Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,985
- 20,263
Napokea maombi ya wafuasi wangu Inbox wakitaka maoni kuhusu utenguzi, na uteuzi wa IGP na DCI. Maoni yangu ni mafupi tu, Jeshi la Polisi lina siasa kali ambazo zinaliangamiza taifa, Ushauri nilishauweka katiks kitabu cha Ujasusi, Mh Rais vunja jeshi hili na unda Huduma ya Polisi.
Kwa maoni yangu, Sifikiri mabadiliko ya mtu ndani ya Jeshi la Polisi, Si Wambura, Si Kingai, hawa wote ni mfumo uleule wa siasa kali za jeshi la Polisi. Ninaamini mabadiliko ya kitaasisi kimfumo, na kisheria ziadi.
Kwa wasiojua wakati wa kumbambikia kesi Mbowe na Wapinzani wengine nchini, Mkuu wa Polisi (IGP) alikuwa Siro, Mpelelezi wa Taifa (DCI) alikuwa Boaz, Mpelelezi wa Kanda ya Dar (ZCO) alikuwa Wambura, na Kigai akiwa mpelelezi wa Mkoa wa Kinondoni. Hawa wote ni kitu kimoja. Leo rais hawezi kumtoa mbinguni mtu wa kuwa IGP au DCI, ni lazima amtoa hukohuko Polisi.
Tatizo sio watu, ni mfumo wa Jeshi zima unaoruhusu siasa kali na hatari kwa Taifa letu. Jeshi la Polisi linaundwa na mfumo wa kikoloni ambao unazingatia kanuni kuu tatu: 1. Mkubwa hakosei, 2, Akikosea rejea kwenye kanuni ya kwanza.
Kwa dunia ya leo mtu asiyejua PGO mbele ya macho ya dunia, leo ankuwa mpelelezi mkuu katika dunia ya kisasa ya modern Spy or Modern Investigator or Modern detective. Ni hatari kwakweli, Ndiomaana ushauri kwa Rais ni kuvunja jeshi la Polisi na kuunda chombo kingine. Dunia ya leo mtu hasifiwi kwa kupambana na majambazi, Bali kwa kuzuia ujambazi. In a digital technology na sio vinginevyo. Leo uhalifu wa silaha umebaki mikoani na maeneo machache, Dinia iko kwenye uhalifu wa Kidigitali ndiko tunakotakiwa kuwekeza kwa nguvu zote. Cyber security ndio eneo muhimu sana.
Tukija uteuzi wa Simon Siro kuwa Balozi, kwangu bado hatujajua kama taifa tunahitaji nini toka katika balozi zetu, Kumteua Siro kuwa Balozi ni lazima tujiulize, ni nini tunataka a delivery ambacho hakuki delivery akiwa IGP. Je uhusiano wetu na Zimbwe ni wakijeshi hadi tupeleke Mjeshi huyu? Ninaamini Zimbawe ni eneo muhimu la kutafuta wateja wa Bandari yetu na Wateja wa mazao yetu ya kilimo, pia usafirishaji, Taifa lingepeleka balozi mwenye ujuzi wa uchumi na masoko kijana akapambane huko kuliko kupeleka Mzee wetu ambae ameshastafu.
_______