Utendaji wa Papa waendelea kuduwaza wengi

Utendaji wa Papa waendelea kuduwaza wengi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Vatican City. Papa Francis ameadhimisha misa yake ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, huku akitoa hotuba ya dakika tano mbele ya waumini wa Parokia ya Mtakatifu Anna.
Jana, katika mahubiri yake mafupi, Papa Francis alishangaza wengi kwa kueleza kuwa binadamu hawana budi kusameheana, kama ambavyo Mungu amekuwa mwenye huruma kwa wanadamu.
Awali, Papa alijitokeza hadharani katika lango kuu la kuingilia kanisa hilo la parokia akiwa amevaa kanzu nyeupe, viatu vyeusi, kuwapungia mkono watu wote, kisha kupeana nao mikono.
Kisha, alibusu, kuwashika mabegani watoto na kueleza kuwa jukumu la binadamu ni kupendana.
“Ningependa sisi sote tuwe na ujasiri wa kutembea katika uwepo wa Mungu,” alisema Papa Francis kwa Kilatini.
Mapema, Papa alifanya maombi binafsi katika Kanisa Kuu la Santa Maria Maggiore na baadaye alikutana na watoto na wasafiri waliokwenda kumsalimia.
Papa, pia ameanza kazi ya uteuzi wa maofisa wa juu wa Vatican, ingawa orodha hiyo haijakamilika wala kuwekwa wazi.
Jumatano usiku muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake, aliusalimia umati wa watu waliofurika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro akitoa wito wa unyenyekevu na kuwaomba waumini wamwombee baraka kabla yeye hajawabariki.
Alhamisi, Papa Francis alirudi kwenye makazi ya watumishi yaliyopo mjini Rome alipokuwa akiishi mbele ya jengo la mikutano ulimofanyika uchaguzi uliomweka madarakani.
“Alifungasha mizigo yake na kwenda kulipia chumba alichofikia ili kuwa mfano bora.
“Pia, alivunja utamaduni wa kwenda kuwasubiri makardinali waliokwenda kumpa pongezi, badala ya kukaa kwenye kiti cha enzi,” alisema msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi.
Ijumaa alikutana na makardinali 106 wakiwamo wale ambao hawakuingia kwenye mkutano wa uchaguzi.
Jumamosi, Papa alikutana na mamia ya waandishi wa habari wa kimataifa na kuweka msimamo wa kanisa lake.
Siku ya Ijumaa, anatarajiwa kumtembelea mtangulizi wake , Papa Benedict XVI, eneo la Castel Gandolfo, nje kidogo ya Mji wa Rome.
Kumtembelea mtangulizi wake kunaelezwa kuwa ni muhimu kwa kuwa kuwepo kwake kunaweza kuleta upinzani katika madaraka yake.
Papa Francis anatarajia kusimikwa rasmi Jumanne katika misa ya uzinduzi ambayo itahusisha maelfu ya waumini.
Ingawa alitajwa kushika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2005 uliomweka madarakani Papa Benedict XVI, baadhi ya watu walitabiri kuwa papa atakayefuatia atatoka nje ya Ulaya.
Akiwa mzaliwa wa Amerika ya Kusini, anaonekana kuwa mtu aliyeshika mno mafundisho na mwenye misimamo.
Hali hiyo inamfanya kuonekana kama mtu wa mabadiliko katika utendaji wa Vatican akisaidiwa na makardinali waliomzunguka.
Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema Papa Francis anakabiliwa na changamoto nyingi katika uongozi wake hasa kwa kuwa kanisa hilo linakabiliwa na kashfa za unajisi zilizowakumba makasisi wake na tuhuma za rushwa.
Changamoto nyingine inayomkabili ni pamoja na suala la wanawake kupewa upadri, kuibuka kwa madhehebu na kupukutika kwa waumini kunakoendelea katika sehemu mbalimbali duniani, ikiwamo Ulaya na Marekani.
Papa Francis au Kardinali Jorge Mario Bergoglio, alizaliwa Desemba 17, 1936 mjini Buenos Aires, Argentina. Ni mfuasi wa Shirika la Wajesuiti tangu mwaka 1969 na alisomea Argentina na Ujerumani. Alipewa ukardinali mwaka 1998.
*Elias Msuya kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.

by: www.mwananchi.co.tz
 
Asa anachozidi kushangaza dunia hapo ni kipi?mbna yote yalishaandkwa?
 
