Utendaji mbovu wa security JNIA

Utendaji mbovu wa security JNIA

Seacliff

Senior Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
158
Reaction score
152
Naomba wana jamvi nisimulie hapa mambo yaliyonitokea nikiwa naondoka Dar es Salaam kupitia uwanja wetu wa JNIA.

Ilikuwa saa tisa na dakika 45 mchana nikiwa kwenye line ya abiria wanaoondoka kwenda safari zao za nje au ndani pale pale. Kama kawaida nimekaa kwenye line nikapita kwenye office ya anayekagua passport na ticket. Ilipofika wakati wa kukagua mizigo yote tuliweka kwenye screen kama abiria wengine. Nilikuwa na sanduku moja na box moja na mfuko mmoja ambao ulikuwa bado haujafungwa. Huo mfuko ulikuwa ni unga wa sembe ya chapa Mama nilionunua Arusha.

Baada ya mizigo kupita na mimi nilipita then ikafikia wakati wa kuchukua mizigo yangu kwa ajili ya kucheki-in. Kabla sijachukua ule unga security mmoja wa kike akaniuliza, hii nini? Nikamwambia ni unga wa sembe kama ulivyoandikwa kwenye package yake hapo juu. Akaniambia kwa tone ya kufoka, "eleza vizuri usipoteze muda hapa". Nikamjibu, my sister ni unga wa ugali ninakaa mbali na Tanzania huwa nina hamu ya kula chakula cha nyumbani nikiwa huko, na ndiyo maana nimebeba huu unga. Akadakia mwingine wa kiume, "tunashaka ni drugs hii kwa hiyo ili ku test kama ni drugs au siyo drugs fungua na ukate package moja na ulambe" Nikawaambia kipimo cha drug ni kulamba? Hata hivyo mimi ndiye mshukiwa kwa hiyo unaniambia nilambe kama ni drug unadhania nitakupa jibu gani? Lazima nitasema sio drug ili nipite. Kwanza huu ni unga unapaswa kuliwa ukiwa umepikwa nikilamba mbichi nitaumwa na tumbo. Ninasafiri mbali kama masaa 15 kwenye hii flight tafadhali fikirieni na nyie. Akadakia mwingine na kusema "anatubabaisha huyu chukua pass yake nenda ku-cancel flight yake".

Mara wakaitana wengine wawili wakawa wanne. Wakaongeza polisi wengine wawili wenye uniform na vyeo vya Inspector na wawili CID. Yule dada wa kwanza akawa ameshakuja na wembe akakata ile pakti moja wakaniambia lamba haraka au tuna cancel flight yako. Wote sasa wakawa kitu kimoja wakajaza watu. Embarrassment ya ukweli.

Polisi mmoja wa uniform mwenye cheo cha inpector alikuwa mstaarabu saana akawaambia kwa kuangalia tu huu ni unga wa ugali, akaja dada mwingine naye akawaambia mnampotezea abiria muda na kazi imesimama hapa chukua hii pakiti moja pitisha kwenye machine yenyewe mumuachie aende. Wale wa kwanza kabisa na polisi mmoja wa kike mwenye cheo cha inspector wakasema no lazima alambe. Nikachotewa size ya kijiko cha chai nikalambishwa wakafurahi na kuniruhusu niendelee. Ila walichukua pass yangu wakaenda kutoa copy. CCTV camera za airport ni shahidi yangu. Naomba uongozi uangalie muda huo 15:45 hrs kwenye departure siku ya tarehe 13/9/2013.

Maoni yangu ni kuwa ikiwezekana hao wafanyakazi wachukuliwe hatua kwa sababu utendaji kama huo wa kutokutumia akili na unatia hasara nchi na kuwafanya wale watendaji wazuri waonekane pia kama hawajui wanachofanya.
 
Maafisa usalama katika viwanja vya ndege wapo kwa ajili ya kusaidia (facilitate) wasafiri kwa kuhakikisha usalama wao na wa ndege na sio harassment ya abiria. Wamefundishwa kutoa huduma hiyo na siyo kufanya kazi ya polisi. Hapo tunao hata huyo polisi pia hakupenda hizo harassment kwa abiria. Hayo ni matokeo ya incompetence ya hao maofisa waliofanya hilo jambo.

