Utenzi Mahiri..........Gogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utenzi Mahiri..........Gogo

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by CAMARADERIE, Sep 15, 2011.

 1. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kuna gogo la muanga, njiani limeanguka
  Waja mafundi kuchonga, kibanzi kutobanjika
  Watu wavunjika nyonga, kwa kupanda na kushuka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Waja wenye mbinu zao, hupanda wakadunguka
  Waja na wavamiao, kwa papara na haraka
  Wako pia waliao, gogo lipo lawacheka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Letu sote gogo hili, kilitaka lakutaka
  Afanyae hatambuli, mja huyo asumbuka
  Thamani yake ni ghali, wala hili si dhihaka
  Kula ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Hili gogo madhubuti, si rahisi kukatika
  Tukishindwa tukaketi, bandu mwisho hubanduka
  Tukikosa jizatiti, gogo litaja anguka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Bandu humaliza gogo, hilo sheti kukumbuka
  Tusijitie mikogo, kudharau kila shoka
  Tusilikimbie zogo, pembeni jema kuweka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ushairi mzuri sana nimeupenda sana.

  Insh'Allah nitarudi baadae
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Watu hawajui shekhe
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,759
  Trophy Points: 280
  Lapokuwa gumu gogo, Shoka linapozidiwa,
  Lipaswi pewa kisogo, Mbinu mpya hutakiwa,
  Kwani gogo la mhogo, lishindwe kupasuliwa?
  Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.

  Msumeno ntatumia, gogo kulibanjuani,
  Mbele kiushindilia, banzi walitakiani?
  Nyuma kiurudishia, gogo lina gumu gani?
  Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.

  Shoka kazi yake kuni, Mpishi lampatia,
  Kumletea jikoni, kuni za kumpikia,
  Zikishapigwa juani, shoka inazipatia,
  Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Swadakta........
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwanza ejaribu Chali, mchanjaji wa Msuka
  Kisha akakwea Duli, kwa dhihaka akashuka
  Nasabawe Mizamyuli, gogo helitaharuka
  Gogo haliebu shoka, li kweche lakwerezuka

  Akapanda Sefu Chalyo, baba la miraba nyuka
  Akarudi na miyayo, mpwawe Miza mizuka
  Alimasi yake yayo, mpini ukapasuka
  Gogo haliebu shoka, li kweche lakwerezuka

  Seremala hachanjili, apikia kwa nkaa
  Nyie mwamleta Chili, mchomaji wa chokaa
  Hapa tumtaje Pili, kwa mipingo kachakaa
  Gogo haliebu shoka, li kweche lakwerezuka
   
 7. a

  amiride JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  muruwa kabisa enzi za wasomaji mashairi maarufu kina mariam ponda na mzee khalifani wangeghani vizuri
   
 8. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naaam.........Swadakta, ushairi at its best, fani hii ni adimu na si sote wenye uwezo wa kucheza na lugha/ ghani namna hii, Heshima kwako

  <br />
  <br />
   
 9. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naam........Nadiriki kusema nimejifunza na naendelea kujifunza mengi toka ktk tungo zako, sijamuona mwalimu wangu klorokwini, hapiti huku?


  <br />
  <br />
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Si jiti hili ni gogo, kijasho kiliwatoka
  Migongo yengia pogo, walichoka wakauka
  Kimewashinda kigogo, walia watu wacheka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Mashoka yao ya vyuma, wageni mbali metoka
  Kuja gogo kulipima, kijasho kikawatoka
  Kuona isitiqama, gogo lilivyotukuka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Gogo mevuka viunzi, vya kiangazi masika
  Limekabili mionzi, bila ya kutetereka
  Kalilinda Mwenye Enzi, thabiti halina shaka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Muhali gani malenga, na gogo lisochangika
  Gogo hili sio changa, kwa kweli limepevuka
  Limebeba nyingi kunga, na siri za mamlaka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Ukiliona karibu, vile lilivyoongoka
  Ukapewa masahibu, na vile lilivyon'goka
  Utatamani kutubu, mlinzi Mola Rabuka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

  Wazamani na wa sasa, gogo walilizunguka
  Kwa hila walipapasa, wajuzi walosifika
  Gogo limekuwa tasa, katu halikupasuka
  Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala
   
 11. A

  Albimany JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Gogo ukilijuulia,katu halitashindika.
  kwanza nikulipandia,halafu ukashuka.
  liguseguse ubavuni,kama laparuzika.
  ukiliona laini.hapo usibebe shoka.
  sikila gogo ,lachanjwalo kwa shoka.

  Ukucha ni zana, pia yaweza tumika.
  Ukijulia kuliparura,lazima litabambuka.
  Anza na matawi, kuyakuchakucha.
  Ukifika kigogoni,lishaanza kuchimbuka.
  Sikila kigumu,chachanjwa na skoka.

  Ziko zana kali,zishindazo shoka.
  Simsumeno, panga na sishoka,
  ni mfano wa patsi,ilioviringika.
  zavunjazo magogo,yalioanguka.
  Si magogo yote,yachanjwayo kwashoka

  Yataka hekima,hadi kupasuka.
  Ukilipatia pakuanzia,lile hutetemeka.
  Hutoka maji shinani,likaanza kuweweseka.
  Ukiingiza patasi,laanza kubogojeka.
  Ugumu ni mwanzoni,ukitumiaakili lakatika.

  ISIMBA MKALI ALINYESHWA CHAI, NINI CHASHINDIKA?.
   
 12. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tungo zenu nimesoma, nyote mlotangulia
  Gogo limefanya goma, au hamjajulia?
  Ya nini kushika tama, acheni kulia lia
  Gogo hilo gogo gani, hakuna alikatae?

  Kateni mbele na nyuma, hakika litabanjuka
  zana zenu ziwe vyuma, vile visivyo pindika
  msifanye ya hujuma, ustadi wahitajika
  Gogo hilo gogo gani, hakuna alikatae?
   
 13. a

  amiride JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  bandu bandu yamara gogo, gogo la choo laona mengi
   
 14. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Gogo liso chanjika

  ukataji mbele nyuma,hili lakubalika
  ongeza kwa kujituma,huku walishikashika
  siache kulisukuma,lengo liweze banjika
  Gogo liso chanjika,faidae iko wapi?

  Nini wajipa kadhia,kwa gogo liso chanjika
  Mwishoe waja tufia,na ndugu uwape shaka
  Ni bora kujiachilia,hilo halina baraka
  Gogo liso chanjika,faidae iko wapi?

  Kuzidi lazimishia,ni wewe wajiumiza
  hutopata yafidia, gogo hilo miujiza
  Muda wako tajutia,na lengo hutotimiza
  Gogo liso chanjika,faidae iko wapi?

  Ni vyema useme basi,ni tendo la uungwana
  sitoe tena nafasi,gogo halina maana
  Hata unoe patasi,huwezi lichanachana
  Gogo liso chanjika,faidae iko wapi?

  Gogo hilo ni la tasa,umri limezidia
  ona ya kwake mikasa, nuksi tajipatia
  mfano wake ni kasa,chunguza utanambia
  Gogo liso chanjika,faidae iko wapi?
   
Loading...