini nawambia.
43.Hapo vyazidi viliyo.
Vya watoto siku hiyo.
Wanalikosa pumbao.
Baba awaondokea.
44.Nikizidi kupa picha.
Vilio hapo vyachacha.
Baba leo watuacha.
Wanao tutaumia.
45.Watuachia na nani.
Wanao sisi yakini.
Baba yuko kitandani.
Amri aisubiria.
46.Huku yuwaza sana.
Yale mambo yaso mana.
Yuwaoneshwa bayana.
Na Maika sikia.
47.Mambo yalo na uovu.
Mambo yenye upotevu.
Hivi sasa hana nguvu.
Baba za kujitetea.
48.Huku yake familia.
Kwa aliyojifanyia.
Hawajui nawambia.
Aliyofanya sikia.
49.Hawajui ni haramu.
Mali yake muadhamu.
Alolala kwa nidhamu.
Kitandani nawambia.
50.Ni wanazidi kulia.
Kwa mwingi ulo udhia.
Baba awaondokea.
Yuwaiaga dunia.