Utekaji Ndege ya Misri:Abiria apiga selfie na Mtekaji

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg
image.jpeg


Abiria mmoja ndani ya ndege cha "Egypt Air" alijitia ujasiri na kuomba kupiga picha na mtekaji wa ndege hiyo raia wa Misri.Abiria huyo anasema aliamua kupiga picha hiyo ili kupata kumbukumbu ya tukio la "kutekwa" kwa ndege hiyo ambayo aliamuliwa kwenda Cyprus toka Alexandria badala ya Cairo uliyokuwa ni uelekeo wake.

Mtekaji alitaka apewe nafasi ya kuongea na mkewe ambaye alikuwa Cyprus.Mpaka sasa Rais wa Cyprus anasema hawajui hasa lengo la mtekaji japo ni dhahiri sbb zake si za kigaidi
 
kuna watu humu duniani wana mambo ya ajabu sana na wanakubali lolote litokee
 
Ana kasoro gani na akina Membe/Memba walioteka ATC kwa maembe dodo manne hadi Athens Ugiriki?
Dah Mkuu rudi tena kwa ufafanuzi kidogo wengine hatuja bahatika kuona ATC ikifanya kazi ,ilitekwa mwaka gani ?
 
Wengine hatujui maana ya selfie, selfie mtu anajipiga mwenyewe au hata wakiwa wengi mmoja kati yao ndio anaipiga hiyo picha.
 
Jamaa wametokea bomba sana ila afya ya mtekaji ni dhoofu sana na anaonekana amekata tamaa ya maisha
 
Ilikuwaje mkuu?
Uzi upo humu mkuu, ila ninachokumbuka walikuwa wanne waliingia kama abiria wengine walipoanza safari wakasimama na kumwamuru pilot awapeleke Athens kile kifuko cha bank waliweka maembe manne wakawaambia abiria ni mabom walipokamatwa kufungua mfuko wakakuta maembe, waliomba wasirudishwe nyumbani kwa hiyo walifungwa huko baada ya hapo sina taarifa zao tafuta huo Uzi utaupata
 
Dah Mkuu rudi tena kwa ufafanuzi kidogo wengine hatuja bahatika kuona ATC ikifanya kazi ,ilitekwa mwaka gani ?
Namshukuru Mungu nimeziona hapo viwanja vilikuwa vidogo, ilikuwa boing 737 ikiingia Dodoma barabara inafungwa inapita barabarani hakuna magari kupita, wajanja wameua shirika na mtaji wamekula wabaaaya. kuhusu utekaji umesaidiwa hapo juu
 
Back
Top Bottom