Ndugu yangu na rafiki mpendwa Abdul Msangi ambaye ndiwe Manager Security wa hapo JNIA, tafadhali pitia CCTV uangalie vema tukio hilo na kujudge validity yake.
kwa kawaida vimiminika au maji unatakiwa iviweke kwenye check inn luggage , na kama ni kubeba mkononi unatakiwa ununulie hapo hapo airport kwenye duty free shop, hivyo kuondoa hatari kwa abiria na kuonjeshana. kama ni sumu iwe ya panya nk itakuaje ni threat kwa abiria? au atawanywesha kwa nguvu? na kama umeona na hivyo basi mwambie abiria aweke kwenye chek in luggage. hao pilisi walitaka tu kuonyesha mabavu yao sio vizuri kutetea hii kitu.Pole sana kwa yaliyo kukuta mkuu,kwa kawaida kuna mashine ya kutest unga,kulazimishwa kuonjeshwa haikuwa njia sahihi.
Ilikuwa ni kiasi cha kuchota unga kidogo na kuuingiza kwenye mashine na majibu yangepatikana hapo hapo na ungeruhusiwa kuendelea na safari. Au pia kuna vifaa vya kutestia viko kama tester za umeme(au kwa lugha rahisi screw drivers)nikiasi cha kukichukua na kukichoma kwenye mzigo unaoshukiwa na majibu yangepatikana there and then.
Lakini pia kaka kuna wakati ambapo inamlazimu mtu kulazimishwa kuonja alichokibeba ila ni katika situation zifuatazo:
1. Huwezi ukatest maji kwenye mashine na kugundua kama ni acid au any other burning chemical, ili uweze kuyatest ni lazima yaonjwe, na wa kuyaonja ni abiria mwenyewe kwani maji hayo ni ya kwake. Kama itakuwa ni kitu tofauti na maji lazima abiria atagoma kuyaonja.(hii inakuwa pale afisa mkaguzi anapokuwa na mashaka na kimiminika hicho)
2. Kuna baadhi ya watu hubeba dawa zao za kienyeji kwa ajili ya safari, hivyo basi huwezi kuzitest zaidi ya kuwaambia wazionje kama kweli ni dawa na wanazitumia, kama sio dawa za kunywa basi wanashauriwa waziweke kwenye check in luggages.
3. Endapo afisa mkaguzi kawa na mashaka na mzigo wa abiria,baada ya kuutest na kugundua kuwa sio drugs, lakini akawa na mashaka kuwa inaweza kuwa ni sumu ya aina yoyote ile ambayo inaweza kuleta madhara wakati wa safari basi atamuhitaji mwenye mzigo aonje ili kuthibitisha kuwa sio sumu. Endapo itakuwa sumu basi hata muhusika hataweza kuonja.
NB:
MARA NYINGI MASUALA YA USALAMA HAYANA FORMULAR, ILI ABIRIA AWEZE KUSAFIRI LAZIMA AFISA MKAGUZI ARIDHIKE KUWA ALIYEMKAGUA NI SALAMA KABLA HAJAMRUHUSU KUENDELEA NA SAFARI. NI SUALA LA MTU KUJIRIDHISHA.
kwa kawaida vimiminika au maji unatakiwa iviweke kwenye check inn luggage , na kama ni kubeba mkononi unatakiwa ununulie hapo hapo airport kwenye duty free shop, hivyo kuondoa hatari kwa abiria na kuonjeshana. kama ni sumu iwe ya panya nk itakuaje ni threat kwa abiria? au atawanywesha kwa nguvu? na kama umeona na hivyo basi mwambie abiria aweke kwenye chek in luggage. hao pilisi walitaka tu kuonyesha mabavu yao sio vizuri kutetea hii kitu.
Hapo JNIA panahitaji marekebisho kwa kweli...
Hivi hao viongozi/wakubwa wa hapo JNIA huwa hawatembelei viwanja vya nje kujua wenzetu wanafanyaje kazi?Uongozi hauna utaratibu wa kuwapeleka wafanyakazi wake nje ya nchi kujifunza namna wenzaoa wanavyofanya kazi?
Yaani ukitembea ktk viwanja vya nje,ukaja kutazama na cha kwetu...TUNATIA AIBU SANA...
Wafanyakazi wapo local, local tuuu, customer care ya wale security ni ovyooo, wanaombaomba tips ovyoo...sijui hata mishahara yao ikoje? Niliwahi kusikia hapa kuna AJIRA za kujuana sana.
Hebu mamlaka tupieni jicho hiyo TAA....mgeni yeyote taswira ya kwanza ni Airport...haya majamaa yanatuaibisha sana ndugu zanguni.
Yakuongea na bosi wao ni mambo ya ulaya..huku unaweza kujibiwa hayupo na ukaendelea kuchezeshwa rumba.Ilikuwa ni very simple tu ungesema unataka kuongea na boss wao basi,na uwaambie kwamba wenyewe huwezi kuongea nao,unajuwa siku zote endapo unajuwa una haki na haki haitendeki basi fanya dharau na wewe,stu.upid hao polisi hawana hata haya kabisaaa....
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums