Utekaji (kidnapping): Chatu anayeitafuna Tanzania

nenda kasome katiba vizuri.
Nadhani mnashindwa kuelewa nacho maanisha.

Katiba imetoa mwongozo mzuri wa haki za binadamu. Vitabu vya Mungu vimetoa mwongozo mzuri kabisa wa usawa baina ya binadamu.

Mashirika ya kimataifa yametoa miongozo ya usawa baina ya binadamu.


Lakini practicality haipo.... nadhani mnafikiria ki-2D ndiyo maana mnashindwa kuelewa nachomaanisha.

Haki na usawa wa kibinadamu duniani upo kwenye matamanio tu kama nyie mnavyotamani Mo angetreatiwa kama binadamu wa kawaida kama wewe.

Huenda tunavyongea hapa kuna mtu Loliondo alipotea lakini hata hatafutwi na Wizara ya mambo ya ndani. Kwanini? utajijibu.

Ok, nitaenda kusoma Katiba itasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini binadamu wote ni sawa. Ni kweli binadamu wanatakiwa wawe sawa lakini sivyo ilivyo.

Wewe na Magufuli mpo sawa? labda kwenye viungo vya kibailojia tu. Mbele ya kadamnasi Magufuli atachukuliwa binadamu wa hali ya juu kukuzidi wewe.
 

sasa hiyoo tofauti ya kutritiwa tofauti ni kuvunja sheria. everybody is equal under the law.

ndo ukapewa mifano za inchi zilizoendelea ambazo wanawatrit binadamu wote sawa pasipo kuvunja sheria.

marekan anaweza kupiga inchi fulani kisa raia wake ambae hana status yoyote.

ukianza kubadilika kimawazo siku ukiwa rais wa inchi utaleta mabadiliko tufanane na wenzetu wanaothamini raia wake wote bila ubaguzi cheo/umaarufu/utajiri.


tunachotaka ata siku moja ukitekwa wewe utafutwe kama mo anavyotafutwa.
 
Yooooo! Akili hizi ni za kikolomije kolomije. Mleta mada kachambua kwa uzuri sana hofu ya usalama wetu bila kujali tabaka zetu kimaisha, ila kwa sababu wewe ni bwanyenye flani basi umeamua ulete matabaka ktk mada isiyo na mlengo wa matabaka.
BTW, kama unamuona MO ni muhimu zaidi ya wengine waliotekwa, fine, but MO mwenyewe anahitaji hao watu wa hali ya chini ili aendelee kuwa tajiri. Sote tu wa muhimu chini ya jua hili.
 
Haya.
 
Hautanielewa kama utaendelea kufikiria hivi.
 
Mkuu Daby,binafsi nakuelewa! Lakini inapaswa kupaza sauti zaidi ili USAWA upatikane,unapotumia nguvu nyingi kutetea hoja yako kuwa hakuna USAWA unakuwa unaudidimiza USAWA tunaoutaka.
 

haba na haba ujaza kibaba sasa kibaba kimekuwa kimama.kuna mambo serekali inachukulia poa labda kwenye haba na haba
 
Ila kwa hali hii inayoendelea kupachikwa kwa Ugaidi ni rahisi sana, tena anaweza tandikwa kiongozi mkubwa wa serikalini ...
Taifa na vyombo vya usalama vikabaki vinatazamana vianzie wapi juu ya uhuni unaoendelea.
 
Ndiyo wa muhimu zaidi lakini siyo kwamba wengine wanapaswa kupuuzwa na kukejeliwa.Kwa Mfano mtu kapotea Waziri anasema huyo kaenda kutafuta maisha,hiyo si kejeli hiyo.Wakimaliza Kwao watahamia kwetu
 
Kwahiyo unaona ni halali na sawa kabisa kutekana ngoja wakuteke na wakufanyie usodoma kabisa uone raha yake
 
Kwa kweli inasikitisha kuona viongozi tuliowapa madaraka wanavyokuwa wabinafsi kutokua na huruma na roho za watu zinazoteseka kisa tu hayupo upande wao.. Nawaomba sana Hawa watekaji waangalie pia upande wa pili.. Kama wanaulinzi mkali basi wajitahidi hata shangazi zao. Tuone Kama watatoa kauli za jeuri namna hii. . Nchi imefika katika hatua mbaya ya mgawanyiko ulio wazi Baina ya chama na chama pia matajiri na masikini.. Ipo siku watajuta, Kwani wao ni nyama na mifupa Kama wengine.. Walikuwepo watesi wakubwa zaidi yao wapo wapi leo.. Inahuzunisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…