ubarikiwe ni hv ili kutengeneza uahitaji yafuatayo:
caustic soda,mafuta:,mawese,nazi,nyonyo,mbosa au mise.,chumvi,glicerin,perfume na rangi.
i) JINSI YA KUTENGENEZA.
Chukua caustic soda kg1 changanya na maji lita 5 koroga kwa dk 5 acha kwa siku 7.N.B:Chombo utacho tumia kuchanganya isiwe plastic.
ii)Baada ya siku hizo saba changanya na mafuta lita 10 ikumbukwe mafuta utayotumia ni aina moja wapo kati ya hizo tajwa hapo juu hasa kwa kuzingatia ni yapi yana bei nzuri sokoni.
Mafuta hayo unayachemsha sawa sawa yahive hii unaweza kutambua kwa kutumbukiza karatas nyeupe ikitoka nyeupe yameiva so acha yapoe na baadae koroga kwenye mchanganyiko huo huo na kuweka glicerin robo lita,chumvi robo kg,rangi kijiko cha chai,na perfume kijiko cha chai.
Baada ya kukoroga utapata uji mzito ambao utapeleka kwenye "mould" hv ni vifaa maalum vyenye umbo tayari kama mche wa sabun vyaweza kuwa vya mbao au chuma.Tunatumia hivi kutokana na bei ya mashine ya sabun hz kuwa ghali mno.
Ili iitwe sabuni inatakiwa
-Ngumu kuiisha
-Yenye povu jingi
-Nyeupe
VIAMBATA VYA kutengenezea sabuni
1)Mafuta-mawese,mise,wanyana
2)Maji
3)Caustic soda(costiki soda)
VIFAA VYA KUTENGENEZEA
-Ndoo za plastiki lita 20 nne
-Diaba 1
-Mti wa kukorogea
-Mashine ya kukorogea
-Box la kugandishia
-Mhuri wa biashara
-Mzani wa saa
-Vibao vya kukatia
VIFAA VYA USALAMA
-Mask
-Groves
-Gum boots
-Goggles (miwani)
-Overall
-Ndoo ya maji au mchanga
FORMULA
-mafuta lt1+caustic soda grm135+maji mls350+sodium siligate prm100
KUCHANGANYA
pima maji ktk ndoo ya plastic kisa weka caustic soda ktk maji weka kidogokidogo huku ukikoroga mpaka itakapo yeyuka.mchanganyiko huu unaweza kuchemka na kutoa mosh usiogope. acha ipoe kuanzia masaa 8 nazaidi
KUCHANGANYA NA MAFUTA
yeyusha mafuta kwa kuyapasha joto kidogo ambapo unaweza kuyashika, tia sangi na mimina kidogo2 kuchanganya michanganyiko huku ukikoroga. mimina kwenye box la kugandishia acha igande tayari kwa kukata.Pia weka sodium siligate
JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUNAIWIA MIKONO View attachment 376324
Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.
Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono. Fuatana nami mwanzo mpaka mwisho.
MAHITAJI; .
Sulphonic acid .soda ash .maji yaliyochujwa vizuri .pafyum .Rangi yoyote inayovutia .sless .Chumvi
JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi.
Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako. Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.
Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai.
Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu.
Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.
Kwa ufupi mpendwa hapo juu amesaidia sana maelezo ila mimi ningependa kama upo dsm naweza kuja kukufundisha.0717539573 ila ukipata semina ya Dr.Lunyungu ni nzuri kwani hata mimi ni zao lake.
mbona lahisi sana just pm me nd i will send u the simple way how to make it, however u need to find out where u can buy your supply material( vitu unavyohitaji kutengeneza):A S-key:
if you can share public do so kuliko haya masuala ya PM PM kama unauza pia just say kama tunaweza kununua huo utaalamumm najua vitu vingi kwa dsm niPM ili tuwe na kikundi tutengeneze vitu kibao.Make c unajua na uchaguzi unakuja taasisi nyingi tutapokelewa vizuri ili tujikwamue kwani ka kiwanda ketu lazima wanasiasa wakaneemeshe na kura hatuwapi.