Wamefundishwa namna ya kukagua na kubaini vitu hatari kwa usalama wa abiria na ndege na sijawahi kusikia kama kuonja ni moja ya procedure waliyofundishwa. Ni udhaifu wa kiutendaji na unapaswa kumwandikia Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege.

Msafiri wa anga ana haki zake na kwa MAONI YANGU UNGEKATAA KUONJA NA KUOMBA UONANAE NA SUPERVISOR. Ni juu ya hao kuwa na procedure ya kugundua vitu kama hivyo na kama ulivyosema kama ni madawa sidhani kama ungewaambia kuwa ndio ni madawa baada ya kuonja.

Nina hakika huyu dada ameonyesha kuwa yeye au ni mshiriki wa hayo mambo na anafanya hivyo ili kukomoa wasafiri baada ya serikali kuwaijia juu hawa maafisa kutokana na baadhi yao kushiriki kkuwasaidia wasafirishajoi wa madawa ya kulevya. She acted emotionally to express her anger on the accusations being leveled against them.

Viwanja vya ndege ni biashara na inabidi tujifunze kutoa huduma ili kuvutia wasafiri wanaopita katika viwanja vya washindani wetu. Huduma na pamoja na kuhakikisha kuwa tuna usalama wa kutosha katika viwanja vyetu na kuhakikasha tuna taratibu nzuri za huduma kwa wateja wetu kuhakikisha huo usalama na sio sehemu za malumbano, unyanyasaji na jukwaa la siasa kwa wanasiasa wetu.
 
Pole sana ndugu yangu! Kwa serikali hii iliyo ozesha mfumo mzima wa utendeji, bado Tanzania tuna safari ndeeeeefu ya kubadilika.

Hivi hata kama abiria ana makosa, huu ndio mfumo au utaratibu wa kumchukulia hatua? Kwamba anapewa adhabu hata kabla ya kupatikana na makosa? Tena adhabu yenyewe anapewa na mawakala wa ukaguzi na sio chombo kilicho idhinishwa kutoa adhabu!!

Ningekuwa mimi, ningewaambia wa-cancel hiyo safari halafu ulianzishe SEBENE ili kuonyesha jamii kwamba pamoja na kuhakikisha usalama wa wasafiri lakini njia zinazotumika Tanzania si sahihi.
 
Ilikuwa ni very simple tu ungesema unataka kuongea na boss wao basi,na uwaambie kwamba wenyewe huwezi kuongea nao,unajuwa siku zote endapo unajuwa una haki na haki haitendeki basi fanya dharau na wewe,stu.upid hao polisi hawana hata haya kabisaaa....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hivi hao askari hawana mbwa,panya au mashine za kudetect madawa ya kulevya..ina maana wanatumia njia ya kulamba na kusoma packet tu.
 
Alafu kuwaonyesha haupo nyuma kisheria na sheria unazijua baada ya kukufanyia hivyo ungeomba majina yao wote kwa mkubwa wao....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Pole kaka!! lakini hii ni kawaida hapo JNIA, ma askari wote wana njaa kali sana.

Nomba hatua kali zichukuliwe kwa wahusika kwa kutumia ushahidi wa cctv au watazoea.

JNIA ni sehemu ya kuingilia na kutokea wageni hivyo kama first impression yao itakuwa mbaya then tutapoteza tourists kibao kutokana na njaa za hawa jamaa
 
'Kwa aliyekwisha umwa na nyoka hata unyasi ataugopa' na kuna wakati ukitumia common sense unaumia na yot yatokanayo hvyo ni heri lawana kuliko fedheha
 
Hicho kipimo cha kulamba aibu sana....nitawapelekea jiko la mchina wakitaka kupima kama ni sembe wapike ugali kabisa....
 
Nimesikitishwa sn na kitendo cha kumwambia Abiria alambe Unga ikiwa kama njia ya kuverify whether ni madawa au la!