Asa anachozidi kushangaza dunia hapo ni kipi?mbna yote yalishaandkwa?

Mkuu hatuna waandishi siku hizi, na hili eti ndio gazeti makini, uandishi wa siku hizi ni ule wa kupewa hela na kuelekezwa andika hili zaidi ya hapo ni madudu tu, kichwa cha habari na content yake tofauti kabisa
 
Hivi nikwanini wanamuita mtakatifu,vigezo gani huwa vinatumika mpaka uwe mtakatifu
 
Mwandishi kaandika kihisia zaidi kuliko uhalisia. Hawa ndiyo wanaosaidia kushuka kwa taasisi fulani.
 
I thnk kuna vyuo vya uandishi wa habari vyo voda fasta
 
I thnk kuna vyuo vya uandishi wa habari vyo voda fasta

Form 4 au 6 failure ndio wanaendaga kusoma hizi kozi za uhandishi wa habari na utangazaji, kama ilivyo kwa wale wa ualimu. Kwa hiyo, mimi sishangai heading kuwa tofauti na content....
 
Hivi nikwanini wanamuita mtakatifu,vigezo gani huwa vinatumika mpaka uwe mtakatifu
"Baba Mtakatifu" ni jina la anachofanya, sio sifa yake. Ni kama tunavyosema Mtukufu Rais, hata kama mhusika hajatukuka. Wako Mapapa ambao wametangazwa kuwa watakatifu, na wako wengine walikuwa kama mimi na wewe tu.
 
AUGUSTINE MOSHI soma maandiko upate maalifa usipelekwepelekwe kama wafuasi wa kibwetele hakuna babamtakatifu duniani anaetoa utakatifu ni mngu pekeyake ukiwa mkristo fuata nyayo za kristo,siyo za papa ni mwanadamu kama mimi wewe na ombaomba matonya
 
mh kipi ndo cha kuzidi kushangaza hapo????
 
Hivi nikwanini wanamuita mtakatifu,vigezo gani huwa vinatumika mpaka uwe mtakatifu

Kama ni Mkristo na hasa kama ni Mkatoliki swali hilo lisingekusumbua, bila shaka wewe ni Protestant au utakuwa ni Asalam Alekhum. Yesu Kristo aliteua Mitume Kumi na Mbili, katika mitume hao alikuwemo Simon ambaye Yesu alimbatiza jina Jipya akamwita Petro akimaanisha Mwamba na kumteua kuongoza Kanisa pale aliposema. Simon wa Yona wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.........." Petro aliongoza Kanisa na alipofariki alizikwa pale Vatican. Baada ya Pope Petro alifuatiwa na Pope Saint Linus aliyefariki mwaka 76, na alifuatiwa na Saint Anacletus. Mtindo wa kumrithi Kiongozi wa Kanisa Katoliki umekuwepo tangu hapo. Utakatifu wa Pope haumaanishi kuwa yeye ni Mtakatifu la hasha bali Kiti anachokikalia ni Kitakatifu, ni Kitakatifu kwa sababu Yesu Kristo wa Nazareti alimteua Petro Mtume wake kukalia kiti hicho cha kuongoza Kanisa.



TUMSIFU YESU KRISTO WA NAZARETI
 
kweli wewe ni msema ovyo neno petro kwakiebrania ni petra yaani mwanba wa jiwe na mwamba ni yesu. jiwewalilo likataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni na PETRO hakuzikwa ROMA kwani ni ushenzini nandio walio takakumuuwa yesu akiwa mdogo HERODE
 
Papa anaitwa Baba Mtakatifu si kwa nafsi yake binafsi kama mwanadamu bali kwa cheo na dhamana ya kazi zake kama mwakilishi wa Mungu katika Kanisa. Hivyo utakatifu wa papa ni kwa ajili ya nafasi ya kuwa kiongozi mkuu wa kanisa ambaye amerithi mikoba kutoka kwa Petro ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa kwanza wa kanisa (Papa) la kikatoliki. Kwa maneno cheo cha upapa ni cheo kitakatifu hivyo nayekipata naitwa Baba Mtakatifu.
 
papa= ant crist kama unabisha angalia nyuma ya kiti chake msalaba ulivyowekwa
 
Jamani liacheni kanisa katoliki lipumue.Acheni wivu usiyo na msingi.
 
Back
Top Bottom