Huwa inatokea kwa liquids kama maji, ambapo msafiri husika anaambiwa aonje mwenyewe maji yake ya kunywa ili aruhusiwe kuingia nayo onboard, lkn si unga!

Tangu lini binadamu anaonjeshwa unga?
Je kitengo cha madawa ya kulevya walikuwa wapi kiasi cha Security officers kufanya kazi ya ubabaishi?

Hata kama kweli yangekuwa madawa, je baada ya kuonja walitegemea huyo abiria afanyeje?...adondoke chini puuu, ndipo wabaini kwamba ni drugs?...Sumu haijaribiwi kwa kuonja bana!

Ndugu yangu na rafiki mpendwa Abdul Msangi ambaye ndiwe Manager Security wa hapo JNIA, tafadhali pitia CCTV uangalie vema tukio hilo na kujudge validity yake.

Sio lazima kumfukuza mtu kazi, lakini toeni mafunzo zaidi ya huduma bora kwa mteja kwa hao staff wa security ili wamchukulie abiria kuwa ndiye Mwajiri wao.
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta mkuu,kwa kawaida kuna mashine ya kutest unga,kulazimishwa kuonjeshwa haikuwa njia sahihi.

Ilikuwa ni kiasi cha kuchota unga kidogo na kuuingiza kwenye mashine na majibu yangepatikana hapo hapo na ungeruhusiwa kuendelea na safari. Au pia kuna vifaa vya kutestia viko kama tester za umeme(au kwa lugha rahisi screw drivers)nikiasi cha kukichukua na kukichoma kwenye mzigo unaoshukiwa na majibu yangepatikana there and then.

Lakini pia kaka kuna wakati ambapo inamlazimu mtu kulazimishwa kuonja alichokibeba ila ni katika situation zifuatazo:

1. Huwezi ukatest maji kwenye mashine na kugundua kama ni acid au any other burning chemical, ili uweze kuyatest ni lazima yaonjwe, na wa kuyaonja ni abiria mwenyewe kwani maji hayo ni ya kwake. Kama itakuwa ni kitu tofauti na maji lazima abiria atagoma kuyaonja.(hii inakuwa pale afisa mkaguzi anapokuwa na mashaka na kimiminika hicho)

2. Kuna baadhi ya watu hubeba dawa zao za kienyeji kwa ajili ya safari, hivyo basi huwezi kuzitest zaidi ya kuwaambia wazionje kama kweli ni dawa na wanazitumia, kama sio dawa za kunywa basi wanashauriwa waziweke kwenye check in luggages.

3. Endapo afisa mkaguzi kawa na mashaka na mzigo wa abiria,baada ya kuutest na kugundua kuwa sio drugs, lakini akawa na mashaka kuwa inaweza kuwa ni sumu ya aina yoyote ile ambayo inaweza kuleta madhara wakati wa safari basi atamuhitaji mwenye mzigo aonje ili kuthibitisha kuwa sio sumu. Endapo itakuwa sumu basi hata muhusika hataweza kuonja.

NB:
MARA NYINGI MASUALA YA USALAMA HAYANA FORMULAR, ILI ABIRIA AWEZE KUSAFIRI LAZIMA AFISA MKAGUZI ARIDHIKE KUWA ALIYEMKAGUA NI SALAMA KABLA HAJAMRUHUSU KUENDELEA NA SAFARI. NI SUALA LA MTU KUJIRIDHISHA.
 
Hapo JNIA panahitaji marekebisho kwa kweli...

Hivi hao viongozi/wakubwa wa hapo JNIA huwa hawatembelei viwanja vya nje kujua wenzetu wanafanyaje kazi?Uongozi hauna utaratibu wa kuwapeleka wafanyakazi wake nje ya nchi kujifunza namna wenzaoa wanavyofanya kazi?

Yaani ukitembea ktk viwanja vya nje,ukaja kutazama na cha kwetu...TUNATIA AIBU SANA...

Wafanyakazi wapo local, local tuuu, customer care ya wale security ni ovyooo, wanaombaomba tips ovyoo...sijui hata mishahara yao ikoje? Niliwahi kusikia hapa kuna AJIRA za kujuana sana.

Hebu mamlaka tupieni jicho hiyo TAA....mgeni yeyote taswira ya kwanza ni Airport...haya majamaa yanatuaibisha sana ndugu zanguni.
 
Ndugu yangu na rafiki mpendwa Abdul Msangi ambaye ndiwe Manager Security wa hapo JNIA, tafadhali pitia CCTV uangalie vema tukio hilo na kujudge validity yake.

Nasikia sio huyo Msangi...kuna mtu anaitwa sijui JUNGI au JINGU....MSANGI hayupo hapa....ukifuatlia sakata la kina Masogange utaona Manager anatajwa kwa jina hilo juu
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta mkuu,kwa kawaida kuna mashine ya kutest unga,kulazimishwa kuonjeshwa haikuwa njia sahihi.

Ilikuwa ni kiasi cha kuchota unga kidogo na kuuingiza kwenye mashine na majibu yangepatikana hapo hapo na ungeruhusiwa kuendelea na safari. Au pia kuna vifaa vya kutestia viko kama tester za umeme(au kwa lugha rahisi screw drivers)nikiasi cha kukichukua na kukichoma kwenye mzigo unaoshukiwa na majibu yangepatikana there and then.

Lakini pia kaka kuna wakati ambapo inamlazimu mtu kulazimishwa kuonja alichokibeba ila ni katika situation zifuatazo:

1. Huwezi ukatest maji kwenye mashine na kugundua kama ni acid au any other burning chemical, ili uweze kuyatest ni lazima yaonjwe, na wa kuyaonja ni abiria mwenyewe kwani maji hayo ni ya kwake. Kama itakuwa ni kitu tofauti na maji lazima abiria atagoma kuyaonja.(hii inakuwa pale afisa mkaguzi anapokuwa na mashaka na kimiminika hicho)

2. Kuna baadhi ya watu hubeba dawa zao za kienyeji kwa ajili ya safari, hivyo basi huwezi kuzitest zaidi ya kuwaambia wazionje kama kweli ni dawa na wanazitumia, kama sio dawa za kunywa basi wanashauriwa waziweke kwenye check in luggages.

3. Endapo afisa mkaguzi kawa na mashaka na mzigo wa abiria,baada ya kuutest na kugundua kuwa sio drugs, lakini akawa na mashaka kuwa inaweza kuwa ni sumu ya aina yoyote ile ambayo inaweza kuleta madhara wakati wa safari basi atamuhitaji mwenye mzigo aonje ili kuthibitisha kuwa sio sumu. Endapo itakuwa sumu basi hata muhusika hataweza kuonja.

NB:
MARA NYINGI MASUALA YA USALAMA HAYANA FORMULAR, ILI ABIRIA AWEZE KUSAFIRI LAZIMA AFISA MKAGUZI ARIDHIKE KUWA ALIYEMKAGUA NI SALAMA KABLA HAJAMRUHUSU KUENDELEA NA SAFARI. NI SUALA LA MTU KUJIRIDHISHA.
kwa kawaida vimiminika au maji unatakiwa iviweke kwenye check inn luggage , na kama ni kubeba mkononi unatakiwa ununulie hapo hapo airport kwenye duty free shop, hivyo kuondoa hatari kwa abiria na kuonjeshana. kama ni sumu iwe ya panya nk itakuaje ni threat kwa abiria? au atawanywesha kwa nguvu? na kama umeona na hivyo basi mwambie abiria aweke kwenye chek in luggage. hao pilisi walitaka tu kuonyesha mabavu yao sio vizuri kutetea hii kitu.
 
Nilipata safari ya wiki moja nje ya nchi. Kama kawaida nilikuwa na cheti cha kuthibitisha chanjo dhidi ya homa ya manjano. Ugenini sikuulizwa kama ninacho cheti hicho. Kwa mshangao mkubwa niliporejea nchini JNIA nikaulizwa kama ninacho cheti hicho. Hali hii inathibitisha jinsi wasafiri wanavyopotezewa muda wao kwa maswali ambayo si ya msingi.
 
kwa kawaida vimiminika au maji unatakiwa iviweke kwenye check inn luggage , na kama ni kubeba mkononi unatakiwa ununulie hapo hapo airport kwenye duty free shop, hivyo kuondoa hatari kwa abiria na kuonjeshana. kama ni sumu iwe ya panya nk itakuaje ni threat kwa abiria? au atawanywesha kwa nguvu? na kama umeona na hivyo basi mwambie abiria aweke kwenye chek in luggage. hao pilisi walitaka tu kuonyesha mabavu yao sio vizuri kutetea hii kitu.

asante sana kwa maelezo yakomazuri,ungalisoma ya kwangu kwa umakini zaidi nadhani ungalipata mwanga kidogo japokuwa sikueleza kwa undani zaidi na sina haja ya kufanya hivyo.labda niseme machache kidogo:

1.vimiminika vyote vinaruhusiwa kuingia navyo ndani ya ndege isipokuwa lazima ujazo wake uwe 100ml au kushuka chini.yaani kimiminika kisiwe zaidi ya 100ml,na pia visiwe zaidi ya kumi.yaan jumla ya ujazo isiwe zaidi ya 1000mls.yaani mls mia mia kila kimoja.hii haihusishi maji.ukinunua dutty free kimiminika chochote lazima kifungwe kwenye mfuko maalum unaoonyesha(plastic),uwe sealed na risiti iwemo ndani ya mfuko.

2.kwa uchache tu katika usalama wa anga kuna mambo makuu ma5 ambayo huzingatiwa:
a).unlawful seizure of an aircraft
b).sabotage of an aircraft on and off the airport
c).sabotage of an airport
d).sabotage of off airport facilities
e).terrorist attacks
matukio yote yanakuwa categorised katika vipengele tajwa hapo juu.kinachoangaliwa na wanausalama airport sio tu kuzuia ndege isitekwe au mtu asiingie na silaha au mabomu etc bali hata uwezekano wa mtu kumshambulia mtu mwingine aidha kwa silaha au acid au chochote kile kinacholeta madhara.sio kila kitu utakiruhusu kiwekwe kwenye check in luggage.imagine ndo kaweka chupa la acid bahati mbaya likamwagika unategemea nini?BRO,WITH SECURITY SOMETIMES YOU HAVE TO BE RADICAL,UKIFANYA KOSA MOJA KWA MTU MMOJA UMETEKETEZA ZAIDI YA ROHO 200 ZILIZOKO NDANI YA AIRBUS 340 YA EMIRATES.
 
Hapo JNIA panahitaji marekebisho kwa kweli...

Hivi hao viongozi/wakubwa wa hapo JNIA huwa hawatembelei viwanja vya nje kujua wenzetu wanafanyaje kazi?Uongozi hauna utaratibu wa kuwapeleka wafanyakazi wake nje ya nchi kujifunza namna wenzaoa wanavyofanya kazi?

Yaani ukitembea ktk viwanja vya nje,ukaja kutazama na cha kwetu...TUNATIA AIBU SANA...

Wafanyakazi wapo local, local tuuu, customer care ya wale security ni ovyooo, wanaombaomba tips ovyoo...sijui hata mishahara yao ikoje? Niliwahi kusikia hapa kuna AJIRA za kujuana sana.

Hebu mamlaka tupieni jicho hiyo TAA....mgeni yeyote taswira ya kwanza ni Airport...haya majamaa yanatuaibisha sana ndugu zanguni.

The MOMENT OF TRUTH.
 
Sikuzote vyombo vya usalama wanatumia zaidi nguvu kuliko akili. Na hawafikiri kwa kutumia ubongo. S.t.u.p.i.d.
 
Ilikuwa ni very simple tu ungesema unataka kuongea na boss wao basi,na uwaambie kwamba wenyewe huwezi kuongea nao,unajuwa siku zote endapo unajuwa una haki na haki haitendeki basi fanya dharau na wewe,stu.upid hao polisi hawana hata haya kabisaaa....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Yakuongea na bosi wao ni mambo ya ulaya..huku unaweza kujibiwa hayupo na ukaendelea kuchezeshwa rumba.
 
Back
Top Bottom